Audio: Alichosema Askofu Dkt. Josephat Gwajima kwa Kardinali Pengo

Inside10

JF-Expert Member
May 20, 2011
26,060
23,941
This is too much..



SIKU chache baada ya Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Uzima na Ufufuo la jijini Dar, Josephat Gwajima kumtusi Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki nchini, Polycarp Kardinali Pengo, taarifa nyuma ya pazia zimeeleza kuwa mchungaji huyo ametumwa na kikundi cha watu fulani, Uwazi Mizengwe linakupa mchapo kamili.

Gwajima alirekodiwa kwenye ibada ya kanisa lake Jumapili iliyopita ambapo ‘alimtusi’ Pengo akituhumu kuwa ni msaliti kwani amekwenda kinyume na Taasisi ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Baraza la Makanisa ya Kipentekoste (CPCT) na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) kwa kuwataka waumini waisome Katiba Inayopendekezwa kisha wapewe uhuru wa kupiga kura ya “ndiyo” au “hapana” tofauti na vyombo hivyo vyenye dhamana ya kuongoza dini ya Kikristo vilivyotaka waumini waipigie kura ya “hapana” Katiba Inayopendekezwa.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, Gwajima ametumwa na kikundi cha watu ambacho kinaunga mkono hoja ya kukataa Mahakama ya Kadhi kama ilivyokataliwa na vyombo hivyo vyenye dhamana ya kuongoza dini ya Kikristo hivyo kumpinga Pengo ambaye wanaamini anatetea suala la Mahakama ya Kadhi liruhusiwe.

“Gwajima anatumika tu anamkashifu Pengo ili kumchafua na asiweze kusimamia hoja yake ya kuwaacha wapigakura waamue wenyewe kuikubali au kuikataa Katiba Inayopendekezwa wakiamini watu wanaweza kuipigia kura ya “ndiyo” na suala hilo likajadiliwa wakati wenzake wamelipinga,” kilisema chanzo hicho.

Kama hiyo haitoshi, chanzo hicho kilizidi kudai kuwa, Gwajima ametumika kumchafua Pengo kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kuhofia huenda akawa na upande wa mgombea ambaye anampigia chapuo ili apitishwe.

“Siyo tu kuhofia Mahakama ya Kadhi, Gwajima ametumika kumchafua Pengo kwa hofu kuwa huwenda akawa ana mgombea wake anayemtaka awe rais,” kilisema chanzo hicho.

 

Attachments

  • AUD-20150322-WA0004.mp3
    1.2 MB · Views: 37,947
Tatizo watu wametekwa na siasa, hawataki kuambiwa ukweli hata kidogo. Mahaba ya siasa ndio yanayowafanya wamtukane Pengo na kuona kakosea alichokisema. Pengo kama Kardinali wa kanisa Katoliki Tanzania, hawezi kuona mambo yanaenda kinyume halafu akakaa kimya, haiwezekani.

Kanisa halijafikia hatua ya kufanya maamuzi kwa niaba ya waumini wake, kanisa halijafikia hatua ya kulamisha watu katika suala linalohitaji haki na uhuru wa mtu. Kumwambia mtu lazima akapige kura ya hapana hiyo si sawa hata kidogo, na hata kumwambia mtu lazima akapige kura ya ndiyo nayo si sawa hata kidogo.

Mtu anapaswa kupiga kura kwa mujibu wa maamuzi na matakwa yake binafsi na si kulazimishwa. Ni sahaihi kuwaelimisha watu manzuri na mabaya ya katiba pendekezwa lakini si sahihi kuwapangia watu kura ya kupiga.

NB: - Attachment ya audio ni mahubiri ya Mwadhama Kardinali Pengo ambayo ndiyo yamemfanya Gwajima aongee hayo

- Attachment ya video ni mahubiri ya Mchungaji Gwajima

View attachment Kardinali Pengo akiongelea tamko la Maaskofu kuhusu katiba.mp3

View attachment Video ya mahubiri ya Mchungaji Gwajima.avi
 
Maboso,

Maneno yenye busara toka kwako. Sijajua Pengo aliongea nini mpaka kufikia hatua ya kutukanwa hivi!!! Hebu nidokeze kidogo mkuu
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom