AZAM TV, ina maana wakati huu wa mvua Dar hatuangalii Tv?

barafuyamoto

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
32,377
29,738
Habari zenu!
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza. king'amuzi cha Azam hata ikinyesha mvua kidogo, kinagoma kabisa kuonyesha, yaani NO SIGNAL kabisaaaaaa!
Nafikiri teknolojia yenu hapo bado ipi chini maana DSTV ikinyesha mvua kinasua sua kama dk 3 alafu baada ya hapo kinaendelea kupeta, yaani kinakuwa kama kimezoea mvua.
Sasa cha Azam Tv ni mpaka mvua iishe kabisa. Sijajua ving'amuzi vingine vikoje, ila tafadharini rekebisheni king'amuzi chenu tuweze kuona Tv kupitia Azam tv majira yote ya mwaka!
ASANTENI.
 
Mie sio mtaalamu sana ila muonekano WA king'amuzi unachangiwa na mambo mengi. Sio kweli kwamba Azam huwa haionyeshi mvua inaponyesha, actually wakazi wa Dar hamna mvua Ile ya kulinganisha na mvua na radi ya mikoani. Suala night strength ya king'amuzi chako. Signal strength ndio kitu muhimu. Mfano natumia Azam decoder na haijawahi hata kunasa inyeshapo mvua na radi ya Tabora. Kwakuwa signal strength yangu ni over 80%. Hapo inategemea na namna ambavyo dish lako limesetiwa.
 
Mkuu KU Band lnb ni shida wakati wa hali ya hewa kama mvua tofauti na C band ambayo ina stability kubwa hata ipige mvua
 
Mie sio mtaalamu sana ila muonekano WA king'amuzi unachangiwa na mambo mengi. Sio kweli kwamba Azam huwa haionyeshi mvua inaponyesha, actually wakazi wa Dar hamna mvua Ile ya kulinganisha na mvua na radi ya mikoani. Suala night strength ya king'amuzi chako. Signal strength ndio kitu muhimu. Mfano natumia Azam decoder na haijawahi hata kunasa inyeshapo mvua na radi ya Tabora. Kwakuwa signal strength yangu ni over 80%. Hapo inategemea na namna ambavyo dish lako limesetiwa.
Asante, yawezekana! Signal yangu ni 70. Labda una point maana jirani yangu ana dstv ila wakati wa mvua anapeta tu.
 
Sio Azam tu hata dstv mvua ikianza tu ww tafuta shughuli nyingine ya kufanya
 
sasa watu Wa mbeya, Kigoma rukwa na mvua kila kukicha kuna hali gani? ...ili tukiamia mikoa Hiyo tutafute ving'amuzi vingine!
 
Azam strength yake inatakiwa iwe 70/60
Msitari wa juu usome 70 wa chini usome 60
Hapa hata ipige mvua ya namna gani ni mwendo mdundo tu
 
Mie sio mtaalamu sana ila muonekano WA king'amuzi unachangiwa na mambo mengi. Sio kweli kwamba Azam huwa haionyeshi mvua inaponyesha, actually wakazi wa Dar hamna mvua Ile ya kulinganisha na mvua na radi ya mikoani. Suala night strength ya king'amuzi chako. Signal strength ndio kitu muhimu. Mfano natumia Azam decoder na haijawahi hata kunasa inyeshapo mvua na radi ya Tabora. Kwakuwa signal strength yangu ni over 80%. Hapo inategemea na namna ambavyo dish lako limesetiwa.
Usibishe bana ni kweli Azam tv na Mvua inazingua balaa. Mi mwenyewe ni mhanga
 
Back
Top Bottom