AY: Hakuna Rapa mkali Tanzania zaidi ya Joh Makini

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
AY%20na%20Joh.jpg


Rapa AY amefunguka na kusema kuwa toka mwaka 2006 mpaka sasa hakuna rapa ambaye ameibuka na kuwa mkubwa zaidi ya Joh Makini.

AY amesema hayo kupitia kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio na kudai kuanzia mwaka 2006 baada ya Joh Makini kuingia kwenye kundi la 'A list' ya rapa wazuri bongo hakuna rapa mwingine ambaye ameingia kwenye kundi hilo, ila amesema wapo rapa wamekuwa wakijitahidi lakini wanaishia 'B, C na D list' ya rapa wakali bongo.

"Toka mwaka 2006 hakuna rapa amekuwa mkubwa zaidi ya Joh Makini hapa bongo, wapo wanajitahidi lakini wengi wanaishia 'B, C na D list' hata Roma Mkatoliki ni rapa mzuri anajitahidi, lakini natoa ushauri tu kuwa rapa tunatakiwa kuongeza nguvu ya kujitangaza na kazi zetu, maana unaweza kuwa unaweza sana lakini bila kujitangaza huwezi kuonekana" alisema AY

Mbali na hilo AY alitoa ushauri tena kwa wasanii wa hip hop Bongo na kuwataka kutengeneza brand zao na kazi zao kwa kutafuta 'interview' mbalimbali na watu mbalimbali ndani na nje ya Tanzania ili kuongeza wigo wao na kutanua mipaka ya kazi zao.

"Unajua hata rafiki yangu Fid Q nilishawahi kumwambia hata kama wewe ni mkali na unajijua ni mkali sana kitu kikubwa unachohitaji ni kujitangaza , hivyo rapa tunahitaji kujitangaza sana na kutangaza kazi zetu, tujaribu kutafuta Interviews mbalimbali, nataka kuona rapa wetu mwaka 2017 wanashiriki matamasha makubwa, wajiongeze nina uhakika tutafanya makubwa zaidi" alisema AY
 
Had a spark when you stared but now you're just garbage/ Fell from 'Top 10' to 'not mentioned at all'"...Jay Z
 
Hamujaelewa kamanisha kuanzia mwaka huo wasanii wachanga ambao wametoka hakuna wa kumuzid siyo kwamba ndo rapa mkali kuzid wote nchii hii tangu huo mwaka
Mkuu nadhani ww ndio ujamuelewa kama ni hivyo a ngetaja wasanii walioanza na John tu hasingemuweka ngosha maana niwa kitambo sana
 
Joh makini yupo vizuri sana huo ndio ukweli kundi la weusi pia wanajitaidi ukisema anabebwa sielewi anabebwa kivipi
 
Joh Makini ana bebwa, tuwe wa kweli, japo sina maana kuwa hana uwezo kabisa.
Hakuna msanii anayebebwa siku hizi,kuna platform nyingi sana wasanii kusambaza kazi zao wanaolalamika anabebwa wameshindwa kubadilika na mahitaji ya mashabiki
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom