Azam na changamoto ya Simba na Yanga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Azam na changamoto ya Simba na Yanga

Discussion in 'Sports' started by Anselm, Oct 29, 2012.

 1. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Wako watu wanaamini kuwa Azam ni team pekee inayoonekana kuleta changamoto ya kweli katika soka na kumaliza utawala wa miaka mingi wa Yanga na Simba katika mchezo wa mpira wa miguu,binafsi naendelea kuwa mmoja wa wapingaji wa kubwa wa dhana hii.
  Kwa mtazamo wangu soka la Tanzania litaendelea kucheza kwenye nafasi ya mia mbili kasoro mpaka hapo Ligi yetu itakapoundwa na team shindani za kweli, sijui lini....katika kipindi hiki ambacho Ligi yetu imejaa team zilizoundwa kwaajili ya kutengeneza njia za team nyingine tusitegemee miujiza.
  Juzi tumeshuhudia 1 ya mechi iliyonithibitishia mimi binafsi uwepo wa team zilizopo kwaajili ya team nyingine,Simba kumfunga Azam 3-1 ni evidence tosha ya hili ninaloliamini, haiingii akilini ile team iliyokuwa inasifikia kuwa na ukuta imara na kufungwa magoli ma'2 tu katika mechi 7 inageuka kuwa team yenye ukuta mbovu kuliko wa Mgambo Shooting ya Tanga,kilichonishangaza zaidi ni kutoonekana kwa baadhi ya wachezaji ambao wameshiriki katika mechi 7 zilizoruhusu magoli ma'2 tu..hivi walikuwa wapi George Owino na Erasto Nyoni....je uongozi wa Azam hauoni haja ya kumtaka Kocha wao kujieleza kwa kufanya mabadiliko yasiyo na tija alipotoka Boko ambapo badala ya kumuingiza Mshambuliaji mwingine akamuingiza Kiungo Khamis Mcha na siyo hilo tu kuchelewa kwake kufanya mabadiliko ya baadhi ya wachezaji walioonekana kufa mapema hawaoni kama kulikuwa na tatizo? iweje waliona tatizo la Stewart Hall katika mechi ambayo Azam walipoteza dhidi ya Yanga iliyokuwa katika form ya hali ya juu kwenye michuano ya Kagame? au ksbb ile ilikuwa ni Yanga na hii ni Simba?

  Bado nakumbuka shutuma zilizotolewa dhidi ya wachezaji fulanifulani wa Azam baada ya kupoteza mechi ile dhidi ya Yanga wakidaiwa kuhujumu,je uongozi makini wa wana'rambaramba hawa hawajaona element zozote za baadhi ya wachezaji kucheza chini ya viwango vyao hivyo kuhisi hujuma? au wanasubiri mechi na Yanga wakifungwa tena ndo waibue shutuma za hujuma tena?
  Hivi kuna mtu anaweza kuniambia sababu ya msingi ya Stewart kufukuzwa Azam licha ya mafanikio aliyoiletea team hiyo katika muda mfupi? kuna kitu kinataka kunijia akilini...usije kukuta Stewart alifukuzwa kwa kimbelembele chake cha kuifunga Simba kwenye robo fainali ya Kagame akajipalia makaa zaidi kwa kitendo cha kufungwa na Yanga? ,inakuwaje Kocha aliyechukua nafasi yake licha ya kufungwa mechi zote na Simba he is still in safe side na si ajabu anaongezewa mshahara, mazingira haya hayatoshi kuonyesha kuwa baadhi ya team zipo kwaajili ya kuzisafishia njia team nyingine kweli? i.e Azam kwaajili ya kusafisha njia ya Simba?
  Maswali niliyonayo ni mengi sana,nikisema niyaandike yote hapa naweza kujaza pages and pages.

  Nawasilisha!
   
 2. n

  ndomyana JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 4,732
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Juzi kulikua na bonanza hakukua na mechi
   
 3. M

  Masuke JF-Expert Member

  #3
  Oct 29, 2012
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 4,606
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Mkuu Anselm, Inferiority complex itakuua, Azam siku ile ilifungwa kihalali kabisa na wala hapakuwa na longo longo zozote; nitajibu baadhi ya claim zako ulizoweka: kuhusu Erasto Nyoni ana msiba na alikuwa safarini kwao Songea, Kuumia kwa Bocco na kuingia kwa Hamis Mcha; kwa sasa Azam ina washambuliaji wawili yaani Bocco na Mwaikimba na ina wafungaji wawili yaani Bocco na Kipre Tchetche, Mwaikimba ni mshambuliaji sawa lakini sio mfungaji kwa hiyo mbadala wa Bocco kwa siku hiyo haukuwepo hivyo kocha alikuwa sahihi kumuingiza yeyote.

