Attention to John Mnyika na Halima Mdee

Attention to John Mnyika na Halima Mdee

Bramo

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2009
Posts
13,254
Reaction score
10,252
Wakuu John Mnyika na Halima Mdee Amani iwe Nanyi.

Nipende Kujitambulisha kwenu kama Mpga Kura wenu na Mwanachama Hai wa CHADEMA ninayeishi kwenye Mtaa ambao kimsingi Uko Mpakani mwa Majimbo yenu.
Mtaa huu unaitwa Kulangwa, Mwenyekiti wa Serkali ya Mtaa ni Mzee Shija (CCM).
Diwani (CCM) ni yule Bwana aliyeko Lupango kwa Sasa kwa ile issue ya Kuporomoka Jengo ambapo Kampuni yake ilipewa Kandarasi.
Kuna Mabalozi wengi sana Mtaani pale, lakini Mmoja wapo ni Mama Nyoo (CCM, mwenye Mapenzi ya Dhati Kabisa na CHADEMA)

Nije kwenye Hoja ya Msingi Kabisa ambayo imenifanya Kuwaandikia Waraka Huu (Mtaupata pia kupitia kwenye anuani zenu za Ki Electronic - email).
Kwenye Mpaka wa Majimbo yenu kuna Mtaa unaitwa Kulangwa, ingawa kwa Kiasi kikubwa uko kwa Mnyika kuliko kwa Mdee.
Mpakani kuna Mto Tegeta Ambao kwa Kipindi Kirefu sana umesababisha adha na Usumbufu Mkubwa sana Kwa Wakazi wa Kulangwa hasa Hasa kipindi Cha Mvua.
Usumbufu huo ni kwa wakazi kujikuta hawana Bara Bara ya Uhakika kwani kwenye Mto hakuna Daraja, na Pia huo Mto unamomonyoka as Days goes on
(Picha)
Inasemekana kuwa Mnyika umejitolea 5,000,000 TZS kwa ajili ya Ukarabati wa Ile Bara Bara.
Mwanzoni, Bara Bara ilikuwa inapitia kwenye Shamba la Marehemu Kamanda Liberatus Barlow, na kuna Kipindi ililetaga Mgogoro kati ya Kamnda na Wana Nchi.
Kwa kuwa kile kipande Cha Bara Bara kilichokuwa kinapitia kwenye Sehemu ya Kamanda Libe kimeharibisa sana na Mvua.
Wananchi tumeamua Kufanya Yafuatayo.

1. Tumeamua Kujichangisha Kuanza Ujenzi wa Bara Bara Nyingine, ambayo ndo ipo kwenye Ramani - Zaid ya 1,000,000 TZS
2. Kuna Mwananchi Mmoja amejitolea kipande cha Shamba lake Bara Bara ipite ili isilete Adha kwa katu waliosha jenga Maeneo yale (Mungu amzidishie)
3. Bara Bara imeshaanza Kuchongwa kwa Nguvu zetu.
4. Kwa Sababu Kujenga Daraja Kubwa itachukua Muda, kutokana na Gharama, wananchi tukanona ni Bora tukatafuta a Temporary solution
5. Tumemwaga Roli za Mawe kwa ajili ya Kujenga Zege Mtoni ili Maji yakija, yapite na Yasiendelee Kuchimba Mto na Kuleta Madhara zaid.

Nini tunahitaji Kutoka Kwenu

Wakuu John Mnyika na Halima Mdee , siwezi kuficha ni jinsi gani Wananchi wa eneo lile wanavyowakubali na Kuikubali CHADEMA kwa Ujumla (Tawi la CHADEMA kufunguliwa Soon)
Nipende kuwafahamisha kuwa pale kuna Kura zetu zaid ya 3,000 Tayar.

Nini Kifanyike Kuwa win watu wa Kulangwa

Mahitaj Makuu ya Watu wa Eneo Lile ni Bara Bara na Umeme na Maji.
Tunajua kuwa Maji ni Changamoto kwa Wa Tanzania wote, ila la Bara Bara na Maji, Naamini Kabisa Lipo Ndani ya Uwezo wenu.
Niwafahamishe tu kuwa watu tumejitolea tayar Kuchangia Gharama za Nguzo
Kuna Mtu Kaahidi Nguzo 5, Mwingine 2, Mimi Mwenyewe 2.
Mnaweza Kabisa Kuona ni Jinsi gani Tayar Mazingira Mazuri yameshatengenezwa Pale kwa Nyie Kufunga Goli kwa Kisigino
Watu wanataka Mje mtembelee kwenye ule Mradi wa Bara Bara, pia john Mnyika uwezeshe 5000,000 zije kwenye Serikali ya Kijiji na ku Boost Mradi wa Bara Bara.
Nakuhakikishia Zikifika Ngazi ya Mtaa, hakuna atakaye kula hizo Fedha kwa jinsi watu walivyokuwa na Hamasa, hadi Mabalozi ambao kwao kuna Bendera za CCM.
Huu ni Mmoja kati ya Mitaji Mikubwa ya CHADEMA kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mwakani.
Mdee alishapelekaga Makaravat ambayo kwa Sasa yamezolewa na Myo Tegeta

Natumani nitapata a positive response kutoka kwenu.

Nime attach Picha zinavyoonesha jinsi Mto Tegeta ulivyo Poromoka na Pia niemonesha Ujenzi wa Bara Bara Mpya Ulionzishwa na sie wana Mtaa.
Pia Ujenzi wa Kaji Daraja ka Zege ka Muda

Mungu ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Kulangwa, Mungu Ibariki CHADEMA

Kamanda Mikael P Aweda ,as discussed over the Phone, Please hebu Convey hii Message Tafadhali
cc
FREEma Mbowe , @Dr W Slaa , Zitto, Tumaini Makene , Molemo , Mikael P Aweda .

Last edited by a moderator:
Mkuu hongereni kwa kujitolea na kujiletea maendeleo. Nadhani wabunge hao wamekusikia.

Nami nikushauri jambo moja kwamba katika kujenga zege mtoni (drift) jitahidini mpate wataalam wawasaidie vinginevyo mtamwaga pesa mtoni. Nasema hivyo kwa sababu nimewahi kuona mtaa mmoja jimboni ubungo (maeneo ya kimara) walijitolea na kukusanya mawe na kujenga drift bila utaalam, mvua zilivyonyesha zikazoa kila kitu wakarudi back to square one.

Kila la kheri
 
Kwanini Serikali inayokusanya kodi isiwe accountable kwa wananchi wake?...Kazi ya mbunge ni nyingi na mahitaji ni mengi ya msingi...wananchi mnatakwa muwape madaraka kamili hawa CDM ili na wao tuwapime kwa miaka 5 maana hawa miaka 51 bado hatuna barabara, shule, mahospitali, maish yanazidi kuwa magumu, Tembo wanaisha, elimu inashuka, wakulima wanakopwa, dhahabu inaondoka, Tanzanite inaisha, nickel inakwapuliwa, uraniaum inatoweka, Gesi ishauzwa...
 
mleta mada umenikumbusha miaka ya nyuma ilikuwa kila jumamosi kuna kitu kilikuwa kinaitwa utawala. Ilikuwa ikifika siku hiyo watu wanajitolea kufanya kazi kwa pamoja, na ilikuwa inafanyika kazi ya nguvu kikweli. Ilikuwa inapangwa kama ni daraja linajengwa au ni kuelekeza maji sehemu za mashambani kazi hiyo inafanyika na kama kuna aliyekosa anabambuliwa, wakati ule kulikuwa na uongozi wa mwalimu, watu waliishi kwa upendo na mwalimu alikuwa ni mfano. Nina imani hata sasa watu wakiamua wanaweza.
Hongereni sana watu wa kulangwa mmeonyesha mfano. Siyo kila kitu tungoje serikali. Serikali isishindwe na sisi tushindwe
 
Mambo ya maendeleo umeyaongea, ila umekosea kuyaweka kisiasa zaidi.

Jinsi ulivyoandika as if lengo liwe ni kuwin votes kwa ajili ya chadema. Tabia hii inasababisha wakati mwingine kupatiwa vikwazo visivyo na ulazima toka kwa watu wenye itikadi tofauti.

Jitahidini kufikiria maendeleo zaidi kuliko affiliation za vyama. Wabunge wakishachaguliwa wanawatumikia watu wote na kwa lengo la kuleta maendeleo sio kuwawin watu ili wawapigie kura uchaguzi ujao. Ikiwa hivyo yale maeneo ambayo itikadi zake ni fixed against kiongozi hayataendelezwa.

Hongereni kwa jitihada zenu.

Ushauri: Fungueni akaunti ya barabara ya mtaa. Mkiandika taarifa kama hizi andikeni akaunti hiyo na kuwaomba wanavutiwa na shughuli hizo za maendeleo wachangie. You never know anaweza kutokezea "Sabodo" kuwasaidia. Ninachojaribu kusema ni kwamba shirikisheni na wadau wengine wa maendeleo hata kama sio wakazi wa mtaa huo au wanasiasa.
 
