Augustino Lyatonga MREMA, Namvulia Kofia

Augustino Lyatonga MREMA, Namvulia Kofia

Mkuu, ikitokea kwa bahati mbaya ukawa kwenye mazishi ya mrema halafu ukaambiwa useme machache, je ungeyasema hayo?

Hili ndilo tatizo letu kubwa, unafiki. Mtu yuko hai anafanya mambo makubwa kwa ajili yetu kisha hatumthamini. Akifa tunashindana kutoa heshima na sifa kemkem, tukishazika tumesahau
 
Sisi tuliokuwapo enzi zile, tulishuhudia uwezo wake mkubwa ktk kuongoza wizara mbalimbali..alikuwa mtu mbunifu mchapakazi anajua mbinu za kutatua matatizo, ayeaminika anachokitamka hakuwa mnafiki au mbabaishaji..majambazi kujitokeza na kusalimisha silaha halikuwa jambo rahisi.. lkn yeye aliweza..na tangu wakati huo sijasikia tena majambazi wanarudisha silaha..!!!
Kiutendaji huwa namfananisha na Mh. J.P.Maghufuli.
Hata mimi namvulia kofia.
 
Kuna thread zingine nasita hata kuchangia kwa sababu sijui na sielewi kabisa lengo la waanzisha hizo thread. Yawezekana wengi wanaoanzisha hizi thread kinachowasukuma kupindisha historia kunatokana na mambo mawili. Kwanza wanataka kuwaenzi wale wasiostahili ushujaa hata kama ni kweli na pili ni kuwanyima sifa wale wanaostahili hata kama ni kweli. Mfano mzuri ni Augustino Lyatonga Mrema.

Augustino Lyatonga Mrema aliteuliwa na Mwinyi kuwa Waziri wa Mambo ya ndani baada ya kushinda Ubunge kwenye uchaguzi wa mwaka 1990. Ni mwaka huo upepo wa mageuzi ulipoanza kuutikisa ulimwengu kama tunavyoshuhudia hii leo katika baadhi ya nchi kama Tunisia, Egypt, Libya na kwingineko. Kila nchi iliupokea upepo wa mageuzi kwa njia tofauti pamoja na Tanzania nchi ya amani na utulivu (sic)

Hapa Tanzania huu upepo huu wa mageuzi ulileta hofu kubwa kwa chama tawala CCM chini ya Raisi wake Al Haji Hassan Mwinyi. Kila mbinu ilifanyika kuuzima na dola kama ya Gaddafi wa Libya ilikuwa tayari kwa lolote ilimradi mageuzi hayafanikiwi. Kwa bahati nzuri Tanzania ilikuwa na mtu mmoja ambaye bila sauti yake mfumo wa vyama vingi ungebaki kuwa ndoto. Mtu huyo ni Hayati Mwalimu Nyerere.

Ni Mwalimu aliyepaaza sauti yake na kuikemea serikali ya CCM kuwa kuongelea vyama vingi si dhambi tena. CCM kwa shingo upande iliruhusu mjadala kwa mkono moja huku mkono wa pili ukiipa dola ruhusa kuendesha vita dhidi ya wanamageuzi. Hii vita iliyoendeshwa na jeshi la polisi (FFU) ikisimamiwa na Waziri wake ilihakikisha sauti za wanamageuzi haisikiki. Huyo Waziri alikuwa Augustino Lyatonga Mrema.

Uovu aliyoufanya Mrema kwa wanamageuzi mwaka 1991 hadi 1992 hakuna namna ya kuweza kuuelezea bila kutoa machozi. Hii ndiyo moja ya sababu za Raisi Al Haj Ali Hasan Mwinyi mwaka 1993 kuvunja katiba kwa kumzawadia Augustino Lyatonga Mrema cheo baada ya kuwaadhibu na kuwapa vilema vya maisha raia wema - kosa ? kudai haki ! Cheo hicho ambacho hakikuwa kwenye katiba ni Naibu Waziri Mkuu !

