Attention to John Mnyika na Halima Mdee

Attention to John Mnyika na Halima Mdee

Hao wajitafutie shughuli nyingine mapema maana ubunge 2015 kushnei, tena huyo Mnyika anavyojua mipasho inabidi hawe MC.
 
Hao wajitafutie shughuli nyingine mapema maana ubunge 2015 kushnei, tena huyo Mnyika anavyojua mipasho inabidi hawe MC.
haaa, mkuu nadhani inabidi waungane na kina mwigulu, sugu na hata yule wa songea mjini!
 
Ni mambo mazuri mmeyapanga kwa maendeleo ya watu wote, nadhani mbunge wa ubungo na mwenzake wa kawe watashirikiana katika hilo, maana wana mfuko wa maendeleo ya jimbo! Hivo watachota huko!
Kamilisheni haraka mmuite VP aje kufungua
 
Hao wajitafutie shughuli nyingine mapema maana ubunge 2015 kushnei, tena huyo Mnyika anavyojua mipasho inabidi hawe MC.

RED and Bold, sound like a Gay
 
kama kuna ka-ukweli ktk hili....umetumia vigezo gani lkn?

Si unajua wale watu sphincter muscles kwishnei sasa akikaza koo hewa ina escape kupitia back door ending in a GAYish pronounciation like that. Watu wanaongelea mambo ya maendeleo ya wananchi yeye analeta mihemko yake hapa, kanikeraa... ila Bramo kamaliza.
 
Last edited by a moderator:
Kwanini Serikali inayokusanya kodi isiwe accountable kwa wananchi wake?...Kazi ya mbunge ni nyingi na mahitaji ni mengi ya msingi...wananchi mnatakwa muwape madaraka kamili hawa CDM ili na wao tuwapime kwa miaka 5 maana hawa miaka 51 bado hatuna barabara, shule, mahospitali, maish yanazidi kuwa magumu, Tembo wanaisha, elimu inashuka, wakulima wanakopwa, dhahabu inaondoka, Tanzanite inaisha, nickel inakwapuliwa, uraniaum inatoweka, Gesi ishauzwa...

na umegundulika mkondo wa almasi maeneo ya Sengerema na tayari Barrick wameshatoa 10% kwa wahusika na wameshaanza ujenzi wa mgodi.Nchi yetu inaliwa saana jamani watanzania wenzangu
 
Mambo ya maendeleo umeyaongea, ila umekosea kuyaweka kisiasa zaidi.

Jinsi ulivyoandika as if lengo liwe ni kuwin votes kwa ajili ya chadema. Tabia hii inasababisha wakati mwingine kupatiwa vikwazo visivyo na ulazima toka kwa watu wenye itikadi tofauti.

Jitahidini kufikiria maendeleo zaidi kuliko affiliation za vyama. Wabunge wakishachaguliwa wanawatumikia watu wote na kwa lengo la kuleta maendeleo sio kuwawin watu ili wawapigie kura uchaguzi ujao. Ikiwa hivyo yale maeneo ambayo itikadi zake ni fixed against kiongozi hayataendelezwa.

Hongereni kwa jitihada zenu.

Ushauri: Fungueni akaunti ya barabara ya mtaa. Mkiandika taarifa kama hizi andikeni akaunti hiyo na kuwaomba wanavutiwa na shughuli hizo za maendeleo wachangie. You never know anaweza kutokezea "Sabodo" kuwasaidia. Ninachojaribu kusema ni kwamba shirikisheni na wadau wengine wa maendeleo hata kama sio wakazi wa mtaa huo au wanasiasa.

Siku zote nimekua nikisoma posts zako.Leo tu ndo umeandika point.Hongera saana kwa kubadilika.Tanzania ni yetu sote na si ya wachache wenye kung'ang'ania madaraka wakati wameshashindwa kuwatumikia wananchi,na wenye kuneemesha matumbo yao na kuendekeza ufisadi.
 
Wakuu John Mnyika na Halima Mdee Amani iwe Nanyi.

