Auza Figo Yake ili Kununua Simu ya iPhone

Auza Figo Yake ili Kununua Simu ya iPhone

kilimasera

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2009
Posts
3,068
Reaction score
277
Kijana mmoja mwenye umri wa miaka 17 wa nchini China ameiuza figo yake ili aweze kununua simu moja ya iPhone na iPad.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na magazeti ya China, kijana huyo anayeitwa Xiao Zheng alifanyiwa operesheni ya kuliondoa figo lake moja kwenye jimbo la Hunan mwezi aprili mwaka huu.

Pesa alizolipwa kwa kuuza figo lake kijana huyo alinunua simu ya iPhone na kompyuta ndogo ya iPad.

Xiao aliuza figo lake kwa yuan 20,000 ambazo ni sawa na Tsh. milioni 4.5.

"Wakati mtoto wangu aliporudi nyumbani akiwa na kompyuta ya iPad na simu ya iPhone, nilimuuliza amepata wapi pesa za kununulia vitu hivyo, haukupita muda mrefu alitoboa siri kuwa ameliuza figo lake moja, nilihisi kama dunia inatuangukia", alisema mama yake Xiao.

Mama yake Xiao aliripoti polisi lakini hadi sasa hawajafanikiwa kumkamata mfanyabiashara aliyenunua figo yake.

Angalia VIDEO ya kijana huyo baada ya kuuza figo lake.
 
Last edited by a moderator:
huyu mchina bila shaka hata tigo yake imechakachuliwa sana, pia ubongo wake ni kikaragosi.
Yaani figo kwa milion nne tu, kweli akili za kichina ni FEKI
 
pengine ni utoto ila alitumia alichonacho kupata anachotaka.
 
Nafikiri tatizo ni kwamba ameuza figo hiyo kwa bei ndogo na matumizi ya pesa alizopata hayakuwa sahihi.

Hakuna sababu ya kukaa na mafigo mawili ambayo yanachuja chai ya rangi wakati unadaiwa ada ya chuo au kuna viwanja vya low density vinauzwa gezaulole.

Sisi huku tunaona kama ni biashara ambayo ni ya ajabu lkn wenzetu biashara hii ya uuzaji wa viungo ni ya kawaida kabisa.

Naunga mkono idea yake lkn napinga matumizi ya pesa alizopata.
 
Natafuta mteja wa Figo mwenye anataka ananipigie 0765129582
 
Figo zinauzwa bei rahisi tu, ukitangaza unamata hata kwa bei ndogo zaidi ya hapo. Mfano Kigoma kwa waha hata kwa milioni moja unapata! Nasikitika yule mzee wa fursa (R.I.P) alipataje shida ya figo hadi akafariki. Labda kulikuwa na zaidi.
 
Wapi naweza uza figo hapa tz?
 
Back
Top Bottom