Augustino Mrema ampongeza Rais Magufuli kwa kusamehe wafungwa

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
1,606
1,956
Mwenyekiti wa Bodi ya Parole nchini Augustino Mrema amempongeza Rais Magufuli kwa uamuzi wa kutoa msamaha kwa wafungwa mbalimbali.

Amesema ni wazi Mh JPM amesikia kilio cha wengi na kuamua kufanya ubinadamu kwa kuchukua maamuzi hayo ili, kupunguza msongamano wa wafungwa gerezani.

Ameongeza kuwa Mh.JPM ni Rais msikivu na mwenye upendo mkubwa na anaamini ndiye Rais ambaye wengi tulimtarajia.Ndg Mrema pia amedai kuwa upo uwezekano Rais Magufuli hakuwa akipewa taarifa sahihi kuhusu hali za wafungwa magerezani na hii ni kutokana na maslahi ya watu binafsi.

Amezungumzia pia juhudi alizowahi kuzifanya kupunguza msongamano magerezani kwa kuwalipia faini wafungwa walioshindwa kufanya hivyo lakini juhudi hizo zilikwamisha kwa maslahi ya watu binafsi.

========

Mwenyekiti wa Bodi ya Parole, Augustine Mrema amepongeza uamuzi wa Rais John Magufuli wa kutoa msamaha kwa wafungwa na kumuelezea kama Rais mwenye upendo wa aina yake.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumamosi, Mrema amesema ni wazi kuwa Rais amesikia kilio cha watu na kuamua kufanya ubinadamu ili kupunguza msongamano wa wafungwa magerezani.


“Namvulia kofia kabisa, huyu ni Rais msikivu, ana mapenzi ya kweli kwa Watanzania naweza kusema tumepata mtu ambaye tulikuwa tunamtaka,”


Mrema amesema upo uwezekano kuwa Rais alikuwa hapewi taarifa sahihi kuhusu hali ya magereza.


“Magerezani kuna uozo, wapo watu wengine wanajaa kule kwa makosa ambayo wanaweza kulipa faini tu wakatoka,”


“Nilianzisha kampeni ya kuwalipia faini wafungwa ambao walishindwa kujilipia lakini kutokana na maslahi ya baadhi ya watu nikaambiwa nisitishe kwa madai kuwa wafungwa hao hawajajutia makosa. Hii si sawa, naomba watu wa magereza wabadilike hakuna sababu ya kuwajaza wafungwa kule ambao wanatakiwa kutoka


Chanzo: Mwananchi
 
Mrema hiyo ya Babu Seya ilikuwa kiki yake tangia alipopewa hicho cheo,ila ikàbuma..!!
 
Mzee WA kiraracha kapata kiki Mpya ya mjini, tutamkoma aisee, yaani Dr. Shika ndo kaishapotezwa mjini.
 
Ktk Inji hii hakuna alieshika cheo cha naibu waziri mkuu zaidi ya Mzee wa Kiraracha pekee...Yesu na Maria..
 
Back
Top Bottom