Baada ya kuutwaa Unaibu na kwa kulewa madaraka, ndipo ndoto ya Augustino Lyatonga Mrema ya kuukwaa Uraisi ilipozaliwa. Akizidi kuwaminya wanamageuzi na kuingilia kazi za wizara mbali mbali bila mpangilio, wajanja wenzake ndani ya CCM wakamstukia na mwaka 1994 wakaingiza kwenye katiba ya chama kipengele ambacho kingekuwa kikwazo kwa hizo ndoto zake. Kipengele hicho kilikuwa cha Shahada.

Lyatonga wa Kiraracha baada ya kukwama akadandia gari la mageuzi mwaka 1995, miaka mitano tangu upepo wa mageuzi uanze kuvuma ! Mwaka 2010 baada ya kuona mambo hayaendi, akabwanga manyanga kulilia Uraisi akaipigia magoti CCM na kumlamba miguu Raisi Jakaya Mrisho Kikwete na kwa huruma ya mafisadi kaweza kuambulia Ubunge na hivi sasa Uenyekiti wa kamati mojawapo za Bunge.

Huyo ndiye Augustino Lyatonga Mrema, Mbunge wa Vunjo na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa ambaye kuna watu wanamvulia kofia kwa kuongoza mageuzi ! Hiyo ndiyo Tanzania yetu, tumezoea kuwapa watu sifa hata wale ambao historia zao zinatia kichefuchefu na orodha ni ndefu kwa hiyo haishangazi hata kidogo. Itakuwaje umsifie Lyatonga wa Kiraracha usimsifie nyota wake Mkwere ?
 
Lyatonga hana kitu anapenda sana maslahi, amemsifu mkere mda woote hata katika hali ngumu ya kiuongozi kama sasa!!
 
Huyu Mrema anaweza kuwa na Umri gani?
Wakati akiwa Home Affairs alifanya kitu!You remember alichange magari ya Moshi /Dodoma/Mbeya/Mwanza kusafiri mchanatu!!!!Ajali zilipungua kidogo
 
Mrema ni mchapakazi na ni mtu wa vitendo sio porojo tukubali hilo wandugu. Anabadilisha maneno kuwa vitendo na akifanya kitu kinaonekana. Sio kama viongozi wa sasa maneno mengi yaliyopangika lakini matendo sifuri na hakuna kinachoeleweka. Mrema akiwa serikalini alifanya mambo watu wakapata tumaini jipya. Akiwa upinzani pia alifanya upinzani ukaonekana. Tatizo alizungukwa na maadui wengi kuliko marafiki hata kama una nguvu namna gani ukikosa support hutafika mbali. Wamemfrustrate mpaka kumletea magonjwa sugu lakini Mungu yuko pamoja nae. Kwa nafasi aliyoko tutegemee pia kuona mabadiliko. Tumpe moral support tutaona changes.

Well done Mrema. Chapa kazi tuko nyuma yako.
 
Mkuu Mag3, pole sana! Hata Nyerere kuna watu wachache wanamchukia sana. Na umeona watu wanamsifia Mtukila hapa kwa mambo aliyofanya awali siyo ya sasa hivi.

Wakati Mrema alipokuwa mambo ya ndani alifanya kazi kwa mujibu wa mamlaka iliyomweka madakani. Mara zote amekonga nyoyo za wananchi wengi katika utendaji wake na amekuwa mtetezi wa haki za wananchi bila upendeleo na bila kujihusisha na ufisadi.

Mara zote waliompinga ni mafisadi tu!

Sasa amekuwa mbunge wa Vunjo kwa miezi 4 tu lakini angalia angalia vile Vunjo inavong'ara. Usalama wa raia, miradi akina mama, akina baba hawashindi tena vilabuni, maji. Sijui mengine ila haya nimeyasikia kwenye vyombo vya habari.
 
Lyatonga si msafi ki hivyo bali ni mtu anaye pursue personal agenda sawa na madikteta wengine kama akina Hitler, Pinochet nk. Silaha wanayotumia ni nguvu ya ushawishi ili kupata sympath ya umma na kuwafumba umma wasione maovu yao. Tuliona jinsi Mrema alivyokuwa anawaita wakwepa kodi kule Kiraracha badala ya kwenye ofisi maalum.

