Azam Media kipindi cha alasiri ni aibu kubwa, fanyeni kitu haraka

CarloJesus

JF-Expert Member
Nov 5, 2019
431
833
Maudhui ya kipindi kiujumla yalilenga kutuhabarishana habari mbalimbali za uchumi,siasa, Jamii na burudani ndani na Nje ya mipaka ya nchi yetu.

Nyingi za habari hizi zimekua muhimu na nyeti kama taarifa za Serikari kutoka kwa viongozi wetu kwa umma.

Niseme tuu uwasilishaji wa kipindi hiki na watangazaji wake, kama kweli hawa ndo wamesomea habari Ile mnaita "Junalizimu". Basi ni aibu kubwa na mnachafua brand.

Hakieleweki kama huwa wanapiga soga, wanachofanya (maana nako wanafeli) ,au ni comedians, na mbaya zaidi kote huko huwa wanakuwa kama vituko.

Walau segment ndogo ya michezo ya ndugu Zuberi inakuwa sawa.

Kwanini msimchukue Raymond wa kipindi ha saa sita hadi saa saba, mbona huwa anafanya vizuri, sio hao watoto hapo.

Vinginevyo hamjali professionalism na mnakumbatiana kindugu ndugu.

Hivi hili nalo mpaka wataalamu waliosomea habari walione.

Sina wivu, ni mtazamo huru kabisa kutaka kuboresha zaidi kwa michango ya sisi walaji wenu

Ukiachilia mbali ujumbe unaolalia upande mmoja, mbona TBC wanawashinda namna ya kuwasilisha habari?

Yaani siku hizi ukifungua redio badala ya kukutana na habari, unakutana na soga wanazopiga watu redioni au kwenye TV.

Hivi hamuwezi kujifunza kwa Idhaa za Kimataifa kama BBC, Idhaa ya Ujerumani, Ifaransa na China.

Mbona wanatumia nusu saa tu na bado tunapata habari murua gena katika uwasilishaji mzuri kabisa.

Azam media mmewekeza sana katika miundombinu vizuri, tahadhari tupeni jicho katika rasilimali watu pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kipi kizuri ITV zaidi ya kipindi cha saa 20:00-20:58?? Ukilinganisha na TV zingine kama Clous, Azam TV E n.k

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu uko nyuma Sana...ITV Wana vipindi vingi na makala za kuelemisha Kama usalama wa barabarani,Kilimo ,viwanda....big up pia kwa TBC kwa makala nyingi nzuri za kiuchumi ukiacha habari zao kujipendekeza za kichama

Hayo ma cloudts na tveee hakuna Cha maana zaidi ya nyimbo tuu Tena nazo hawaji na kitu tofauti kama kumchimba msanii , history zao nk

Hebu fuatilia kipindi Cha Country music TBC jpili asubuhi uone tofauti

Michezo kadhalika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
sagaciR,
Kupanga ni kuchagua, huko sijaona cha zaidi na ndio sababu ITV ni SUPERBRAND AFRIKA MASHARIKI.
 
Back
Top Bottom