Lukolo
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 5,143
- 3,212
Mzozo wa wapenzi wawili usiku, umesababisha mmoja wa kike kupiga mayowe ya kumuita mwenzake mwizi, akavamiwa na watu waliompiga na kumchoma moto hadi kufa.
Kisa hicho kimetokea mkazi wa Magazini mjini Mpanda mkoani Katavi, Florence Mabuga (29), ambaye baada ya kuvamiwa na watu akidhaniwa mwizi, alipigwa na kuuawa na mwili wake kuchomwa moto mbele ya nyumba yake.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari, amethibitisha kuuawa kwa mkazi huyo katika
kisa hicho kilichotokea katika mtaa wa Nsemulwa-Magazini hivi karibini, usiku wakati Mabuga akimsindikiza mpenzi wake wa kike akitokea nyumbani kwake.
Akisimulia mkasa huo wa kusikitisha, Kamanda Kidavashari alisema Mabuga ambaye alikuwa msimamizi wa vibarua wa kujenga nyumba mjini humo, siku hiyo baada ya kurejea nyumbani, alitembelewa na mpenzi huyo ambaye jina lake halijafahamika.
Inadaiwa wakati Mabuga akimsindikiza rafiki huyo, ulizuka mzozo baina yao ambapo Mabuga alitishia kuwa usiku huo angechoma nyumba ya rafiki huyo, ndipo kwa hasira na hofu ya kuchomewa nyumba, alipiga yowe akiashiria kuwa Mabuga ni mwizi.
Kwa mujibu wa Kidavashari, Mabuga alianza kutimua mbio mara alipoona kundi la wananachi wenye hasira wakiwa na silaha mbalimbali za jadi wakikimbilia alipokuwa amesimama na rafiki yake huyo.
Inadaiwa kuwa wananchi hao walifanikiwa kumkamata Mabuga aliyekuwa akijaribu kuingia ndani ya nyumba yake, na kuanza kumpiga na kumsababishia mauti.
Uchunguzi wa awali wa kipolisi umebaini kuwa Mabuga alisingiziwa tu na mpenzi wake huyo, kwani hakuiba kitu chochote, ila mpenzi wake huyo alimpigia mayowe ya mwizi baada ya kuzuka mzozo baina yao, alidai.
Kwa mujibu wa Kidavashari mtuhumiwa huyo anaendelea kusakwa ili sheria ichukua mkondo wake, pia hakuna mtu yeyote aliyekamatwa hadi sasa kwani wananchi hao walikimbia eneo la tukio mara baada ya kufanya unyama huo
Source: Haya!
My Take!
Hivi utajisikiaje kama wewe ulikuwa ni mmoja wa hawa watu walioshiriki kumua huyu ndugu halafu unakuja kujua kwamba hakuwa mwizi? Lakin haya yote yametokana na kukosekana kwa kuaminiana kati ya raia na vyombo vyetu vya usalama. Kama hawa wezi wangekuwa wakikamatwa wanashughulikiwa ipasavyo baada ya kukamatwa naamini wananchi wangepunguza hizi tabia za kuwaua.
Mimi siku zote huwa najiuliza ni kwanini wananchi huwa wanapenda kumuua mtu ambaye tayari wameshamkamata, yupo mikononi mwao? Kwanini wasimpe tu adhabu kiasi na kumpeleka polisi? Nilishuhudia tukio moja Makambako Njombe ambalo sitakaa nilisahau, ambapo mwizi mmoja aliyekuwa anafukuzwa alipoona hana uwezo wa kukimbia zaidi, alivua shati na kulitupa halafu akaanza kumwita mtu mwingine aliyekuwa karibu mwisho. Wakimbizaji kwa vile hawajui walifika wakamvamia dogo wa watu na kuanza kumpiga, halafu yule mwizi halisi akakimbia. Wala sijui yule dogo alifanywaje, inawezekana aliuawa kwa sababu wapigaji walikuwa wanatumia silaha yoyote. Na yule dogo alikuwa analia na kuomboleza kwamba yeye siyo mwizi, lakini wapigaji hawakuwa wakisikia chochote.
Sasa nasema, hivi huu ndiyo ustaarabu watanzania? Kwanini likitokea tukio tunakimbilia kuua? Mimi ningeweza kusema ni halali kuua mtu mwenye silaha ambaye anapambana na raia kwa bunduki, huyo akikamatwa afanywe lolote, lakini huyo mwizi wa simu ambaye yupo mikono mitupu tu hana hata kisu, unamuua wanini? Watanzania tubadilike jamani, hii hali inahuzunisha sana. Kuna mmoja aliwahi pia kuuawa pale Mabibo hosteli kwa style hii hii.