Azam TV kunani?

Rio Tinto

JF-Expert Member
Sep 18, 2014
777
451
AZAM TV Mulitangaza mtaonyesha games zote za EURO 2016 lakini mpaka sasa hatuwaelewi...game ya Switzerland hamkuenyesha...game ya Wales hamkuonyesha najua mtaonyesha game ya England na Urusi ila mngesema toka mapema kuwa mtaonyesha baadhi ya mechi na sio zote...

DSTV itabaki kuwa DSTV tu kwa uswahili huu wa AZAM TV
 
DSTV itabaki kuwa DSTV tu kwa uswahili huu wa AZAM TV
Hata mimi nimeudhika sana ijapokuwa badala yake yalikuwepo maidha mazuri sana hususan kwa mwezi huu mtukufu wa Ramadhan ila siko pamoja nawe unapo linganisha DSTV na AZAM.

Pamoja na kuipandisha chati AZAM ukilinganishana na TV nyengine ,suala la kuzilinganisha AZAM ya walalahoi na DSTV ya walalahai , sio sawa.

DSTV Compact laki moja kwa mwezi, AZAM ni robo laki, 25,000 kwa mwezi wapi na wapi?
 
AZAM TV Mulitangaza mtaonyesha games zote za EURO 2016 lakini mpaka sasa hatuwaelewi...game ya Switzerland hamkuenyesha...game ya Wales hamkuonyesha najua mtaonyesha game ya England na Urusi ila mngesema toka mapema kuwa mtaonyesha baadhi ya mechi na sio zote...

DSTV itabaki kuwa DSTV tu kwa uswahili huu wa AZAM TV
We jamaa unalipia 25000 unataka kulinganisha na wanaolipa malaki? Angalia unacholipia kinafanana na wanachokudelivia?
 
Du nini hii jamani? Kwa nini Azam mmeanza kuwa wahuni? Hii si mara ya kwsnza kujitapata mtaonesha mechi live halaf mnashindwa na wala hamuombi samahani!
 
mnapenda vya bwelele ehee! yaani mnataka kwa 12000/= muone mechi zote zaa ulaya...mtakaa sana labda msubiri Laliga...Me nshasema ntakufa na Dstv yangu...hata wafanye 500000/=ntalipa tu coz hawana mbadala..#HuuMchezoHautakiHasira
 
Tafuteni recorded zinazosupport powervu tegeni kwa muhindi nyuzi66 muenjoy mechi zote free
 
Kwa malalamiko haya juu ya azam kila siku ata juzi niliponunua king'amuzi kingine baada ya kuachana na Zuku niliamua kuchukua tu Startimes tena sasa Startimes wapo safi siyo km mwanzo
 
Kwa malalamiko haya juu ya azam kila siku ata juzi niliponunua king'amuzi kingine baada ya kuachana na Zuku niliamua kuchukua tu Startimes tena sasa Startimes wapo safi siyo km mwanzo
Mkuu nipe uhakika maana nilikuwa nataka kununua king'amuzi cha startimes
 
Back
Top Bottom