Vilevile katika kipindi chake cha uwaziri wa mambo ya ndani aliwapendelea kwa kuwapandisha vyeo mapolisi wengi kutoka kabila lake
 
Mkuu, ikitokea kwa bahati mbaya ukawa kwenye mazishi ya mrema halafu ukaambiwa useme machache, je ungeyasema hayo?

mazishi? Hapa hapana mrema asiongelewe ivo ata kama unamtetea! Ujumla wa shushushu mrema ni wa ajabu! Ila kwa kuwa ni mpinzani ambaye hajawai kustaafu ushushu,siwezi kumpinga wala kumsifia. Kwa ufupi ni mtu aliyekuwa imara. Kundi lake naweza kuwaweka pia magufuli,mwandosya, dr.slaa,na mwakyusa. Ni watu walio na image ya Tanzania.
 
He's really controversial. Nilichanganyikiwa zaidi alipokua anampigia debe jk dodoma, aliporudi dar kamsimamisha Mutamwega kupeperusha bendera ya urais ya chama chake kuchuana na huyo huyo jk
 
Kuna thread zingine nasita hata kuchangia kwa sababu sijui na sielewi kabisa lengo la waanzisha hizo thread. Yawezekana wengi wanaoanzisha hizi thread kinachowasukuma kupindisha historia kunatokana na mambo mawili. Kwanza wanataka kuwaenzi wale wasiostahili ushujaa hata kama ni kweli na pili ni kuwanyima sifa wale wanaostahili hata kama ni kweli. Mfano mzuri ni Augustino Lyatonga Mrema.

Augustino Lyatonga Mrema aliteuliwa na Mwinyi kuwa Waziri wa Mambo ya ndani baada ya kushinda Ubunge kwenye uchaguzi wa mwaka 1990. Ni mwaka huo upepo wa mageuzi ulipoanza kuutikisa ulimwengu kama tunavyoshuhudia hii leo katika baadhi ya nchi kama Tunisia, Egypt, Libya na kwingineko. Kila nchi iliupokea upepo wa mageuzi kwa njia tofauti pamoja na Tanzania nchi ya amani na utulivu (sic)

Hapa Tanzania huu upepo huu wa mageuzi ulileta hofu kubwa kwa chama tawala CCM chini ya Raisi wake Al Haji Hassan Mwinyi. Kila mbinu ilifanyika kuuzima na dola kama ya Gaddafi wa Libya ilikuwa tayari kwa lolote ilimradi mageuzi hayafanikiwi. Kwa bahati nzuri Tanzania ilikuwa na mtu mmoja ambaye bila sauti yake mfumo wa vyama vingi ungebaki kuwa ndoto. Mtu huyo ni Hayati Mwalimu Nyerere.

Ni Mwalimu aliyepaaza sauti yake na kuikemea serikali ya CCM kuwa kuongelea vyama vingi si dhambi tena. CCM kwa shingo upande iliruhusu mjadala kwa mkono moja huku mkono wa pili ukiipa dola ruhusa kuendesha vita dhidi ya wanamageuzi. Hii vita iliyoendeshwa na jeshi la polisi (FFU) ikisimamiwa na Waziri wake ilihakikisha sauti za wanamageuzi haisikiki. Huyo Waziri alikuwa Augustino Lyatonga Mrema.

Uovu aliyoufanya Mrema kwa wanamageuzi mwaka 1991 hadi 1992 hakuna namna ya kuweza kuuelezea bila kutoa machozi. Hii ndiyo moja ya sababu za Raisi Al Haj Ali Hasan Mwinyi mwaka 1993 kuvunja katiba kwa kumzawadia Augustino Lyatonga Mrema cheo baada ya kuwaadhibu na kuwapa vilema vya maisha raia wema - kosa ? kudai haki ! Cheo hicho ambacho hakikuwa kwenye katiba ni Naibu Waziri Mkuu !

Baada ya kuutwaa Unaibu na kwa kulewa madaraka, ndipo ndoto ya Augustino Lyatonga Mrema ya kuukwaa Uraisi ilipozaliwa. Akizidi kuwaminya wanamageuzi na kuingilia kazi za wizara mbali mbali bila mpangilio, wajanja wenzake ndani ya CCM wakamstukia na mwaka 1994 wakaingiza kwenye katiba ya chama kipengele ambacho kingekuwa kikwazo kwa hizo ndoto zake. Kipengele hicho kilikuwa cha Shahada.

