Mwenyekiti wa chama cha TLP bwana Augustine Lyatonga Mrema ametangaza kuendelea kukitetea kiti chake cha ubunge katika jimbo lake la Vunjo kwa tiketi ya chama chake.
Hakuna wa kumng'oa Mrema pale Vunjo!
Kwa hiyo hats CCM hamtasimamisha MTU?
Kwani mwaka 2010 hakusimamishwa mtu?
Kuongea ni jambo lingine na kumaanisha ni kitu kingine! Mrema kuna wakati hamaanishi anachoongea na haongei anachomaanisha
Amepitishwa ama amejipitisha kuweka jina na picha kwenye orodha ya wagombea?Sidhani kama wanavunjo wanautayari wakurudia makosa.
Mrema atakuwa mbunge Vunjo mpaka atakapoamua mwenyewe. Sisi wenyeji wa jimbo hili tulimpigia kura mwaka 2010.Mpinzani wake ni CCM. Anayebisha aweke kura za pamoja za Chadema, NCCR na CUF uchaguzi uliopita jimboni hapa. Kumshinda Mrema Vunjo mpaka UKAWA wachanganye na CCM which is impossible. Hakuna kilichobadilika.Mrema ni mbunge anayengoja kuapishwa.Tutampigia kura tena Oktoba. Tembeleeni Vunjo huwezi ku describe alivyo na support kubwa.