Aua mke na kumtupa katika shamba la kahawa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aua mke na kumtupa katika shamba la kahawa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Dec 28, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Dec 28, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  MKAZI wa Kijiji cha Iyula wilayani Mbozi mkoani Mbeya, Padri Msyalika (50), anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kumuua mkewe kwa kumpiga na kitu butu kichwani
  kisha kuutupa mwili wake kwenye shamba la kahawa la ndugu yake.

  Mwili wa mwanamke huyo, Magreth Mwakalambo (48), ulikutwa Desemba 26, mwaka huu katika shamba la kahawa la ndugu wa mumewe, Loid Msyalika (56) katika kitongoji cha Chawama kijijini hapo.

  Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Advocate Nyombi alisema baada ya kugundulika kwa mwili huo, Polisi walianza kufanya uchunguzi na ndipo uchunguzi wa awali ukaonesha kuwa aliuawa na mumewe wakiwa chumbani na ndipo mume huyo alipoubeba mwili wa mkewe hadi shambani alikoutelekeza.

  “Uchunguzi wa awali unaonesha marehemu aliuawa na mumewe aitwaye Padri Syalika mwenye umri wa miaka 50, mkulima na mkazi wa Iyula wakiwa chumbani nyumbani kwao kisha kuubeba mwili wa marehemu na kwenda kuutelekeza shambani hapo umbali wa meta 30 kutoka nyumbani kwao,” alisema RPC.

  Kamanda Nyombi alisema walibaini hayo baada ya kufika ndani ya chumba na kukuta na matone ya damu iliyoonekana kuchuruzika kutoka nje ya nyumba.

  Kwa mujibu wa kamanda huyo, chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa kimapenzi ambapo marehemu alikuwa akituhumiwa kuwa na uhusiano ya kimapenzi na watu wengine.

  Wakati huo huo, Kamanda Nyombi alisema Desemba 26, mwaka huu saa saba mchana katika Kijiji cha Ifumbo wilayani Chunya, mwanamume asiyefahamika jina wala makazi yake, alikutwa akiwa ameuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali kisogoni na wasiofahamika.

  Alisema chanzo cha mauaji hayo hakijafahamika, lakini uchunguzi zaidi juu ya matukio yote mawili unaendelea.
   
Loading...