Lyatonga wa Kiraracha baada ya kukwama akadandia gari la mageuzi mwaka 1995, miaka mitano tangu upepo wa mageuzi uanze kuvuma ! Mwaka 2010 baada ya kuona mambo hayaendi, akabwanga manyanga kulilia Uraisi akaipigia magoti CCM na kumlamba miguu Raisi Jakaya Mrisho Kikwete na kwa huruma ya mafisadi kaweza kuambulia Ubunge na hivi sasa Uenyekiti wa kamati mojawapo za Bunge.

Huyo ndiye Augustino Lyatonga Mrema, Mbunge wa Vunjo na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa ambaye kuna watu wanamvulia kofia kwa kuongoza mageuzi ! Hiyo ndiyo Tanzania yetu, tumezoea kuwapa watu sifa hata wale ambao historia zao zinatia kichefuchefu na orodha ni ndefu kwa hiyo haishangazi hata kidogo. Itakuwaje umsifie Lyatonga wa Kiraracha usimsifie nyota wake Mkwere ?

Ndugu Mag3 nimesoma post yako na hama kwa hakika imejaa ukweli japo ina maswali mengi sana ambayo yanamsifia tena Mrema kwa mbali!!!!

1. Umeishasema baada ya Mrema kufanya aliyofanya alipandishwa cheo, hapo una-confirm kuwa alikuwa akifuata matakwa ya ccm! sio? je kwako wewe dhana ya kuwa ulifanya kosa na baadae ukabadilika haipo? kama Mrema alifuata itikadi za chama chake na baadae akabadilika na kuwa mwiba kwa CCM,hauoni kuwa huyu mtu alicheza muziki ule ule wa mabadiliko ambao aliupinga? kwa wana mapiunduzi na wapenda mabadiliko je huu si ni ushindi?? yaani inataka mtu abaki na itikadi zake zile zile na hawezi kubadilika? wangapi leo waliokuwa CCM na wako upinzani walivyokuwa CCM walikuwa wazuri tu au waliondoka bila mizengwe? nitajie mmoja aliyekuwa CCM ambaye sasa yuko upinzani na aliondoka CCM kwa sababu hakipendi CCM! mmoja tu! hata hao akina Sita na ,Mwakyembe ni ma-vuvuzela ambayo Mrema amewapita kwa mbali sana, Nilijua kitendo chake cha kuondoka CCM kwa position zile ILIKUWA CHACHU kwa mawaziri wengine WANAOIPINGA ccm ILI HALI WAMO HUMO HUMO... wangehamia UPINZANI but to date we have only Mrema in record!

2. Kwa dhana yako ya kuangalia upande mmoja then hakuna watu wanaostahili siga nchi hii! Mrema anasifiwa kuanzia alipokuwa waziri mpaka alipokuwa upinzani sifa hizi hata kamahauzitaki kazi yake imeonekana, imedumu na leo ipo! sidhani kama hili lina hitaji mjadala mrefu! akiwa CCM still alipigana na mafisadi enzi hizo watu hawajui rushwa kama hii leo!

3. Na kama unavyosema wenzake waliweka kipengele ku-mbana maana yake walimuogopa , HII SIO SIFA? waliogopa kitu gani mpaka wakabadili sifa za kugombea urais? go west go east Mrema type ndio wanaotakiwa Tanzania ! strong and moving! hapa naona umemsifia bila kujua

4. Tukishindwa ku-waenzi viongozi waliojituma kulitumikia taifa kwa namna yeyote ile then hatujatapata bado viongozi wa kuwasifia , Nyerere unasema aliwaambia CCM walete mabadiliko! mabadiliko hewa kama vile tulivyo uhuru hewa! Nyerere leo hii analaumiwa seriously kuwa mabadiliko ya katiba na kuweka nguvu kubwa kwa rais yeye ndiye alianzisha-KUSEMA RUHUSU VYAMA VINGI HAIKUTOSHA MAG3 please note this down...ILIKUWA DANGANYA TOTO ILIKUWA GERESHA NASHANGAA UNAMSIFIA NYERERE KWA HILI..KATIBA ILITAKIWA IBADILIKE, TUME YA UCHAGUZI ILITEULIWA NA CCM HUKU NYERERE AKIONA, ACHILIA MBALI CHAGUZI ZILE ZA KIVULI NA MTU -which is rated to be serious crime of century!.., in short, uozo mwingi wa CCM leo umeanzia kwa Nyerere, je Nyerere hapaswi kusifiwa kwa mema mengine??

