Aunt Ezekiel: Sitaki marafiki tena

Pistol

Senior Member
Oct 13, 2015
194
86
BAADA ya urafiki wa waigizaji mashuhuri na wanaozungumzwa sana nchini, Wema Sepetu na Aunty Ezekiel ‘Mama Cookie’ kuvunjika, waigizaji hao wameibuka na kudai kwamba hawahitaji marafiki.

Ilishangaza Aunty Ezekiel kutomualika Wema Sepetu katika sherehe ya mtoto wake na mnenguaji wa Diamond Platinum, Moses Iyobo iliyofanyika mwishoni mwa wiki ukumbi wa Serena Hotel.

Aunty Ezekiel alipoulizwa kuhusu urafiki wake na Wema, alisema hataki marafiki kwa kuwa hawamsaidii chochote hivyo kwa sasa rafiki yake mkubwa wa kufa na kuzikana ni mwanae tu.

“Rafiki yangu aliyebaki ni mtoto wangu ambaye atakuwa rafiki wa kufa na kuzikana, Aunty Ezekiel wa kipindi kile si wa sasa, kwa sasa nimeongezea jina naitwa ‘Mama Cookie’ naishi maisha mengine, nawaza kumlea mwanangu muda wote sina muda na marafiki wengine,” alisema Aunty Ezekiel.

Aunt Ezekiel aliongeza kwamba Iyobo na Cookie ndiyo wanaompa furaha na ndiyo wamebaki kama baba na mama yake.

Chanzo:Mtanzania
 
Pesa ipo kumbe, sherehe ya mwanae imefanyika Serena, sipati picha mjengo na ndinga anayovuta iyobo na aunt.
 
Sijui kwa nini wema hadumu na mashoga. Rafiki yake ambae yuko nae muda ni martin tu,maybe na petit, aunt walikuwa mashost nao umekufa. Au yeye anapenda awe juu ya wenzie, mwisho wanachoka, au tu inatokea Kila mtu ana move on
 
Anaogopa Iyobo asinyakuliwe na shoga zakke. Mana hiyo ndo tabia yao mastar wa kike kuchukuliana mabwana. Hongera sana Aunty.
 
Ulimwengu huu bila kuwa na shoga wala rafiki kwa mtoto wa kike tena mtanzania ni ngumu.

Ni mwendelezo wa kuropoka wanaofanya "mastaa" wa Bongo kila Mara wanapohojiwa na media. Hebu wajaribu kuwa makini.
 
Naona huyu naye kaanza kukua sasa.

Utoto unaisha taratiibu kichwani.

Ila siku akipigwa kibuti lazima usikie mengine
 
Hawa mademu wa bongo movie sijapata sababu kwanini watu hadi wanahonga... Ni sababu ya kuonekana kwenye media au nini?ukipata mda wa kukaa nao hata kwa dk 10 utawachoka

Story zao za kwenye magazeti wanalipia, hata uwaonavyo katika picha siyo wao kihalisia, ni filters
 
Sijui kwa nini wema hadumu na mashoga. Rafiki yake ambae yuko nae muda ni martin tu,maybe na petit, aunt walikuwa mashost nao umekufa. Au yeye anapenda awe juu ya wenzie, mwisho wanachoka, au tu inatokea Kila mtu ana move on
Petit washakorofishana,Martin wamepatana tena juzi juzi tu
 
Ulimwengu huu bila kuwa na shoga wala rafiki kwa mtoto wa kike tena mtanzania ni ngumu.

Ni mwendelezo wa kuropoka wanaofanya "mastaa" wa Bongo kila Mara wanapohojiwa na media. Hebu wajaribu kuwa makini.
Inawezekana sana ....rafiki umekutana nae ukubwani kudumu kwenye urafiki ni shida sana. Mie shost zangu nilikaa nae mtaa mmoja na tulisoma wote olevel na alevel.....chuo sikuwaga na shost na wala kazini ninaye mmoja ambae nae basi tupotupo tu.....ila wale wa utotoni mpaka leo tupo poa na ni kama ndugu.
 
Kama ameamua kubadilika ni vzuri mana hata kwenye magazeti siku hizi haonekani. Ni jambo zuri sana .
 
Sijui kwa nini wema hadumu na mashoga. Rafiki yake ambae yuko nae muda ni martin tu,maybe na petit, aunt walikuwa mashost nao umekufa. Au yeye anapenda awe juu ya wenzie, mwisho wanachoka, au tu inatokea Kila mtu ana move on
Huyu Dada atakuwa anawapanda wenzie kichwani kias kwamba wanashindwa kuvumilia yaani wema anapendaga MTU ambaye haelewani nae na rafiki yake iwe hivo hivo kitu ambacho kinaboa, haiwezekani wote , kina kajala,snura, Aunt wote wakawa wanamkosea yeye tu
 
Back
Top Bottom