Atimua kwa mganga baada ya kushindwa masharti

Atimua kwa mganga baada ya kushindwa masharti

X_INTELLIGENCE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2014
Posts
10,778
Reaction score
14,987
Kuna dada mmoja anaitwa Kasinde alikuwa anajimudu sana kifedha alikuwa na majumba na magari mengi ya kifahari, kutokana na hali ngumu ya maisha aliyokuwa nayo chinchilla coat aliamua kumfuata Kasinde ili amsaidie ikiwezekana apate mafanikio kama aliyokuwa nayo yeye. Kasinde akamuuliza mara mbili mbili chinchilla coat kuwa ana moyo mgumu? chinchilla coat akasema kuwa kwa hali yoyote kwa vyovyote vile yupo teyari.
hqdefault.jpg

Siku ikawadia Kasinde na chinchilla coat wakachukuana hadi huko kisiwani pemba, walipofika huko walimkuta Nyani Ngabu anaswali hivyo walisubiri amalize kuswali kisha waendelee na maongezi juu ya kilichowapeleka.

Baada ya Nyani Ngabu kumaliza kuswali walisalimiana na Kasinde ilionekana wazi kwa chinchilla coat kuwa Nyani Ngabu na Kasinde wanafahamiana kwa muda mrefu na hicho ndicho kilikuwa sahihi, Nyani Ngabu alikuwa mganga mashughuri sana uko kisiwani pemba. Kasinde akamwambia Nyani Ngabu kuwa chinchilla coat anataka kuwa kama yeye.
bag-of-cash-resized.jpg

Pembeni mwa chumba walimokuwemo kulikuwa na mabegi matatu, Nyani Ngabu akamwambia chinchilla coat aende akachukue begi moja, bila hiyana chinchilla coat akaenda kuchukua moja kati ya mabegi yale matatu kama alivyoagizwa lilikuwa begi zito tofauti na muonekano wake wa nje. Baada ya kulichukua lile begi Nyani Ngabu akamwambia chinchilla coat alifungue lile begi, chinchilla coat hakuamini macho yake baada ya kulifungua lile begi kwani ndani ya lile begi kulikuwa kumesheheni mibunda ya fedha isiyokuwa na idadi. Nyani Ngabu akamwambia lote ilo ni lakwako na utarudi nalo nyumbani leo ila ukifika nyumbani mwanao mpendwa multiphill90 hutomkuta utakuta amesha safiri kwenda kwenye ile safari ambayo mtu akienda huwa harudi. chinchilla coat alitetemeka sana akamuomba Nyani Ngabu muda wa kufikiri. Wakatoka nje yeye na Kasinde , Kasinde akamwambia kubari ndugu yangu bora wewe umeambiwa umtoe mwanao mpendwa mimi nilitoa kizazi changu kabisa hivyo sitokuja kupata mtoto kabisa na ukikataa hutokuja kufanikiwa tena.. chinchilla coat alitetemeka sana na alijuta kwa uamuzi wake wa kutamani vitu asivyo viweza.
MTQxMTc0OTk0NjYyODYwNDg0.jpg

Uzalendo ulimshinda chinchilla coat hakuweza kufanya alichoagizwa na Nyani Ngabu chinchilla coat na Kasinde waliondoka kwa mganga.

.......itaendelea

NB: majina ya wahusika hayahusiani na uhalisia wa hii story, nisameheni kwa kutumia majina yenu ila lengo ni kuelimishana
 
Naikumbuka.. Nitajitahid nikupatie audio ya hii kitu kwakua muhusika mwenyewe nipo nae karibu sana.. Asante umeielezea kwa undani sana..
Also nitaulizia alipo yule dada wa hammer
itakuwa vyema mkuu
 
Back
Top Bottom