Azam imesikitishwa kufukuzwa Kwa Robertinho

Labani og

JF-Expert Member
Sep 15, 2020
15,783
24,215
Klabu ya Azam Fc imesikitishwa na kitendo cha Klabu ya Simba Sc kufikia makubaliano na aliyekuwa Kocha wao Roberto Oliveira maarufu kama Robertinho aliyepewa mkono wa kwaheri mchana wa leo

Akizungumza na Kishamba Media, Afisa Habari wa Azam Fc, Hasheem Ibwe, amesema wao kama Azam kuelekea kwenye mchezo wao dhidi ya Simba Sc walikuwa wanamtaka kocha huyo aendelee kuwepo kwa kuwa wamezoea kuchukua alama tatu kwake huku akionyesha kusikitishwa na kuondoshwa kwa kocha huyo

Ibwe ameongeza kuwa bado kwa sasa Azam Fc ipo kwenye safari ya kuusaka ubingwa wa ligi kuu soka Tanzania Bara 2023/2024 ambapo ameweka bayana kuwa bado wana imani na kocha wao Yusuf Dabo na kwamba hawana mpango wa kuachana na kocha wao

#KishambaUPDATES

1699422089608.jpg
 
Back
Top Bottom