5. Mwisho nimesema kwa lolote lile alilofanya Mrema then aliimarisha upinzani in his generation and today we have at least strong upinzani kwa sababu ya misingi ya akina Mrema...... note that Saul turned out to be PAUL in bible....people change whether they pretend or not walio-upande wetu si adui zetu
 
...tatizo langu kwa Mrema na Mtikila, they are jack of all trades... and they end up with no tangible results... Hawamalizi wanachokianzisha. Wakishabikiwa kidogo, thats it. That becomes the end in itself! They need a fully flegded, round of completed strategy!
 
Waberoya, sina maneno ya kuongeza kwenye majibu yako kwa Mag3. I salute you
 
Bila kumsahau Rev. Mtikila ni moja ya wapambanaji wa kweli

Nikikumbuka vituko vya Mtikila kwenye uchaguzi mdogo jimbo la Tarime mpaka akapigwa mawe na kukiri kuwa alikuwa anafanya kazi ya kuwavuruga wapinzani kwa sababu alihongwa na CCM, huwa sina imani naye tena. Yeye akomae na kufungua kesi mahakamani tu kwani anaweza na anapenda.

Mtikila wa enzi zile siyo huyu CCM wamekwisha mchakachua akili.
 
Mkuu Mag3, pole sana! Hata Nyerere kuna watu wachache wanamchukia sana. Na umeona watu wanamsifia Mtukila hapa kwa mambo aliyofanya awali siyo ya sasa hivi.

Sijasema namchukia Mrema ila naamini niliyoyasema ni ya ukweli na ndiyo maana huyapingi. Mtikila usimweke kwenye kundi moja na Mrema kwa sababu Mtikila ni moja kati ya watu walioonja machungu mikononi mwa Mrema wakidai mageuzi.

Wakati Mrema alipokuwa mambo ya ndani alifanya kazi kwa mujibu wa mamlaka iliyomweka madakani.
Na katika kufanya kazi kwa mujibu wa mamlaka iliyomweka madarakani alihakikisha anapiga vita mageuzi hata ikibidi kuwashambulia na kuwaumiza wana mageuzi, nafikiri mpaka hapo bado tunakubaliana.

Mara zote amekonga nyoyo za wananchi wengi katika utendaji wake na amekuwa mtetezi wa haki za wananchi bila upendeleo na bila kujihusisha na ufisadi.
Mmm, ungejua hungetamka maneno hayo. Hata hivyo alioweza kukonga nyoyo zao ni kweli walimganda kama shati lililonyeshewa mvua na si ajabu alihama nao kutoka CCM, akahama nao kutoka NCCR mageuzi na hadi leo anao. Ukweli ni kuwa wote hao hawakushiriki kwenye mageuzi toka mwanzo na walikuwa wadandiaji tu (opportunists) kama yeye.

Mara zote waliompinga ni mafisadi tu!
Duh, kwa hiyo aliokuwa akiwatupia mabomu kwa miaka minne wakidai mabadiliko ndio walikuwa mafisadi na siyo CCM. Nakumbuka alipoapa kuwa hawezi kuhama CCM na kudai kuwa akifanya hivyo na yeye atakuwa mwehu !

Sasa amekuwa mbunge wa Vunjo kwa miezi 4 tu lakini angalia angalia vile Vunjo inavong'ara. Usalama wa raia, miradi akina mama, akina baba hawashindi tena vilabuni, maji. Sijui mengine ila haya nimeyasikia kwenye vyombo vya habari.