  Kufungwa magoli mawili ndani ya mechi saba ni sawa lakini jiulize hayo magoli mawili yote walifungwa na Toto Africa hivyo mechi zilizobaki hawakuruhusu goli, kama Toto ambayo ni ya pili kutoka mwisho iliweza kupachika mabao mawili tena na huyo beki wako Erasto Nyoni unayemsifia akiwepo na wewe ukaona sawa kwa nini uone sio sawa Azam kuruhusu magoli matatu mbele ya timu inayoongoza ligi toka mechi ya kwanza tena mbele ya washambuliaji hatari wa ukanda wetu kina Okwi, Sunzu na Ngasa na tena bila ya huyo beki wako unayemsifia?

  Mkuu kama mlitarajia mechi dhidi ya Azam iwe ndo ngazi yenu ya kuipita Simba kajipangeni upya. Na kingine ambacho unashindwa kuelewa ni kwamba mpira ndivyo ulivyo, msimu uliopita sisi tulifungwa na Villa squad timu ambayo ilishuka daraja lakini tukaja kuwatandika mkono waliokuwa mabingwa watetezi.
   
 4. B

  Baba Kiki JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2012
  Joined: May 31, 2012
  Messages: 1,368
  Likes Received: 489
  Trophy Points: 180
  Mkuu hoja zako zimekaa kinazi mno. Kupitia maandiko yako mengi, huwa najua una upeo mkubwa lkn ushabiki unakuzidi nguvu. Hivi kwa nini huwa mnatanguliza neno hujuma kwa kila mechi? Je timu hazifungwi kwa makosa ya kimchezo au ya kimbinu? Sasa kipi cha ajabu hapa? Kwa takwimu za timu zote za ligi kuu inayoendelea sioni ajabu ya Azam kufungwa 3 -1 na Simba
   
 5. Gamaha

  Gamaha JF-Expert Member

  #5
  Oct 30, 2012
  Joined: Jul 17, 2008
  Messages: 2,695
  Likes Received: 753
  Trophy Points: 280
  Yanga mnatoka sana mapovu
   
 6. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #6
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  kama timu bigwa wa africa mashariki alitandikwa goli tatu na mtibwa ambayo sijui hata kwenye msimamo wa ligi ni wa ngapi leo unaushangaa azam kufungwa na simba na umesahau miezi michache iliyopita azam nae alitufunga idadi hiyohiyo ya magoli..nenda jangwani kawaulize okwi ni nani ndipo utakapo shangaa kwanini aliwafunga goli 2...
   
 7. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #7
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  wanasahau hata wao walichezea 5-0
   
 8. Gamaha

  Gamaha JF-Expert Member

  #8
  Oct 30, 2012
  Joined: Jul 17, 2008
  Messages: 2,695
  Likes Received: 753
  Trophy Points: 280
  ha ha kwa ujinga wao wanajifariji kuwa timu yao haikuwa sawa badala ya kukubali kuwa simba ni timu bora
   
 9. adakiss23

  adakiss23 JF-Expert Member

  #9
  Oct 30, 2012
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 3,346
  Likes Received: 655
  Trophy Points: 280
  Tatizo ni usimba n uyanga kujaa ktk miubongo ya wachezaji wa azam. Siku azam ikicheza na simba kina sureboy aggrey wanacheza kama timu ya baba yao lkn wakicheza na yanga wanatepeta sana. Same kwa humud mourad jabir azizi wakicheza na yanga wanakaza ikicheza na simba wanapotea

  Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
   
 10. n

  ndomyana JF-Expert Member

  #10
  Oct 30, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 4,732
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Kaka anselm hamna yatakacho discuss hi mijitu ya rage imekaa kinazi tuu
   
