Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,618
- 9,610
Kiongozi wa juu kabisa nchini Iran Ayatollah Ali Khamenei ameiita Israel kuwa sio taifa, bali ni ngome ya kigaidi huku akiyataka mataifa ya Kiislamu kupambana nayo, katika wakati wanapoadhimisha siku ya maandamano ya kuwaunga mkono Wapalestina.
Ayatollah Khamenei ametoa matamshi hayo wakati kukiwa na wasiwasi kati ya mahasimu hao wa kikanda, kufuatia lawama za Iran dhidi ya Israel kwamba ilifanya mashambulizi mfululizo ya majini, ilikishambulia kinu chake na kumuua mwanasayansi mwandamizi wa Iran.
Kiongozi huyo wa Iran amesisitiza kwamba anguko la utawala wa kizayuni umekwishaanza na ametoa mwito kwa Wapalestina kuendelea kupambana na amezihimiza serikali za Kiislamu kuwasaidia.