Rais wa klabu ya Simba Evans Aveva anashilikiwa na jeshi la polisi

Nyenyere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
14,769
10,650
Taarifa zilizothibitishwa ni kwamba kiongozi huyo wa Simba FC Aveva anashikiliwa polisi urafiki kwa tuhuma za rushwa. Anashikiliwa na TAKUKURU tangu juzi kwa tuhuma za rushwa. Hakuna ufafanuzi zaidi uliotolewa baada ya polisi na TAKUKURU kugoma kufafanua zaidi kwa sababu uchunguzi bado unaendelea.



Chanzo: Efm radio

==================

UPDATES:



Taarifa zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii zinadai kwamba, Rais wa klabu ya Simba Evans Aveva anashilikiwa na Jeshi la polisi kwenye kituo cha Urafiki.

Aveva anashikiliwa na Polisi kwa bibali cha Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa TAKUKURU lakini bado haijafahamika moja kwa moja anakabiliwa na tuhuma gani.

Kamanda wa Mkoa wa kipolisi Kinondoni, ACP Chistopher Fuime amethibitisha kumshikilia rais wa klabu ya Simba na alipoulizwa ni tuhuma gani zinazomkabili kiongozi huyo wa juu kabisa wa wekundu wa Msimbazi alisema ni vizuri swali hilo wakiulizwa TAKUKURU.

“Kama unaweza labda ungewauliza watu wa TAKUKURU wanaweza wakajua ni lini uchunguzi wao utakamilika ni lini watampeleka mahakamani. Sisi tunamshikilia kwasababu TAKUKURU hawana mahabusu binafsi, vinginevyo wangekuwanae kule na wangejibu maswali yote ambayo wananchi wanataka kujua,” amesema Foibe kamanda wa Mkoa wa kipolisi Kinondoni wakati anahojiwa na kituo kimoja cha radio cha jijini Dar es Salaam.

“Tunamshikilia, yupo kwenye mikono salama. Sisi tunaendelea na uchunguzi wetu, sheria inaturuhusu kufanya uchunguzi tunaruhusiwa kukamata, kupekuwa kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu,” amesema Musa Milaba afisa habari wa TAKUKURU.


Chanzo: Shaffih Dauda

===============

UPDATES;

Asubuhi ya August 4 2016 taarifa zilianza kusambaa katika mitandao ya kijamii kuhusiana na Rais wa Simba Evans Aveva kutiwa mikononi mwa Polisi kutokana na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) kuagizwa
kukamatwa kwa kiongozi huyo.

Millardayo.com ilifuatilia kwa kina kuhusiana na taarifa hizo na kufanikiwa kumpata kaimu afisa msemaji wa TAKUKURU Tunu Mleli na kuweka wazi kuwa kilichomfanya Rais wa Simba kukamatwa ni tuhuma za uchepushwaji wa pesa za usajili za mshambuliaji wa zamani wa klabu hiyo Emmanuel Anord Okwi kwenda Etoile du Sahel ya Tunisia.

“Ni kweli Aveva amekamatwa na polisi baada ya TAKUKURU kuagiza hivyo kutokana na tuhuma za rushwa zinazomkabili, tuhuma zinazomkabili ni uchepushwaji wa fedha kutoka account ya Simba kwenda katika account yake na baadae kuanza kufanyiwa mgawanyo katika account nyingine, ni fedha za usajili wa Okwi kutoka Etoile du Sahel”

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Emmanuel Okwi aliuzwa na Simba mwaka 2013 na kujiunga na klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia kwa ada ya uhamisho wa zaidi ya Tsh milioni 450, malipo yalicheleweshwa kulipwa hadi FIFA walipoingilia kati na mwaka huu malipo ndipo yalikamilika.
 
Rais wa Simba, Evans Aveva anashikiliwa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru).


Taarifa zinaelezwa kuwa Takukuru wanamshikilia Aveva kwa tuhuma za rushwa ingawa haijaelezwa ni tuhuma zipi.


Msemaji wa Takukuru, Mussa Misalaba amethibitisha kukamatwa kwa Aveva ambaye kweli anashikiliwa.

"Hii ni kazi yetu, tunaendelea kuifanya na niwahakikishie kuwa yupo katika mikono salama kabisa," alisema.

Habari za uhakika zinaeleza, Aveva amekamatwa jana na amelala katika moja ya vituo vya polisi jijini Dar es Salaam.
 
simba sc wanaumizana wenyewe !! Evans aveva ajirudi tarudi akubali kukaa Mesa moja na Michael wambura pasipo kufanya hivyo atazidi kuangukia PUA Mara kwa Mara.
 
Mikono ambayo sio salama ni ipi? hawa wanaojiita mikono salama si ndio hao hao tunaowalalamikia kila siku??
 
engine rock

Aveva ni kiongozi wa kijamii na vyema wanajamii tukafahamu kulikoni sababu za kushikiliwa na TAKUKURU. Unajua kwenye eneo la michezo kumekuwepo na tuhuma za rushwa, ubadhilifu au matumizi mabaya ya ofisi.


Mimi sielewi mambo haya ya sheria lakini kwa mtu ambaye anaongoza taasisi inayotambulika ni tofauti na 'vibaka' wa kawaida. Si ni pale uchunguzi ukikamilika ndio anakamatwa, kuhojiwa na kupelekwa mahakamani!?

Mfano akina Mh. Lugola walituhumiwa na kupelekwa mahakamani (nadhani ilikuwa ni baada ya mahojiano ya kina) na kesi imeenda leo nimesoma kuwa DPP amewafutia mashitaka.

Sasa chukulia tangia siku ya kwanza walipotuhumiwa wangelikamatwa na kuwekwa ndani, kwanza serikali ingelikuwa imeingia gharama kubwa kuwalinda na kuwahudumia watu watatu pia familia na jamaa zao wangelikuwa wamekwazika kisaikolojia na kiuchumi! Au ana tuhuma kubwa ambazo ni hatari kwake kuwa nje!?
 
Back
Top Bottom