Audhiwa kilabu cha pombe na kujitoa uhai | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Audhiwa kilabu cha pombe na kujitoa uhai

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jan 12, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 12, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  MKAZI wa Tambani Kitonga wilayani Ilala mkoani Dar es Salaam Kiraryo Chacha (39), amejinyonga baada ya kuudhiwa na wenzake katika kilabu cha pombe.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile alisema Chacha alikutwa amejinyonga kwa kutumia khanga ya mke wake aliyokuwa ameitundika katika mkorosho uliopo jirani na banda la kuku juzi saa 3 usiku nyumbani kwake Msongola.

  Kwa mujibu wa mtoto wa marehemu (jina limehifadhiwa) muda mfupi kabla ya Chacha
  kuchukua uamuzi huo, alirudi nyumbani akiwa amelewa na kusema atajinyonga kwa sababu kilabuni wamemuudhi.

  Kijana huyo alisema baba yake alilalamika kuudhiwa na watu waliokuwamo kilabuni ingawa hakuwataja majina na baadaye aliingia chumbani kwake na hakumuona mpaka alipomkuta amejinyonga.

  Maiti yake imehifadhiwa katika Hospitali ya Amana huku polisi wakiendelea na upelelezi.
  Katika tukio jingine, mkazi wa Tabata Kisiwani aliyetambuliwa kwa jina moja la Lasta (30), amekutwa amekufa katika machinjio ya nguruwe ya Tabata wilayani Ilala huku akitokwa na povu mdomoni na mwili wake ukiwa hauna jeraha lolote.

  Maiti hiyo iliokotwa juzi saa 12.30 asubuhi na chanzo cha kifo hicho hakijafahamika na maiti amehifadhiwa katika Hospitali ya Amana kwa uchunguzi zaidi.

  Aidha mvuvi Ibrahimu Ally (30), mkazi wa Mtoni Sabasaba amekutwa akiwa amekufa huku maiti yake ikielea ufukweni mwa bahari ya Hindi eneo la Kurasini katika Kijiji cha Wavuvi.

  Maiti hiyo ambayo iliopolewa na wananchi wa eneo hilo, iliokotwa ikiwa haina jeraha lolote na inasemekana marehemu alikuwa akivua samaki peke yake na mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Temeke.
   
 2. khayanda

  khayanda JF-Expert Member

  #2
  Jan 13, 2011
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 248
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wamemgusa panako siri kubwa yake ambayo hakuwa tayari kusubiri kuona wengine wakifahamishwa. Jamaa wamemtisha san hadi aemkabili Mungu huku amelewa, Pole zake
   
 3. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #3
  Jan 13, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Duh...nini hicho walimboa nacho huko kilabuni jamani?Unaweza kukuta hata haikua kitu kikubwa au cha maana..pombe tu ndo imekuza mambo!Nwyz apumzike salama!
   
 4. Shomari

  Shomari JF-Expert Member

  #4
  Jan 13, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,107
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  yote haya ni ugumu wa maisha
   
Loading...