Nipende Kujitambulisha kwenu kama Mpga Kura wenu na Mwanachama Hai wa CHADEMA ninayeishi kwenye Mtaa ambao kimsingi Uko Mpakani mwa Majimbo yenu.
Mtaa huu unaitwa Kulangwa, Mwenyekiti wa Serkali ya Mtaa ni Mzee Shija (CCM).
Diwani (CCM) ni yule Bwana aliyeko Lupango kwa Sasa kwa ile issue ya Kuporomoka Jengo ambapo Kampuni yake ilipewa Kandarasi.
Kuna Mabalozi wengi sana Mtaani pale, lakini Mmoja wapo ni Mama Nyoo (CCM, mwenye Mapenzi ya Dhati Kabisa na CHADEMA)

Nije kwenye Hoja ya Msingi Kabisa ambayo imenifanya Kuwaandikia Waraka Huu (Mtaupata pia kupitia kwenye anuani zenu za Ki Electronic - email).
Kwenye Mpaka wa Majimbo yenu kuna Mtaa unaitwa Kulangwa, ingawa kwa Kiasi kikubwa uko kwa Mnyika kuliko kwa Mdee.
Mpakani kuna Mto Tegeta Ambao kwa Kipindi Kirefu sana umesababisha adha na Usumbufu Mkubwa sana Kwa Wakazi wa Kulangwa hasa Hasa kipindi Cha Mvua.
Usumbufu huo ni kwa wakazi kujikuta hawana Bara Bara ya Uhakika kwani kwenye Mto hakuna Daraja, na Pia huo Mto unamomonyoka as Days goes on
(Picha)
Inasemekana kuwa Mnyika umejitolea 5,000,000 TZS kwa ajili ya Ukarabati wa Ile Bara Bara.
Mwanzoni, Bara Bara ilikuwa inapitia kwenye Shamba la Marehemu Kamanda Liberatus Barlow, na kuna Kipindi ililetaga Mgogoro kati ya Kamnda na Wana Nchi.
Kwa kuwa kile kipande Cha Bara Bara kilichokuwa kinapitia kwenye Sehemu ya Kamanda Libe kimeharibisa sana na Mvua.
Wananchi tumeamua Kufanya Yafuatayo.

1. Tumeamua Kujichangisha Kuanza Ujenzi wa Bara Bara Nyingine, ambayo ndo ipo kwenye Ramani - Zaid ya 1,000,000 TZS
2. Kuna Mwananchi Mmoja amejitolea kipande cha Shamba lake Bara Bara ipite ili isilete Adha kwa katu waliosha jenga Maeneo yale (Mungu amzidishie)
3. Bara Bara imeshaanza Kuchongwa kwa Nguvu zetu.
4. Kwa Sababu Kujenga Daraja Kubwa itachukua Muda, kutokana na Gharama, wananchi tukanona ni Bora tukatafuta a Temporary solution
5. Tumemwaga Roli za Mawe kwa ajili ya Kujenga Zege Mtoni ili Maji yakija, yapite na Yasiendelee Kuchimba Mto na Kuleta Madhara zaid.


Nini tunahitaji Kutoka Kwenu

Wakuu John Mnyika na Halima Mdee , siwezi kuficha ni jinsi gani Wananchi wa eneo lile wanavyowakubali na Kuikubali CHADEMA kwa Ujumla (Tawi la CHADEMA kufunguliwa Soon)
Nipende kuwafahamisha kuwa pale kuna Kura zetu zaid ya 3,000 Tayar.

Nini Kifanyike Kuwa win watu wa Kulangwa

Mahitaj Makuu ya Watu wa Eneo Lile ni Bara Bara na Umeme na Maji.
Tunajua kuwa Maji ni Changamoto kwa Wa Tanzania wote, ila la Bara Bara na Maji, Naamini Kabisa Lipo Ndani ya Uwezo wenu.
Niwafahamishe tu kuwa watu tumejitolea tayar Kuchangia Gharama za Nguzo
Kuna Mtu Kaahidi Nguzo 5, Mwingine 2, Mimi Mwenyewe 2.
Mnaweza Kabisa Kuona ni Jinsi gani Tayar Mazingira Mazuri yameshatengenezwa Pale kwa Nyie Kufunga Goli kwa Kisigino
Watu wanataka Mje mtembelee kwenye ule Mradi wa Bara Bara, pia john Mnyika uwezeshe 5000,000 zije kwenye Serikali ya Kijiji na ku Boost Mradi wa Bara Bara.
Nakuhakikishia Zikifika Ngazi ya Mtaa, hakuna atakaye kula hizo Fedha kwa jinsi watu walivyokuwa na Hamasa, hadi Mabalozi ambao kwao kuna Bendera za CCM.
Huu ni Mmoja kati ya Mitaji Mikubwa ya CHADEMA kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mwakani.
Mdee alishapelekaga Makaravat ambayo kwa Sasa yamezolewa na Myo Tegeta

Natumani nitapata a positive response kutoka kwenu.

