Atlas Primary School - Madale, Dar

dar mtoto anatoka mbagala anasoma kibaha .
 
Daaah! kwa kweli kwa Aziz Alli na Madale kwa mtoto ni mbali sanaa! mbona hapo kuna shule nyingi tu nzuri ziko karibu kama Holy Cross ipo Mtoni Kijichi!
 
Hicho kibasi kinapitaga home kwetu.kwanza wanafika SAA tatu kasoro watoto hao shule,...wanachoka sana
 

Yaani ni bora wengi tunaliona hili.. Nimewataarifu mara kwa mara hawaelewi ila this time watakumbana na mkono wa sheria
 
Ona dharau hizo sasa...
Mi mtt wa ndg yangu ndio alikua huko but ashamaliza std 7 kitambo
 
Bora umpeleke ubungo...madale mbali
 
Kwanza huyo jamaa mwenye shule ni jeuri sana,alitoa majibu ya jeuri kwenye kikao cha wazazi mimi sikuamini kama ni yeye.Na hilo suala la usafiri kurekebisha wanalizungumza sana ila utekelezaji ni sifuri

Muda ni hakimu mzuri, hizi kelele tunazopiga ni kwa manufaa yake ila kwakua anajidai kutojali ipo siku itadoda
 
Muda ni hakimu mzuri, hizi kelele tunazopiga ni kwa manufaa yake ila kwakua anajidai kutojali ipo siku itadoda
Sasa hivi anatamba maana shule zake kidogo ada ipo chini lakini ipo siku shule yake itadoda asipowasikiliza wadau
 
ATLAS MADALE PRIMARY SCHOOL - PS0203126

WALIOSAJILIWA : 263
WALIOFANYA MTIHANI : 263
WASTANI WA SHULE : 191.8669
KUNDI LA SHULE : Watahiniwa 40 au zaidi
NAFASI YA SHULE KWENYE KUNDI LAKE KIWILAYA: 8 kati ya 96
NAFASI YA SHULE KWENYE KUNDI LAKE KIMKOA : 35 kati ya 433
NAFASI YA SHULE KWENYE KUNDI LAKE KITAIFA : 160 kati ya 9736
 
Halafu walivyo watu wa ajabu siku ukienda kumhamisha mtoto pale wanakupeleka kwa mwalimu wao sijui ni mshauri au ni mwalimu wa taalum.Anaanza kukuhoji kwa unyenyekevu ooohhh tatizo liko wapi,ukishamwelezea anakwambia tupe muda tutajirekebisha na umwache mtoto aendelee kusoma hapahapa.Mimi nikawaambia jirekebisheni kwanza mkikaa sawa nitamrudisha mtoto hapa,basi toka mwezi wa tisa mwaka huu mpaka leo hawataki kunipa namba ya uhamisho wananizungusha mara jina la mtoto limekosewa,mara mwalimu anayeshughulikia hayupo yaani ili mradi ni karaha tu
 
Mimi nakulipa hela huwezi nilitea ujeuri.... Mbona shule kubwa Kama feza hawana ujeuri

Tatizo ni human nature, management system n.k...hapa ndipo binadamu tunapotofautiana.. Huyu mmiliki wa shule anakua kama wakinga, yaani anafanya biashara kama hataki vile
 
Academic wise wako poa sana, madhaifu yao ni usafiri tu na mengine madogo madogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…