Awamu hii dili za kununua magari ya Serikali (TOYOTA) na pikipiki zimekuwa nyingi sana. Wahindi watatumaliza

Sir John Roberts

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
9,653
16,003
Nimeshtushwa na kasi ya Serikali ya awamu ya 6 ya kuagiza magari kupitia wakala TOYOTA TANZANIA LTD ambayo ipo chini ya familia ya Karimjee kwa wingi sana ndani ya muda mfupi.

Kupitia ofisi za wakuu wa mikoa RCs serikali imenunua LC 300 series ambazo ni latest (kumbuka hawa wakuu wa mikoa walikuwa na magari LC GX V8 ), idara za TASAF wameletewa LC hardtop hii ni kwa nzima (hapo kabla zilikuwepo Land-rover defender), wakuu wa idara za elimu Toyota Hilux double cabin, wakurugenzi wa halmashauri GX V8 idara za serikali, Mawaziri na Ofisi ya rais sijagusa.

Tuhamie kwenye pikipiki Wakala Mohamed Dewji ameingiza boxer hapa nchini tunaambiwa za kilimo mpaka sasa nyingine zinafanya biashara ya bodaboda na nimesikia watendaji wa kata na vijiji nao wameagiziwa.

Sasa jamani hoja yangu ni kuwa hizi ni biashara hawa wahindi wanazitafuta huko Serikalini kwa kushirikiana na viongozi lakini tujiulize je kweli kipaumbele cha Serikali kwa sasa ni magari na pikipiki?

Je magari yaliyopo na pikipiki zilizopo haziwezi kutuvusha kipindi hiki? Mama Samia sijui kama upo humu JF lakini nakuomba wakufikishie ujumbe hawa maajenti wa kihindi mkicheka nao wataifilisi hii nchi. Jamani tuwe wazalendo kidogo tufanye yale ya msingi sisi bado ni nchi masikini.

Ni hayo tu kwa leo.
 
Back
Top Bottom