Nime attach Picha zinavyoonesha jinsi Mto Tegeta ulivyo Poromoka na Pia niemonesha Ujenzi wa Bara Bara Mpya Ulionzishwa na sie wana Mtaa.
Pia Ujenzi wa Kaji Daraja ka Zege ka Muda

Mungu ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Kulangwa, Mungu Ibariki CHADEMA


Kamanda Mikael P Aweda ,as discussed over the Phone, Please hebu Convey hii Message Tafadhali
cc
FREEma Mbowe , @Dr W Slaa , Zitto, Tumaini Makene , Molemo , Mikael P Aweda .



A good thing ulipomtaja tuu Mnyika,CHADEMA NA TATIZO na hizo kuraaaa....yepo umeshatatua tatizo.Kama mtu kusema daraja kuja na likaja...Mkulu akitoka kuwakuwadia waafrica kwengine kwa wachina pale Addis atakuja ahidi,na magufuli atakupa jilambishlambisha....halafu watasema CCM ndio ina serikali na yenyewe ndio inatenda..Solved..Halafu mnayanyima kura.Kwani kilichotenda ni jina la mnyika/CDM na kura,mkulu akiwa na ziada ya tamaa ya sifa za huyu bwana mdogo.
 
Ungewa PM tu kuliko kutaka sifa kwa kuanzisha thread

Jamaa kalenga....magamba huhitaji waomba na kuwalilia kama magamba wengine...wewe eleza shida halafu wasifie CDM na kueleza utendajiw ao na kukubalika na watu.hat ahel aya majanga itachukulia kma vile wanakwenda zima moto ikulu.

Nona kimekuuma sana..umeshaanza kazi nini?
 
Mkuu kwa bahati nzuri nimejikuta nimezaliwa katika nchi ambayo imesheni Dhahabu, Tanznite, Nickel, Chuma, Coal, Gesi, Almasi, Uranium, Ruby, Greenite, Saphires, Gypsum, Magadi, Chumvi, Mito, Mabonde yenye Rutuba, Maziwa yenye samaki wengi, Bahari kuanzia kusini hadi kaskazini, Visiwa vyenye vivutio vingi vya utalii, Mbuga za Wanyama zenye vivutio vya upekee serengeti, ngorongoro, tarangire, selou, katavi, gombe, milima mirefu duniani mt Kilimanjaro na Mt Meru...Na zaidi nalipa kodi nyingi kuliko mfanyakazi mwingine yeyote katika dunia hii kwani wao huwa wanafile tax return mwisho wa mwaka na kurudishiwa kiasi walichotumia kwenye usafiri na vitendea kazi makazini mwao! Hapa kwetu mfanyakazi analipa kodi kwa kila transaction anayoifanya!... C'mon unaniambia nisiulize Rasilimali zangu na kodi yangu inafanya nini?... Kennedy hapa umemquote vibaya Mkuu... rejea mazingira yaliyomfanya akatoa hilo tamko...

magamba na tamaa zao...tanzania imejaa madini kila mahali.Soon hata wachimbaji hawatakuwa na haja ya kusafiri,labda wale wachuuzi.
 
Ni mambo mazuri mmeyapanga kwa maendeleo ya watu wote, nadhani mbunge wa ubungo na mwenzake wa kawe watashirikiana katika hilo, maana wana mfuko wa maendeleo ya jimbo! Hivo watachota huko!

??????????????????????????????????????? o.k
 
Mkuu Mbona Povu, Huku hadi Mabalozi wa Nyumba Kumi kumi, Nje wana Bendera za CCM, Mioyo yao imefunikwa na Mapenzi ya Dhati kwa CHADEMA.
Ndo wamenituma,
Hebu nawe pitia basi pale Lumumba ukapewe Buku Saba yako Na Kibabu chenu Shigela

Teh teh..usmtishe sana huyo gamba.Vibration kidogo litabanduka na kuanguka ktk sakafu na kuvunjika.Hanui mabalozi wato CCM kwa vile bado wanaweza kula hela za ushihidi wa viwanja mitaani,hela kampeni, etc.
 
Hadi hapo daraja hesabuni limejengwa,ila siku wanawatembelea hakikisheni mna vijana wa CDM wawe wanarekebisha hapo mto mtoni hata kupanga viroba wakiwa na skafu zao au kofia.Muda huo huo patajaa makatapila,na malori.
 
sasa mkuu Bramo mbona pale ilipohamishiwa barabara kuna mlima mkali mno? au kuna mpango wa kujenga daraja ili ukali wa ule mlima upungue?

