authentic
JF-Expert Member
- Mar 18, 2013
- 663
- 241
anzisha media house yako kisha kila mwaka watakie watu wako salam za christamass.Naona Azam Media ni kama wanajilazimisha kutoa salamu za Christmass kwa watazamaji wao, maana matangazo yao yote wanaishia kuliruka neno Christmas na kutaja heri ya Mwaka Mpya.
Binafsi naona kama wanajichosha bure tu tu sijui ni katika Muktadha wa dini yao kupingana na shamra shamra za Christmass maana Jingle wanatumia za Christmass ila kulitamka wanapata kigugumizi.
Nawasihi Azam Media wajikite katika kuheshimu imani za watazamaji wao wote maana wao wamejitanabaisha kama Media isiyo na udini lakini kwa ndani wana itikadi za kidini kwa kubeza dini moja na kuheshimu imani moja pekee.
Azam Media Badilikeni, tambueni kuna Great Thinker tunawafuatalia kwa karibu pamoja na maudhui yenu.