 11. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #11
  Oct 30, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Kitu kimoja ambacho nafarijika nacho sana ni kuwa licha ya kupewa majina ya kila aina na Watani zangu,wengine wananiita Mnazi wa kupindukia,wengine wananitabiria inferiority complex itaniua lkn all in all hoja zangu kama mmekuwa mkizichunguza zimekuwa zinawasaidia sana Wahusika wakuu ambao mimi huwalenga 1 kwa 1,hapa nitawakumbusha chache tu:-
  1. Nilimchana Kamwaga akasoma humu akajirekebisha,sasa hatapiki ovyo tena kwenye media.
  2. Niliandika issue ya Azam kumng'ang'ania Ngassa, faster wakamweka sokoni.
  3. Nikaandika suala la Boban kuogopwa pamoja na utovu wa nidhamu wote ambao amekuwa anauonyesha,Viongozi wa Simba wakasoma hapa wakapata somo sasa wameanza kumwadhibu.
  4. Jana tu niliandika hapa kushangazwa na jinsi Kocha wa Azam alivyowatengenezea Simba ushindi rahisi,Viongozi wake wakasoma waka'act faster.
  5. Etc, etc...
  Vitu vingi ninavyoandika hapa licha ya kuonekana ninaviwakilisha kinazi kama baadhi ya Wadau wanavyonishutumu lkn vimekuwa vikiwasaidia wahusika ambao mimi nawalenga katika kufanya maamuzi, ksbb hiyo basi vyovyote vile nitakavyochukuliwa na Watani zangu mimi sijali ilimradi Msge inakuwa delivered.
  Big up uongozi wa Azam kwa kuchukua hatua,yule Mhindi alikuwa anawazika mapema.
   
 12. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #12
  Oct 30, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Kiongozi nikukanushe kuwa eti tulitarajia mechi yenu na Azam ndo iwe ngazi yetu ya kukwea kileleni,nope....baadhi yetu mathalani mimi nilijua kabisa kwa hapa ligi ilipofikia na kwa jinsi team yenu ilivyojipanga sasa hivi ndani na nje ya uwanja nilifahamu kabisa Azam asingetoka na ushindi,labda kama mmiliki wa hiyo team si Bakhresa Swahiba Mkubwa wa Zacharia HansPop, lkn sawa Azam afungwe lkn amefungwaje? hili ndo lililonisukuma kuja na hoja hii!
  Pamoja na kwamba sisi wengine siyo makocha by proffesional lkn ukaribu wetu katika mchezo huu umetufanya tuwe na uelewa mzuri tu wa haya masuala,tukubali tukatae kwa jinsi Bonjak alivyoiongoza team yake kwenye mchezo ule ni dhahiri kabisa aliwatengenezea ushindi rahisi ambao hata nyinyi wenyewe wana Simba hamkuutegemea, mpaka leo sielewi ni kwanini alifanya vile, mwanzoni niliamini ni maagizo rasmi ya waajiri wake lkn Waajiri na wenyewe wame'mind wamempiga chini....haiingii akilini team inapoteza mwelekeo waziwazi yeye badala ya kupiga sub za maana kuokoa jahazi ndo kwanza anazidi kuidhoofisha team, is he a Coach by proffesional kweli? I doubt....ngoja sasa arudie njaa yake kule Serbia ndo atajua kuwa maharage ni mboga au mbegu
   
 13. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #13
  Oct 30, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mkuu hawa nawafahamu wala hawanipi shida,waache wabwabwaje wahusika wana'act!
   
 14. adakiss23

  adakiss23 JF-Expert Member

  #14
  Oct 30, 2012
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 3,346
  Likes Received: 655
  Trophy Points: 280
  Okwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii

  Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
   
 15. M

  Masuke JF-Expert Member

  #15
  Oct 30, 2012
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 4,606
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Hapo ndo unapopotea na mimi kushindwa kuelewa unachotaka kusema, mwanzoni uliwalaumu viongozi wa Azam pamoja na mmiliki wake kwamba walifukuza kocha wa mwanzo kwa sababu aliifunga Simba na wamiliki wa Azam ni wapenzi wakubwa wa Simba ndo maana wakatimua, jana ulisema kufungwa kwa Azam ilikuwa ni mipango ya timu nzima ya Azam kuanzia kwa mmiliki na viongozi wengine kisa tu hawataki Simba kushuka toka kileleni, leo unawasifia viongozi wa Azam kwa kumfukuza kocha wao mserbia kwa sababu alisababisha ushindi rahisi kwa timu ya Simba, yaani habari yako ni mchanganyiko tupu hata hueleweki nini unataka kusema.

  Jana nilikujibu baadhi ya hoja zako na mimi nikaweka zangu lakini hakuna uliyojibu hata moja badala yake unawapamba viongozi wa Azam kwa kumfukuza kocha wakati jana ulikuwa unawalaumu kwa unazi wao kwa timu ya Simba, kwa hiyo msimamo wako ni upi viongozi wa Azam wanaipenda Simba au Kocha ndo alitaka Simba imfunge? Kubalini tu Azam walizidiwa uwezo siku ile na tatizo lao walijiamini kwa sababu beki yao ilikuwa imeruhusu magoli machache lakini hapo hapo wakashindwa kujua wanacheza na washambuliaji wa aina gani hata wao pia wakashindwa kujua wamefunga magoli mangapi ndani ya hizo mechi nane walizokuwa wamecheza, timu inafunga wastani wa goli moja kwa kila mechi hata siku na Simba pia walifanikiwa kupata goli moja hivyo lakini tatizo tu washambuliaji waliokutana nao ndo ilikuwa dhahama kwao.
   