Kweli ukistaajabu ya Musa subiri ya Farao, yaani Augustino Lyatonga Mrema kwa hii miezi minne ameweza kufanikisha hayo yote ! Halafu bila aibu unasema hayo unayasikia tu kwenye vyombo vya habari - vya Vunjo ? Kweli ukipenda chongo utaita kengeza, anyway nakupa benefit of doubt kwani mashabiki wa Mrema mko wengi ila tatizo moja tu, tuliopigwa virungu 1991, 1992, 1993, 1994 hadi 1995 hatuwezi kumsahau kirahisi, tutamkubuka sana Augustino Lyatonga Mrema.

Muhosni, kuna mdahalo uliofanyika ukumbi wa Kilimanjaro Hotel kwa wagombea Urais mwaka 1995, uutafute umsikilize shujaa wako alivyokuwa akijibu hoja. Wagombea walikuwa Mkapa, Cheyo, Lipumba na Mrema mwenyewe ! Nakutakia siku njema.
 
...tatizo langu kwa Mrema na Mtikila, they are jack of all trades... and they end up with no tangible results... Hawamalizi wanachokianzisha. Wakishabikiwa kidogo, thats it. That becomes the end in itself! They need a fully flegded, round of completed strategy!

Mkuu hebu tulia kwanza kidogo.

Mtikila alianzisha sera ya makabachori na walalahoi. Pamoja na kulaumiwa kuwa ya kibaguzi, ndiyo iliyochangia kutufumbua macho kwamba hawa wahindi wanashirikiana na serikali yetu kutuibia. Hakuwahi kuiacha pamoja na kuwekwa ndani mara kadhaa.

Mtikila amesimamia hoja ya mgombea binafsi katika kipindi cha miaka takriban 15. Hakutetereka pamoja na kudhihakiwa, kufungwa jela, na kuandamwa kisiasa.

Mtikila hajaacha hoja yake ya Utanganyika hadi leo.

Point yangu kuu ni kwamba, kushindwa kwetu kuwathamini na kuwasapoti wapiganaji wa ukweli ndo kinawafanya wabadilike. Angalia pamoja na mtikila kufadhiliwa na RA alijisahau akamlipua.

Mikakati ya Mrema unaweza kuiorodhesha mwenyewe
 
Nikikumbuka vituko vya Mtikila kwenye uchaguzi mdogo jimbo la Tarime mpaka akapigwa mawe na kukiri kuwa alikuwa anafanya kazi ya kuwavuruga wapinzani kwa sababu alihongwa na CCM, huwa sina imani naye tena. Yeye akomae na kufungua kesi mahakamani tu kwani anaweza na anapenda.

Mtikila wa enzi zile siyo huyu CCM wamekwisha mchakachua akili.

Ilikuwaje hadi ccm wakamchakacha Mtikila akili. Ni kiasi gani ni kosa la mtikila nini mchango wetu kama watu ambao alikuwa anapigania haki zetu?
 
Kwa kweli inatakiwa kuwalinda hawa viongozi wenye kuonyesha misimamo ya kweli na wenye uwezo mkubwa wa kupambanua mambo na wenye ujasiri mkubwa,
Kama hawakutunzwa basi ni raisi mno kwa mafisadi kuwanunua
Mtikila na ujasiri wake wote alinunuliwa na Rostam kwa kiwango cha chini ya milioni tano, na akawa kimya kabisa japo bado anajaribu kufurukuta lakini sio kwa ile nguvu
Mrema, baada ya kupoteza na hakukuwa na uwezo wa kumsaidia nadhani alirejea CCM na kumpigia magoti JK, na kweli akapewa safari ya In dia kutibia na kutoka hapo akawa CCM kwenye Upinzani
Tujaribu kuwatunza wakina Zitto, Kafulila na wengineo kama kmweli bado hawajaingia kwenye ile mikono
 
meg3 Mrema kupiga wanamageuzi mabomu enzi zile ndiko kunakomfutia ujasiri wake? jaribu kuanalaizi ishu kwa wakati husika, kumuhukumu mrema wa wakati ule kwa mazingira ya sasa sidhani kama ni sahihi.
Soma vizuri pandiko alilokujibu waberonya amekupa hadi mfano wa mt paulo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom