Atokewa na Mwl Nyerere, apewa ujumbe.

Ndibalema

JF-Expert Member
Apr 26, 2008
10,956
4,648
Hivi karibuni kuna mwanamke mmoja Mkoani Ruvuma alijitokeza mbele ya kituo cha terevisheni cha TBC1 na kusema (kwa uhakika) kuwa amekuwa akitokewa na mwalimu Nyerere na kupewa maagizo ampelekee Rais jakaya Kikwete kuwa Chama(CCM) kimeacha maadili na kinafanya mambo ambayo hayampendezi Mwalimu.
Wengi walimpuuza huyu mama.
Naomba wana JF mnisaidie, Hivi kitu kama hicho kinawezekana?
Kuna dalili ya ukweli wowote juu ya anachokisema huyu mama?
 
kutokewa haiwezekani. ni akili yake imeshajituni hivyo na kwa sbb hiyo amemwona nyerere ambaye yupo akilini mwake tu! anajifanya kama wale watoto wa fatima ureno lakini suala la hao watoto lilikuwa la kiroho sio la kisiasa!
 
Katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu, tutegemee watu wa aina hiyo wengi tu, wapo wanaoweza kus
sema eti chenge ametokewa awe Rais wa nji hii!!!
 
Nchi haiwezi kuendeshwa kwa mambo kama haya na hayakubaliki popote pale.Mtu akiisha kufa amekufa tu cha msingi kama aliacha maandiko ni kuyasoma, kuya elewa na kufanyia kazi yale ambayo yanaweza kutusaidia au kuteelimisha au kutuasa na siyo siyo suala la mtu kuibuka na kusema kuwa mara Nyerere kanitokea leo kasema hivi.Haya mambo yakiiachwa kuna mtu ataibuka na kusema Kinjikitile kasema tupigine tena vita vya maji maji, hii siyo aibu kweli?
 
Aende kanisani!!

kule wao wanaamini mambo kama haya, manabii kama wakina Paul wanaoteshwa usingizini na ndio chanzo cha Bible!
 
Back
Top Bottom