Pia kama tungekuwa na Mrema madarakani, ujambazi ungepungua sana Tanzania. Jamaa alijua kuzitumia "siku saba"
Hatutaweza kupata maendeleo mpaka pale viongozi wetu watakapoweza ku level na wananchi. Kwa maana kwamba watambue hali halisi na ku act accordingly badala ya kujigeuza na kujifanya tofauti kabisa na wananchi....Kwamba wawe in touch instead of out of touch. Mambo aliyokuwa akiyafanya Mrema yalipekea kuambiwa kuwa ni kwasababu ya kutokusoma nk,na kwasababu yalikuwa ni nje ya utashi wa kisomi na siasa uchwara za kikabila,ikawa rahisi kwake kuwa branded "kichaa" na huku ukiangalia kiundani,uelewa mdogo wa wananchi uliosababishwa na ufinyu wa elimu ndo silaha kubwa ya ccm na mafisadi wake. Mrema clearly leveled with THE PEOPLE na he was amongst them.....In reality,he was the right one for our generation.Siasa zetu zilitufanya tuwaone viongozi wetu kama ndugu zetu,hata mwalimu alisema waitwe ndugu..Na kwa ufahamu wetu,tukasema ni ndugu hawa na usomi wao walioupata kwa jasho letu watatusaidia.
Waliosoma ubepari tafsiri yake ikawa ni ubinafsi,hakuna undugu,undugu ni kwenye maandishi tu lakini utendaji ni ubinafsi,hawaku level na wananchi na taizo hilo bado lipo....Hapo classes za walio wasomi na wasio wasomi ambao ni watawaliwa na watu wa kudanganywa zikawa created. Wananchi bado hawaelewi kuwa inawezekana kuwa hold accountable hao ndugu..Ni mentality mbaya sana inayotu cost hadi sasa kwasababu mwalimu alikuwa akiwaamisha tu hata kama wakifanya kosa gani,mradi tu waliitikia kauli mbiu za zidumu fikra sahihi na kwamba hawa ni ndugu...Tuko karibu na viongozi kuliko wao walivyo karibu na sisi,at least kifikra na kimatarajio kwasababu kila mwananchi akienda kupiga kura pale penye kuidondosha kwenye sanduku yuko peke yake,ni kama ahadi anajiwekea na ndugu huyo anayemchagua,lakini wakati wa vote tallying, ajenda yao hiyo haina nguvu na wakati wa kuuliza huwezi kuuliza mwenyewe kama ilivyo wakati wa kudondosha kura yako peke yako kwenye sanduku, na mabadiliko ni lazima mobilization...ani sasa hata yule aliyeko nyuma yako amabye hujui alimpigia nani kura awe consulted.
Ni mkorogo lakini kwa kifupi Lyatonga was a honest and a decent man who leveld with his people. Aliyashughulikia matatizo jinsi yalivyo na si kufanya usanii kwa kutumia usomi na mambo ya protokali.
This man is a honorable man beyond all the dirty politics.....Alikuwa na nia ya ukweli na halisi ya kumsaidia mtanzania....Tanzania kama familia,tulifanya makosa kumpuuzia ndugu yetu Mrema,mwalimu na yeye kama baba,alifanya makosa yaliyo icost familiy yetu na ambayo bado yanaendelea kui cost,kama kweli mwalimu aliamua kuwa siasa za vyama hazina nguvu zaidi ya siasa za maslahi ya Taifa kwasababu ukoloni ulishaondoka,basi angeondoa ubinafsi na kuhakikisha kuwa Taifa linaongozwa kwa misingi ya uzalendo wa kweli....Mwalimu kama binadamu alifanya kosa.
Hivyo basi ujambazi na matatizo ya kijinsia kama alivyosema Kwame very minor kwa watu wasomi,ila ukweli ndio matatizo tuliyonao ambayo wao kama wasomi hawaoni kama yana exist...Ni kama mwalimu tu na hotuba za nguvu ambazo kinadharia zinakubalika lakini kivitendo hazi level na hali halisi...Hadi tutakapowachagua viongozi wenye kuwa in touch na wananchi halisi,bado hata tatizo la ufisadi litaonekana kama chuki binafsi tu kama anavyo ainisha mkuu wetu wa nchi.