Mkuu Ye Soya,
Tunaednelea Kuchangishana, last week tumepitisha Jembe cut Kupunguza Kile Kigongo aisee
 
Last edited by a moderator:
Kwanza nimshukuru mleta uzi (thread). Ni kweli kwa kipindi kirefu eneo letu la Kulangwa limekuwa limefungwa (land locked) hasa kipindi cha mvua. UMto tegeta umezunguka maeneo matatu. Kwanza, upande wa magharibi ukiwa unaelekea Mivumoni kuna mto na barabara kipindi cha mvua ni mbaya, hapo tulijitahidi miaka ya nyuma angalau kwa sasa tumedhibiti hali. Pili, upande wa Kaskazini ukiwa unaelekea Sala sala (ambako ndo mleta uzi ameongelea jitihada zinazofanyika) kuna mto ambao unatishia hata nyumba zilizo jirani na mto huo. Barabara hii ilichongwa kwa jitihada zetu wananchi. Tatu, upande wa mashariki ukiwa unaelekea Goba vilevile kuna mto Tegeta ambao magari hayapiti kipindi cha mvua.
Kwa kweli wananchi wamekuwa wanajitahidi ila wanasiasa waliochaguliwa ili kuhamasisha nguvu za wananchi katika mtaa na kata hawafanyi kazi zao. Tatizo la barabara kwa mtaa wetu ni la muda mrefu lakini uongozi haufanyi jitihada za kulitatua. Wenzetu wa Kinzugi hivi karibuni walitengenezewa barabara inayotoka Goba hadi eneo lao. Kinachosikitisha magari yaliyokuwa yakipeleka kifusi cha barabara ya Goba-Kinzugi yalikuwa yakipitia hapo mtoni na hata hayakufanya jitihada yoyote ya kurekebisha barabara ili magari mengine yapite.
Ukija katika suala la umeme mtaa huu vile vile ni kama umefungwa. Maeneo ya jirani yanayozunguka mtaa wa Kulangwa (Mivumoni, Salasala, Kisauke/Madale, na Goba) yote yana umeme. Kulangwa ipo katikati ya maeneo haya lakini mara nyingi tumekuwa tukipigwa danadana na watu wa TANESCO.
Hata kwa suala la elimu, shule za sekondari za kata zote zimewekwa Goba. Na mwisho, usalama wa raia na mali zao umeanza kuwa mashakani. Hivi majuzi kuna kijana alivamiwa na kuporwa hela. Ndani ya miezi mitatu iliyopita matukio ya uporaji yalikuwa zaidi ya matatu. La hivi karibuni likihusisha silaha za moto.

Kwa kuwa kuna uwajibikaji mdogo wa viongozi wa kisiasa ngazi ya mtaa na kata (bahati mbaya wote ni wa CCM) nafikiri kuna haja ya wawakilishi wetu (Wabunge) kulifanyia kazi hili. Mh. Mnyika analijua hili maana licha ya kuandikiwa baraua na wanamtaa yeye mwenyewe alijionea hali ya barabara alivyokuja kuzindua tawi pale mivumoni.

Mwisho, niwashi waheshimiwa Wabunge watupiganie wana Kulangwa ili bajeti ya barabara, Ujenzi wa kituo cha Polisi itengwe.
 
Wakuu John Mnyika na Halima Mdee Amani iwe Nanyi.

Nipende Kujitambulisha kwenu kama Mpga Kura wenu na Mwanachama Hai wa CHADEMA ninayeishi kwenye Mtaa ambao kimsingi Uko Mpakani mwa Majimbo yenu.
Mtaa huu unaitwa Kulangwa, Mwenyekiti wa Serkali ya Mtaa ni Mzee Shija (CCM).
Diwani (CCM) ni yule Bwana aliyeko Lupango kwa Sasa kwa ile issue ya Kuporomoka Jengo ambapo Kampuni yake ilipewa Kandarasi.
Kuna Mabalozi wengi sana Mtaani pale, lakini Mmoja wapo ni Mama Nyoo (CCM, mwenye Mapenzi ya Dhati Kabisa na CHADEMA)