 16. adakiss23

  adakiss23 JF-Expert Member

  #16
  Oct 30, 2012
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 3,346
  Likes Received: 655
  Trophy Points: 280
  Chezea Mzee AkiliMali ww.. Kawambulula mashabiki wengi wa Yanga.

  Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
   
 17. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #17
  Oct 30, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Kiongozi wewe ndo unajipoteza,read between lines utagundua kuwa point yangu kuu kwenye hii thread hapo juu mpk wakati ule nilipokuwa naiandika ilikuwa ni kushangazwa kwangu kwa Viongozi wa Azam kutochukua hatua yoyote wakati uzembe wa wazi ulionekana kwa Mwalimu hali iliyopelekea team yenu kuvuna ushindi mwepesi,nikatolea na mfano namna Stewart alivyofukuzwa,kwangu mimi kumwacha Bonjak kwa upuuzi ule haikuwa sawa na ndo hapo nilipoanza kuhisi kuwa kuna mpango kuanzia juu,lkn jana hiyohiyo jioni wakatangaza kumfukuza na mimi nimewapongeza sasa kosa langu liko wapi Mkuu?
  Kubali kataa wamiliki wa Azam ni Simba damu,sasa kama matokeo yale ni maagizo yao ila wameamua tu kumtoa kafara Kocha,au Kocha alipewa fungu na yule Mhaini wenu aidhoofishe team au ndo ujuzi wake katika kuingoza team ndo umeishia pale hiyo wanajua wahusika sisi tunachojua ni kuwa ile Azam mliyocheza nayo siyo Azam tuliyoizoea kuiona toka mwaka juzi wako yule M'brazil Itamar....
  Sasa Coming back to your hoja, kuna tofauti kubwa kati ya kufunga na kufungwa wala si lazima vyote viende pamoja,team inaweza kuwa nzuri kwenye one of the two,Azam walishathibitisha ubora wao kwenye deffensive na ndo maana kabla ya mechi ya juzi walikuwa wamefungwa magoli mawili tu, je ni kweli katika mechi 8 (siyo 7) zote walizocheza hawakukutana na team yenye ma'forward wakali? je umejaribu kuchunguza ni kina nani walitumika kutengeneza record hiyo nzuri katika mechi 8? na je walijumuishwa kwenye mechi ile,kama hawakujumuishwa na ilhali baadhi yao walionekana kwenye benchi wako sawia tunapata picha gani? sawa Erasto Nyoni yuko msibani,vipi kuhusu wengine to mention few Joseph Owino,Ibrahm Mwaipopo? unakumbuka siku ile game ikiendelea nilikuambia beki 3 ya Azam ilikufa kabisa na kusababisha wote Okwi, Ngassa na Cholo kukimbilia upande ule,haya ameumia mshambuliaji Kocha anaingiza Kiungo wakati kwenye benchi kulikuwa na Washambuliaji Kipre Bolou,Mwaikimba na Zahoro Pazi.....ziko team zinazoweza kutumia viungo watupu pasipo kuwa na mshambualiaji hata mmoja na zikapata matokeo mazuri lkn si Azam na kina Jabir Azizi na Abdulhalim Humud wake,game kama ile ndo ilikuwa ya kumuingiza Mwaikiki nina uhakika angeamsha jina,yeye kaua mashambulizi na kusababisha beki ya Simba kukosa kazi ya kuokoa na kujiingiza kwenye kazi ya kushambulia,kwanini wasile 3? infact kwa kiwango kile kama ndo angekutana na Yanga iliyochanganya mwendo sasa hivi wangetimuana sana kwa shutuma za hujuma,sijui alikuwa anapiga hesabu gani yule Mzungu njaa...fikiria kiungo kilichopwaya kaja kukiimarisha mwishoni washakula 3....yule Kocha siyo bure...sasa kwakuwa kafukuzwa kama ilikuwa ni maagizo ya ma'boss wake najua atakuja kuropoka tu lkn kama lilikuwa ni fungu lililokabidhiwa kwake direct kutoka kwa yule Mkuu wenu wa usajili atakuwa anajijutia kimoyomoyo sasa hivi.
   
