kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 18,263
- 17,561
Umoja wa Afrika na SADC ni vema sasa kuanza kushughulikia viashiria vya kuvunjika kwa amani miongoni mwa nchi wanachama badala ya kusubiri hadi yatokee kama haya yanayotokea Zimbabwe. Viashiria vya uvunjivu wa amani kama vile udikteta, wizi wa kura, kung'ang'ania madaraka, na wizi wa mali za wananchi vinafahamika vema ndani na nje ya nchi wanachama. Kwanini tusiingilie kati kuzima viashiria vya uvunjifu amani badala ya kusubiri jeshi kupindua au vurugu za aina nyingine zitokee kisha ndio mtoe matamko?