Atiwa mbaroni kwa tuhuma za 'kumchinja' dada yake

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Mkazi wa kijiji cha Wavu kata ya Shabaka wilayani Nyang'hwale mkoani Geita Shilinde Mbushi [41] akishirikiana na mwanaye Ndebile Shilinde [21] anadaiwa kumuua dada yake Kweji Mbushi [40]

RPC%20Geita%20Mponjoli.jpg

Mponjoli Rodson Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita

Mkazi huyo anatuhumiwa kufanya mauaji hayo kwa kumkata kata kwa kitu chenye ncha kali na kutenganisha kichwa na kiwiliwili chake na kisha kutoweka na kichwa chake June 8 saa nne za usiku kabla ya kichwa hicho kupatikana juzi na watuhumiwa tayari wanashikiliwa na polisi.

Kamanda Mponjoli Rodson amefafanua kuwa kichwa cha marehemu Kweji kilipatikana juzi kikiwa kimetelekezwa huku akitoa rai kwa jamii kuacha vitendo vya kujichukulia sheria mikononi.

Mponjoli Rodson Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita anazungumzia tukio hilo la kikatili wa aina yake.

Chanzo: UTV
 
Labda hizi ndizo dalili za mwisho wa dunia na kwa hakika mwisho wake utaanzia Tanzania nchi inayoendelea kulaaniwa kila kukicha. Au tulikula nyama ya mtu?
 
Hivi walioko Geita ni watu wenye nafsi kweli? kila nikijaribu kutafakari yale yabayoripotiwa kutoka geita napata wasiasi kama watu wa kule wanatokana na Adamu au mnyama tu. Kuzimu inaweza kuwa salama kuishi kuliko Geita.
 
Duh! awamu hii ni kuchinjana kwenda mbele au kutokana na ile kauli ya tutaishi kama shetani?. Ee Mwenyezi Mungu tuepushe na balaa hili la kuchinjana.
 
Back
Top Bottom