Nije kwenye Hoja ya Msingi Kabisa ambayo imenifanya Kuwaandikia Waraka Huu (Mtaupata pia kupitia kwenye anuani zenu za Ki Electronic - email).
Kwenye Mpaka wa Majimbo yenu kuna Mtaa unaitwa Kulangwa, ingawa kwa Kiasi kikubwa uko kwa Mnyika kuliko kwa Mdee.
Mpakani kuna Mto Tegeta Ambao kwa Kipindi Kirefu sana umesababisha adha na Usumbufu Mkubwa sana Kwa Wakazi wa Kulangwa hasa Hasa kipindi Cha Mvua.
Usumbufu huo ni kwa wakazi kujikuta hawana Bara Bara ya Uhakika kwani kwenye Mto hakuna Daraja, na Pia huo Mto unamomonyoka as Days goes on
(Picha)
Inasemekana kuwa Mnyika umejitolea 5,000,000 TZS kwa ajili ya Ukarabati wa Ile Bara Bara.
Mwanzoni, Bara Bara ilikuwa inapitia kwenye Shamba la Marehemu Kamanda Liberatus Barlow, na kuna Kipindi ililetaga Mgogoro kati ya Kamnda na Wana Nchi.
Kwa kuwa kile kipande Cha Bara Bara kilichokuwa kinapitia kwenye Sehemu ya Kamanda Libe kimeharibisa sana na Mvua.
Wananchi tumeamua Kufanya Yafuatayo.

1. Tumeamua Kujichangisha Kuanza Ujenzi wa Bara Bara Nyingine, ambayo ndo ipo kwenye Ramani - Zaid ya 1,000,000 TZS
2. Kuna Mwananchi Mmoja amejitolea kipande cha Shamba lake Bara Bara ipite ili isilete Adha kwa katu waliosha jenga Maeneo yale (Mungu amzidishie)
3. Bara Bara imeshaanza Kuchongwa kwa Nguvu zetu.
4. Kwa Sababu Kujenga Daraja Kubwa itachukua Muda, kutokana na Gharama, wananchi tukanona ni Bora tukatafuta a Temporary solution
5. Tumemwaga Roli za Mawe kwa ajili ya Kujenga Zege Mtoni ili Maji yakija, yapite na Yasiendelee Kuchimba Mto na Kuleta Madhara zaid.


Nini tunahitaji Kutoka Kwenu

Wakuu John Mnyika na Halima Mdee , siwezi kuficha ni jinsi gani Wananchi wa eneo lile wanavyowakubali na Kuikubali CHADEMA kwa Ujumla (Tawi la CHADEMA kufunguliwa Soon)
Nipende kuwafahamisha kuwa pale kuna Kura zetu zaid ya 3,000 Tayar.

Nini Kifanyike Kuwa win watu wa Kulangwa

Mahitaj Makuu ya Watu wa Eneo Lile ni Bara Bara na Umeme na Maji.
Tunajua kuwa Maji ni Changamoto kwa Wa Tanzania wote, ila la Bara Bara na Maji, Naamini Kabisa Lipo Ndani ya Uwezo wenu.
Niwafahamishe tu kuwa watu tumejitolea tayar Kuchangia Gharama za Nguzo
Kuna Mtu Kaahidi Nguzo 5, Mwingine 2, Mimi Mwenyewe 2.
Mnaweza Kabisa Kuona ni Jinsi gani Tayar Mazingira Mazuri yameshatengenezwa Pale kwa Nyie Kufunga Goli kwa Kisigino
Watu wanataka Mje mtembelee kwenye ule Mradi wa Bara Bara, pia john Mnyika uwezeshe 5000,000 zije kwenye Serikali ya Kijiji na ku Boost Mradi wa Bara Bara.
Nakuhakikishia Zikifika Ngazi ya Mtaa, hakuna atakaye kula hizo Fedha kwa jinsi watu walivyokuwa na Hamasa, hadi Mabalozi ambao kwao kuna Bendera za CCM.
Huu ni Mmoja kati ya Mitaji Mikubwa ya CHADEMA kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mwakani.
Mdee alishapelekaga Makaravat ambayo kwa Sasa yamezolewa na Myo Tegeta

Natumani nitapata a positive response kutoka kwenu.

Nime attach Picha zinavyoonesha jinsi Mto Tegeta ulivyo Poromoka na Pia niemonesha Ujenzi wa Bara Bara Mpya Ulionzishwa na sie wana Mtaa.
Pia Ujenzi wa Kaji Daraja ka Zege ka Muda

Mungu ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Kulangwa, Mungu Ibariki CHADEMA


Kamanda Mikael P Aweda ,as discussed over the Phone, Please hebu Convey hii Message Tafadhali
cc
FREEma Mbowe , @Dr W Slaa , Zitto, Tumaini Makene , Molemo , Mikael P Aweda .



Bramo nime salute uandishi wako yaani hata mtu ambaye hajui issue akisoma anakosa swali. Lakini jambo uliloandika hakika ni nyeti kwani linahusu maendeleo hakika mwenyewe siishi dar lakini naunga mkono hoja
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom