Auawa na majambazi akiwa nyumbani kwake

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
MFANYABIASHARA Edmund Liwa anayefanya shughuli zake maeneo ya Kariakoo, ameuawa na majambazi baada ya kupigwa risasi wakati akiwa na wenzake nyumbani kwake Kimara Temboni jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Mark Kalunguyeye amesema kuwa, tukio hilo limetokea jana, majira ya saa 3 usiku, huko Kimara Temboni.

Amesema kuwa mfanyabiashara huyo akiwa na wenzake nyumbani kwake wakiwa katika mazungumzo ya hapa na pale, ghafla walivamiwa na majambazi ambao walimpiga risasi na kufa papo hapo.


Baada ya kumuua majambazi hao walipora shilingi. 780,000 alizokuwa nazo pamoja na simu zake tatu za mkononi kisha kutokomea kusikojulikana.


Maiti imehifadhiwa chumba cha maiti Hospitali ya Mwananyamala na Polisi wanaendelea na uchunguzi zaidi juu ya kifo hicho.

http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=3512818&&Cat=1
 
Back
Top Bottom