Kwanini Serikali inayokusanya kodi isiwe accountable kwa wananchi wake?...Kazi ya mbunge ni nyingi na mahitaji ni mengi ya msingi...wananchi mnatakwa muwape madaraka kamili hawa CDM ili na wao tuwapime kwa miaka 5 maana hawa miaka 51 bado hatuna barabara, shule, mahospitali, maish yanazidi kuwa magumu, Tembo wanaisha, elimu inashuka, wakulima wanakopwa, dhahabu inaondoka, Tanzanite inaisha, nickel inakwapuliwa, uraniaum inatoweka, Gesi ishauzwa...
My fellow Tanzanian, ask not what your country can do for you, ask what you can do for your country.

John F. Kennedy
 
Wakishatoa huo msaada uliowaomba halafu wasipate hizo kura, mtawarudishia hela zao?
 
Majitu merngine bana, kwani ukijenga daraja lazima ufungue Tawi la chama? hizi siasa za kuokoteza ni janga kweli.
Kwani hao watu hawana mapenzi na CUF au TLP mpaka kiwe chama chenu cha matukio? wakati mwingine mlikiwa wapi nyie wafanya fujo?mbona hamkuandamana ili daraja lijengwe siku nyingi.
Haya nenda ukalipwe na Makene sh. Elf 10000 hapo Kinondoni.
 
My fellow Tanzanian, ask not what your country can do for you, ask what you can do for your country.

John F. Kennedy

Mkuu kwa bahati nzuri nimejikuta nimezaliwa katika nchi ambayo imesheni Dhahabu, Tanznite, Nickel, Chuma, Coal, Gesi, Almasi, Uranium, Ruby, Greenite, Saphires, Gypsum, Magadi, Chumvi, Mito, Mabonde yenye Rutuba, Maziwa yenye samaki wengi, Bahari kuanzia kusini hadi kaskazini, Visiwa vyenye vivutio vingi vya utalii, Mbuga za Wanyama zenye vivutio vya upekee serengeti, ngorongoro, tarangire, selou, katavi, gombe, milima mirefu duniani mt Kilimanjaro na Mt Meru...Na zaidi nalipa kodi nyingi kuliko mfanyakazi mwingine yeyote katika dunia hii kwani wao huwa wanafile tax return mwisho wa mwaka na kurudishiwa kiasi walichotumia kwenye usafiri na vitendea kazi makazini mwao! Hapa kwetu mfanyakazi analipa kodi kwa kila transaction anayoifanya!... C'mon unaniambia nisiulize Rasilimali zangu na kodi yangu inafanya nini?... Kennedy hapa umemquote vibaya Mkuu... rejea mazingira yaliyomfanya akatoa hilo tamko...
 
Mkuu, wapi nimesema usiulize pesa yako inafanya nini na inatumikaje?. Kwa nini na kwa kigezo gani unasema nimem-quote vibaya katika muktadha wako.
 
Ungewa PM tu kuliko kutaka sifa kwa kuanzisha thread

mkuu unamkatisha mwenzako tamaa kwani ajafanya makosa kutuambia nasi tunaweza tukawaiga kuchangishana kama walivyofanya katika kupiga hatua kimaendeleo.
 
Nzuri hiyo

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Majitu merngine bana, kwani ukijenga daraja lazima ufungue Tawi la chama? hizi siasa za kuokoteza ni janga kweli.
Kwani hao watu hawana mapenzi na CUF au TLP mpaka kiwe chama chenu cha matukio? wakati mwingine mlikiwa wapi nyie wafanya fujo?mbona hamkuandamana ili daraja lijengwe siku nyingi.
Haya nenda ukalipwe na Makene sh. Elf 10000 hapo Kinondoni.

Mkuu Mbona Povu, Huku hadi Mabalozi wa Nyumba Kumi kumi, Nje wana Bendera za CCM, Mioyo yao imefunikwa na Mapenzi ya Dhati kwa CHADEMA.
Ndo wamenituma,
Hebu nawe pitia basi pale Lumumba ukapewe Buku Saba yako Na Kibabu chenu Shigela
 
Hongera sana Bramo, Tanzania inaitaji watu kama wewe-lakini pia nikili kijifunza kitu kutoka kwako. Nafikiria nini chakufanya kwa ajiri ya kijiji/kata/ yangu.

Pongezi zangu Kwa ZeMorcopolo-for the first time he has impressed me (maelezo yake mengi sikutaka kuya-quote).
 
Ni mambo mazuri mmeyapanga kwa maendeleo ya watu wote, nadhani mbunge wa ubungo na mwenzake wa kawe watashirikiana katika hilo, maana wana mfuko wa maendeleo ya jimbo! Hivo watachota huko!
 
Back
Top Bottom