Mwanzo Shiza
Member
- May 21, 2018
- 79
- 36
Siku za hivi karibuni ndugu yetu Dadi Mohamedi (49) na Omary Burian(27) wamekutwa na mkasa wa kuibiwa wakiwa wanasafiri kutoka Dar Mtwara na basi la Zungu. Imeelezwa kuwa waliibiwa vitu vyaombalimbali baada ya kula biscuti zinazoaminika kuchanganywa na madawa ya kulevya. Vijana watatu wanaodaiwa kuhusika na tukio hilo wamekamatwa na jeshi la polisi mkoa wa Lindi. wanaendelea na mahojiano. Na ndugu zetu waloibiwa wanaendelea na matibabu katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Lindi (Sokoine). Kaimu mganga mfawidhi wa hospitali hiyo ameeleza kuwa afya zao zinaendelea vizuri. KWA TUKIO HILI TUJIFUNZE KUTOPOKEA NA KULA CHAKULA CHA KUPEWA NA WASAFIRI WEZETU.