Awamu ya tatu ya mgomo wa madaktari 23 June, 2012

Jackbauer

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
6,038
2,199
Baada ya kushuhudia migomo ya madaktari kwa awamu mbili na baadaye kufuatiwa na majadiliano yalioyoisha hivi karibuni sasa kuna kila dalili ya kutokea kwa mgomo mwingine mara itakapofika tarehe 23 juni 2012.

migomo miwili ya kwanza ilipuuzwa hivihivi lakini mwishowe tuliona viongozi wakuu wa nchi wakirudi nyuma na kuomba huruma ya mazungumnzo.

Je, iwapo mgomo wa tarehe tajwa utatokea ni nani alaumiwe kwa kushindwa kutatua mgogoro huu uliodumu kwa kipindi cha nusu mwaka sasa??


haya ni ya morogoro

TAARIFA KWA UMMA
Katika kikao cha madaktari na wahudumu wa afya Ifakara kilichofanyika tarehe 16.June 2012, Kwa pamoja kilikataa taarifa iliyotolewa na serikali kuhusu madai ya Madaktari na Wahudumu wa Afya. Kikao kilitoa maazimio yafuatayo
1. Tunasikitishwa na msimamo wa serikali kutokuonyesha lengo la kutatua madai ya madaktari na wahudumu wa afya.
2. Tunatangaza mgogoro rasmi dhidi ya serikali kuhusiana na madai yetu kudharauliwa na kutofanyiwa kazi.
3. Tutaungana na madaktari na wahudumu wengine wa afya Tanzania katika mgomo utakaoanza tarehe 23 Juni 2012. Kama Serikali haitafanyia kazi madai yetu
4. Tunaukumbusha umma kuwa serikali ilikuwa na muda wa kutosha kufanyia kazi na kutatua madai ya madaktari na wahudumu wa afya
haya ni ya BUGANDO


TAMKO:
Kutokana na kikao cha tarehe 15/06/2012 hapa Bugando na kanda ya Ziwa kwa ujumla tunatamka kwamba:-
1. Hatukubaliani na namna serikali ilivyo- na inavyoshughulikia suala la madaktari na wahudumu wengine wa afya hapa nchini.

2. Ni vema serikali itoe tamko lenye tija juu ya mgogoro unaondelea kati yake na wafanyakazi wa sekta ya afya nchini

3. Tutaungana na madakrai wote pamoja na wahudumu wengine wa afya katika mgomo utakaonza tarehe 23/06/2012 ikiwa hatua madhubuti na zenye tija hazitachukuliwa

Mungu Ibariki Tanzania Mungu Ibariki Afrika


na haya ni ya Dodoma karibu kabisa na mjengoni
TAMKO LA MADAKTARI NA WAHUDUMU WA AFYA DODOMA
Baada ya kupata muda wa kupitia na kuchambua kwa kina ufafanuzi wa serikali kuhusu madai ya madaktari. Madaktari na wahudumu wa afya Dodoma tunapenda kutoa tamko kama ifuatavyo

1. Tunaunga mkono maamuzi ya kikao cha madaktari na wahudumu wa afya cha tarehe 9/06/2012 kwa kuukataa ufafanuzi wa madai ya msingi kwani hauna nia ya dhati wa kuleta suluhisho la kudumu katika sekta ya afya. Hivyo tupo katika mgogoro na serikali na tutaungana na wenzetu katika mgomo utakaoanza tarehe 23/06/2012.

2. Tunaitaka serikali iache mara moja jitahada zake za kutugawa wahudumu wa sekta ya afya kwani kwa kufanya hivyo kutadhorotesha ufanisi wa utoaji wa huduma za afya katika hospitali mbalimbali nchini. Hivyo tunaitaka serikali ianze mara moja kuwalipa wahudumu wote wa afya posho mpya za kuitwa kazini.

3. Tunawaomba wahudumu wa afya wote na popote walipo kuendelea kuwa pamoja katika kutetea huduma bora na maslahi mazuri katika sekta ya afya.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.

updates;mahakama kuu divisheni ya kazi imetoa zuio la mgomo huu.
madaktari washikilia msimamo wao na baadhi yao kusema
"BASI NASISI HIYO TAARIFA YA SERIKALI TUNAICHAMBUA KWA KINA ,TUNAIFANYIA MPANGO MKAKAKATI KABAMBE,TUNAISHUGHURIKIA,TUTAIFANYIA UPEMBUZI YAKINIFU MBALI NA HAYA MGOMO UKO PALEPALE''

SIKU YA KWANZA
hospitali kadhaa zimeingia kwenye mgomo ikiwa ni pamoja na Bugando,Muhimbili,Mbeya na Amana.
bado ni vigumu ku-assess makali ya mgomo hasa ukizingatia leo haikuwa 'siku ya kazi' tusubiri siku ya jumatatu ambayo ni siku inayohudhuriwa na wagonjwa wengi.

