Azalishwa watoto 17 kimiujiza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Azalishwa watoto 17 kimiujiza

Discussion in 'Jamii Photos' started by MziziMkavu, Nov 18, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Nov 18, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Chausiku, mkazi wa Kijiji cha Imbasemi, Arumeru mkoani hapa, amejifungua watoto 17, na wakati huohuo hivi sasa ana ujauzito wenye “umri” wa mwaka mmoja na miezi miwili. Katika kuzaa watoto hao, Chausiku hana maelezo ya jinsi mimba zinavyoingia tumboni kwake na anasisitiza kwamba ni muda mrefu hajashirikiana na mumewe kwenye tendo la ndoa. “Sifanyi tendo la ndoa na mume wangu, yeye mwenyewe ananiogopa hasa baada ya kuona mimba zinaingia kimiujiza, anasema nina pepo ambalo linanipa mimba,” alisema Chausiku na kuongeza:
  <!--ThumbBegin-->[​IMG]<!--ThumbEnd-->
  “Nashangaa kwa sababu tangu tumeacha kushiriki tendo la ndoa na mume wangu, nimepata watoto 12, hao wote wamepatikana pasipo mimi kufanya tendo, ingawa wote wanafanana na mume wangu.” Kutokana na hali hiyo, Chausiku alisema kuwa mara kwa mara huwa anafikiria kujiua kwa sababu haoni faida ya kuishi, zaidi ya kugeuka chombo cha mateso kwa kubeba mimba za kiumbe asichokifahamu.

  Akizungumzia tukio zima, Chausiku ambaye asili yake ni Mkoa wa Tabora, alisema kuwa awali aliishi na mume wake, Elidaima Kimoso, na kupata watoto watano bila kushtukia hali hiyo kabla ya kuamua kuacha kushirikiana naye kindoa. Alisema kuwa maajabu zaidi yalikuja baada ya kuona mimba zinaingia mara kwa mara na anajifungua watoto wakiwa salama, wakati hakuwa akiingiliana na mwanaume yeyote.

  Kutokana na hali hiyo, Chausiku alisema kwamba kuna wakati alilazimika kwenda hospitali ambako madaktari hawakuona tatizo lolote. “Kuna wakati nahisi nimechezewa kwa sababu kuna ndugu yangu mmoja niliwahi kuhitilafiana naye lakini yeye kwa hasira akanitamkia kwamba nitazaa mpaka nakufa. Mwanzoni nilidharau kauli yake hiyo lakini hivi sasa naanza kuifikiria kwa makini,” alisema.

  Aliendelea kusema kwamba wakati anapopata ujauzito amekuwa akipatwa na matatizo makubwa, yakiwemo yale ya kutokwa na damu nyingi sehemu za siri na maumivu makali ya mwili. “Kwa kweli mimekata tamaa kabisa ya kuishi hapa duniani; nafikiria hata kujitupa barabarani ili nigongwe na gari nife, niondokane na haya mateso ninayoyapata maana sijui yataisha lini!” alisema.

  Hata hivyo, Chausiku alisema kuwa miongoni mwa watoto 17 aliojifungua, 14 ndio wapo hai, wakati watatu ni marehemu. Alisema, mimba tano za mwanzo wakati akishirikiana tendo na mumewe, hazikuwa na matatizo, kwani alijifungua kila alipotimiza miezi tisa lakini kwa zilizofuata, nyingi zimefikisha zaidi ya miezi 14 mpaka 24 yaani miaka miwili.

  Alisema kuwa, maajabu mengine ni pale anapojifungua ambapo kitu kingine kigumu hubaki tumboni na inapopita miezi minne kitu hicho huwa mimba kamili, hivyo wakati akiendelea kumnyonyesha mtoto aliye naye, mtoto huyo huanza kuharisha. “Nalazimika kununua maziwa ya ng’ombe maana mtoto akishaanza kunyonya baada ya siku chache anaanza kuharisha mfululizo. Kila nikiwa nanyonyesha huwa nahisi dalili za ujauzito tumboni,” alisema na kuongeza:

  “Kila ninapohisi hali hiyo huwa nakwenda hospitali lakini nikiwaeleza madaktari, wenyewe hubaki kunishangaa kwamba hawaoni chochote.” Kwa upande wa mume wa Chausiku, Elidaima, ambaye ni mfanyabiashara ya kuuza maji alisema kuwa alifunga ndoa na mkewe mwaka 1980 katika Kijiji cha Samanga, Moshi, Kilimanjaro, lakini amesitisha kushiriki naye tendo la kijamii baada ya kuingiwa na hisia kwamba anaingiliwa na pepo linalompa ujauzito.

  “Ndugu mwandishi mimi kwa sasa nimemwachia Mungu, nimetumia fedha nyingi sana kubaini tatizo la mke wangu lakini mpaka sasa bado linaendelea,” alisema na kuongeza: “Nina zaidi ya miaka 10 simjui mke wangu lakini watoto wanaongezeka.”

  Elidaima aliwataja watoto wao kwa majina kuwa ni Mwanjaa aliyezaliwa mwaka 1980, Tano (1982), Julita (1984), Petro (1986 lakini amekwishafariki), Kapundola (1988, amefariki) na Paulo (1990). Watoto wengine ni Hassan (1994), Joshua (1997), Robert (1999), Pastory (2000), Samuel (2001), Gabriel (2003), Agnes (2004), Valentine (2006, amefariki) na Hilda (2007).

  Elidaima alisema kuwa kwa sasa anaishi na watoto wanne tu, kwani wengine wamechukuliwa na Wasamaria wema kwa ajili ya kumtunzia kwa sababu yeye ameshindwa kumudu gharama za kuwalea. Aliongeza kuwa kwa sasa anaishi katika nyumba ya kupanga yenye chumba kimoja ambayo haina ubora, ndiyo maana anashindwa kumudu kuwalea watoto hao, hivyo kuruhusu wachukuliwe na watu wengine.

  Kwa mujibu wa uchunguzi wa mwandishi wetu, maisha ya Chausiku na familia yake ni ya taabu na kwamba kuna haja ya kumsaidia. Gazeti hili linatoa wito kwa yeyote anayeguswa kumsaidia Chausiku na familia yake, kupiga simu namba 0714 895 555 ili kupokea maelekezo.
  http://www.globalpublisherstz.com/2009/11/03/azalishwa_watoto_17_kimiujiza.html
   
Loading...