 18. M

  Masuke JF-Expert Member

  #18
  Oct 30, 2012
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 4,606
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Mkuu Anselm hapa tutakesha, kuna mambo ambayo hujajibu nimekuuliza kwa nini hujiulizi timu ya Azam kufungwa magoli mawili na timu ya Toto ambayo ni ya pili mwisho lakini unajiuliza sana kwa timu ya Azam kufungwa magoli matatu na timu ya Simba ambayo imeongoza ligi toka mechi ya kwanza?

  Na kingine si kweli kwamba kabla ya mechi na simba Azam ilikuwa imefungwa magoli mawili tu, ukweli ni kwamba ilikuwa imefungwa magoli matatu mawili ilifungwa na Toto na moja ilifungwa na Ruvu shooting.

  Nikukumbushe mwaka jana, hadi mechi ya 25 timu yako ya Yanga ilikuwa imeruhusu magoli 25 ambao ni wastani wa kwamba Yanga ilikuwa imefungwa goli moja kwa kila mechi lakini mechi ya mwisho na Simba timu yako ilifungwa magoli matano vipi nayo ilikuwa hujuma au kocha alificha baadhi ya wachezaji au Minziro alichelewa kufanya sub?

  Umemzungumzia Joseph Owino na hapo hapo unasema udhaifu ulikuwa ni beki wa kushoto lakini unasahau kama Owino ni beki wa kati sasa sijui hapo angeingia acheze tatu au akae katikati abanane na kina Morris na Mourad, hao wengine uliowataja sijui kama wangefanya cha maana zaidi ya walichofanya waliokuwepo, maana hata mechi zingine nane hakuna walichofanya, Azam katika mechi zake nyingi wafungaji wamekuwa ni Bocco na Tchetche na mara moja moja Morris na Humud pale inapotokea kona lakini sio Mwaikimba wala Zahoro.
   
 19. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #19
  Oct 30, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mtani hapa tutakesha kweli,natamani ingekuwa face kwa face,lkn embu nikuulize swali wewe Toto unawachukuliaje lkn? hasa wanapocheza CCM Kirumba?,kumbuka hizo goli 2 Azam aliruhusu katika mechi ambayo ilipigwa kule CCM Kirumba na matokeo kuwa droo ya 2-2 kwa akili yako unafikiria Azam kuruhusu wavu wao kutikiswa mara 2 CCM Kirumba basi ni evidence tosha ya kuwa ni wabovu?... utakwenda pale mtaani halafu tutaona uzima wenu.
  Hlf kitu kingine soka ya kisasa haipo kama unavyoichukulia ile kama mchezaji ni beki wa kati basi yeye ni kati tu,anaganda palepale kati,dogo aliyekuwa kushoto siku ile alikuwa ashazidiwa ujanja,akili ya kawaida kabisa ilibidi Moris au Murad wamsaidie lkn walikuwa hawamsaidii ile inavyotakiwa na Morad alishaonekana kuchoka sasa katika situation kama ile ndo angempumzisha Muradi na kumwingiza Owino,Owino-gere na nguvu mpya angeweza kutekeleza majukumu yote mawili katikati and @ the same time kusaidia ule uchochoro wa kina Okwi waliokuwa wanapitia,hivi akili kama hii kweli inahitaji mtu uwe na leseni ya Fifa ya u'kocha? angalia Kapombe anavyofutaga makosa ya wenzake ndo utaelewa namaanisha nini!
  Issue ya Yanga kuonekana ina ukuta mzuri lkn ikafungwa magoli ma'5 please let's not argue about it,we all know kwanini ilikuwa vile,hutaki sikulazimishi kukubali.
  Hlf issue nyingine mtani unakuwa unachemka utamlinganishaje mchezaji anayecheza kila siku na yule ambaye hajacheza hata mechi 1? ni kweli magoli yote ya Azam yanafungwa na Boko,Tchetche na Humud na 1 sijui alifunga Morris lkn ndo wanaocheza,Mwaikimba au Zahoro hawajacheza hata game 1 utawatuhumu vipi kuwa hawajafanya lolote la maana katika games za nyuma,inawezekana kweli kuwa viwango vyao vilikuwa habiwezi kumweka benchi mathalani Kiboko ya Kaseja(Boko) lkn juzi ndo aliumia kwanini hakumwingiza mmoja kati ya hawa,au wamesajiliwa kwa matumizi gani pale?
  Mtani nasisitiza mshukuruni sana yule Kocha!
   
 20. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #20
  Oct 30, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  natumai haya maelezo yanamtosha sana Anselm, sina cha kuongeza nakushuru sana Mkuu Masuke, kila la heri Simba kwa mechi ya kesho dhidi ya Polisi Moro.
   
Loading...