SIKU YA TATU

Mbeya,Bugando,Muhimbili,Dodoma,amana,KCMC,mwananyamala,TMK,ifakara, wako kwenye mgomo.
kuna tetesi kuwa Ocean road wako mbioni kujiunga.
Vyombo vya habari mbalimbali vyaanza kuripoti madhara ya mgomo huu.baadhi ya waandishi wakataliwa kuingia hospitali ili kuhabarisha wananchi juu ya mgomo.
Channel ten yafanya mjadala na madaktari.madaktari wajieleza vizuri kwa nini wamefikia hatua hii.kesho tutegemee mgomo kuwa mkali zaidi.

SIKU YA NNE
Mgomo bado unaendelea katika sehemu tajwa hapo juu.pia kuna taarifa kuwa hospitali ya hydom imeingia rasmi kwenye mgomo.
waziri wa afya amekwepa kufanya mahojiano ya 'live kupitia star TV' ili kujibu madai ya madaktari.katika kipindi hicho kulikuwepo wawakilishi wa madaktari na wajumbe wa kamati ya bunge huduma za jamii.Mwinyi aliomba udhuru kwa kusema kuna mambo muhimu uanayashughulikia.
huko bugando mkurugenzi wa hospitali anaelekea kurudia kosa lililofanywa na mkurugenzi mwenzake wa Muhimbili kwa kutishia kuwarudisha intern doctors wizarani.tukumbuke kosa hili ni moja ya chanzo cha mgomo huu unaoendelea mpaka leo.

SIKU YA TANO
Kiongozi wa jumuiya ya madaktari Dr Ulimboka steven atekwa na kupigwa hadi kupoteza fahamu.
Madaktari waapa kuongeza mgomo.
Mh pinda kutoa tamko la serikali kesho.

SIKU YA SITA

Afya ya dr ulimboka yaanza kuimarika,asema bado maumivu ni makali!
Pinda akataa kutoa tamko.
mgomo unaendelea huku kukiwa na ripoti ya madaktari bingwa wa MNH wamejiunga katika mgomo

SIKU YA SABA
Hali ya ulimboka si nzuri sana
madaktari bingwa wa MNH,MOI,MUHAS,ORCI, Wametoa tamko rasmi la kujiunga kwenye mgomo.
nawasilisha...
 
duh..tujiandae kzikana tena..ila komaeni mpaka mpewe chenu mbona wao wanachukua chao na hata kisicho chao??
 
naendelea kutafuta updates za matamko kutoka mikoa mingine.nikiyapata nitayarusha.
naona hii movie imefikia patamu.probably hii itakuwa season ya mwisho!
 
Once again, nasimama upande wa madaktari. Na tutawashangaa wale ambao watasema madaktari wameharakisha na wasubiri "serikali ifanyie kazi madai yao"! Serikali hii haiwezi kwenda isipokuwa kwa kulazimishwa. I support the doctors and other health workers in the country!
 
Once again, nasimama upande wa madaktari. Na tutawashangaa wale ambao watasema madaktari wameharakisha na wasubiri "serikali ifanyie kazi madai yao"! Serikali hii haiwezi kwenda isipokuwa kwa kulazimishwa. I support the doctors and other health workers in the country!

atiiiiii,,,,,,,jaman,jaman......
 
Raisi mdhaifu,wabunge wa magamba wapuuzi wanaongozwa na uchizi. Mjinga akiongoza werevu wengi nini kitatokea. Ndio haya.
 
Kama majadiliano yalikuwa yanafanyika kwa siri, hatuwezi kujua nini zilikuwa contents za makubaliano hayo na for the same reason it doesnt make sense kuunga mkono mgomo. Kwanza madaktari walete details za majadiliano yao na serikali. Wamejadili nini, wameshindwana wapi?
 
nitawapa updates za matamko kutoka sehemu mbalimbali.
mzaha mzaha hutumbua usaha!!
 
Kama majadiliano yalikuwa yanafanyika kwa siri, hatuwezi kujua nini zilikuwa contents za makubaliano hayo na for the same reason it doesnt make sense kuunga mkono mgomo. Kwanza madaktari walete details za majadiliano yao na serikali. Wamejadili nini, wameshindwana wapi?
details za mazungumzo hazitosaidia kwa sasa.kimsingi maombi yote ya madaktari yametupwa,hata green cards za bima ya afya,chanjo n.k
 
Please doctors this time iwe kweeeli kabisa! Safisha njia ya fani zingine kuongezewa malipo. Kudos
 
Back
Top Bottom