Auanza Mwaka Mpya Vibaya Kwa Operesheni ya Kuongeza Makalio | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Auanza Mwaka Mpya Vibaya Kwa Operesheni ya Kuongeza Makalio

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jan 9, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 9, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mwanamke mmoja wa nchini Marekani ambaye alitaka kuingia mwaka 2011 akiwa mrembo zaidi na mwenye makalio makubwa amefariki dunia masaa matatu baada ya kufanyiwa operesheni ya kuongeza makalio.
  Mwaka 2011 umeanza vibaya kwa bwana Osvaldo Vargas mkazi wa Florida, Marekani, Amempoteza mke wake ambaye operesheni ya kuongeza urembo na makalio ili aonekane mrembo zaidi mwaka 2011 ilimalizika vibaya na kupelekea kifo chake.

  Lidvian Zelaya mwenye umri wa miaka 35 alitaka kuingia mwaka 2011 akiwa mrembo zaidi kwa kuamua kufanya operesheni ya kutoa nyama nyama na mafuta toka kwenye tumbo lake na kuzihamishia kwenye makalio yake ili kuyafanya yawe makubwa zaidi.

  Masaa matatu baada ya operesheni hiyo, Lidvian aliwahishwa hospitali akiwa amezidiwa sana na wakati mume wake anawasili hospitali Lidvian alikuwa ameishafariki dunia.

  "Amefariki akitafuta urembo, kwangu mimi alikuwa tayari ni mrembo", alisema mume wa Lidvian kwa huzuni.

  "Alikuwa ni mrembo, mwenye furaha na aliyependa kudansi, nataka kujua nini kimetokea", alisema bwana Oswaldo wakati akiongea na waandishi wa habari.

  "Hatumlaumu yeyote lakini tunataka kujua nini kimesababisha kifo chake", alisema Oswaldo akiwa pamoja na mwanasheria wake.

  Lidvian alifanyiwa operesheni kwenye kliniki ya Strax Rejuvenation, ya Florida, hata hivyo kliniki hiyo imesema kuwa sheria zinawabana kusema chochote kuhusiana na kifo cha Lidvian.
   
 2. m

  mzambia JF-Expert Member

  #2
  Jan 9, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Wabongo mpo?
   
 3. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #3
  Jan 9, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Eti kutafuta urembo!
   
 4. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #4
  Jan 9, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  masikini, kumbe mumwewe alikuwa akimpenda akiwa hivyohivyo, ila arogance ilimsukuma kumkosoa Mwenyezi Mungu kwa maumbile aliyompa! hiyo ni zawadi maalum kwa mwaka huu 2011 kutoka kwa Mungu mwenyewe kwenda kwa wote wanaomkosoa Mungu . happy new year, but pole baba kwa kumpoteza mwenzio mwamzoni kabisa mwa mwaka huu. Mungu akufariji
   
 5. L

  Leornado JF-Expert Member

  #5
  Jan 9, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Dah watu hawakomi? mke wa Obasanjo nae alifariki Spain kwenye beauty OP. I t is too risky na mwishoni unakuwa kituko ukianza kuzeeka.
   
 6. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #6
  Jan 9, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  mbongo atajitetea kuwa yeye anatumia dawa za kichina hivo kufa si rahisi bila kukua athari za baadae
   
Loading...