Atheist wengi hawajui wanachokitafuta

Kutokujua kwangu alilopanga Mungu kunanifanya nisijue kama amebadilisha maono. Naweza kusema kuwa maono yake Mungu ni mimi mtu wa peponi kwa sababu ameona kuwa nitakuwa nafanya ibada. Kwaio lazima nitazifanya izo ibada kwaio nitakuwa sijajihangaisha bali nitakuwa natekeleza kile kile alichokiona Mungu wangu.
Ikiwa maono yake ni kwamba mimi ni mtu wa motoni (Allah aniepushie) basi bila shaka itakuwa sifanyi ibadi mpaka kufa kwangu na aliniona zamani kuwa nitakuwa naenda kinyume nae.
 
Kutokujua kwako akubadilishi alilopanga juu yako kipi uelewi !!! unachofanya wewe ni kujichosha kwasababu tayari ameshamua na hakuna wakubadilisha ata ukiswali bila kula , hii ndio tafasiri ya kusukuma ukuta na kujitoa jasho bureee
Tayari safari imeanza kukushinda. mi nilikuomba uwe unanijibu ila tayari unaanza kusepa.

Hakuna mahali ambapo panasema kuwa Mungu ameamuwa fulani aende motoni (kabla ya siku yake ya hukumu). Bali tunasema kuwa ANAJUA wewe utaishia wapi.
Malumbano yenu nimeyafuatilia na nimeona hamuwezi kufika mwisho unaofanana . Kwa vile kila moja anazo Imani zake. Ni vizuri tukaheshimu kila upande bila shurti. Kwa ndiyo democracy yenyewe.

Mungu awepo au asiwepo libakie kuwa swala la mtu binafsi, na lisiwe shurti kwa jamii nzima. Upeo wetu wa kufafanua uwepo au kutokuwa kwa Mungu unalingana na mapokeo yetu. Tuvumiliane
 
Mkuu, mimi sijachangia hii mada ili nimlazimishe mtu kuamini nnachoamini. Ni wajibu wangu kufundisha ninachokijua, na sio wajibu wangu kumlazimisha mtu akubali nnachokubaliana nacho mimi.

Wameuliza, nimewajibu. Akikubaliana na jibu sawa, asipokubaliana nalo kwa sababu tu anachukizwa na nnachoamini mimi, hilo ni juu yake.

Kuna mdau hapo nimemwambia yupo huru kuchagua kama kuamini uwepo wa mungu au kuupinga, simlazimishi mtu mkuu.

JF hakuna mjadala wa imani uliofikia maelewano. Shida ni kwamba wengine wanachangia wakiwa hawana elimu na kulazimisha watakavyo
 
1. Kwahiyo unathubitishia kuwa Mungu wako ana maono tu lakini apangi ?
 
1. Kwahiyo unathubitishia kuwa Mungu wako ana maono tu lakini apangi ?
Yapo anayopanga na yapo asiyoyapanga bali anajua matokeo yake ni yapi.

Inabidi hili swali ndio umeshindwa kulijibu?

Utajuaje kama maono yake yamebadilika baada ya kuacha kusali ikiwa hujui mwanzo maono yake ni yapi?
 
mfano hapa.mimi si kiranga ila umenijibu kwa sababu nimeuliza swali.lakini jibu hili si sahihi.

maana si wewe au mkristo anayejua ni kwanini Mungi hajawahi kuonekana kwa macho.
Tabu sasa wanajifanya wana majibu yote . wafia dini wanashangaza sana..
 
U a right sir [emoji120][emoji40]
 
mimi najua ndio maana nikakuuliza wewe muislamu,biblia haijasema kwanini Mungu hataki tuonane naye.
 
Yapo anayopanga na yapo asiyoyapanga bali anajua matokeo yake ni yapi.

Inabidi hili swali ndio umeshindwa kulijibu?

Utajuaje kama maono yake yamebadilika baada ya kuacha kusali ikiwa hujui mwanzo maono yake ni yapi?
Maono ya Mungu ayajawai kubadilika kwasababu mipango yake wala ashauriani na mtu , na tena anasema ameandika kila kitu kwenye daftari sasa inabadilika nini ? huo ni wasiwasi wako wewe ili uendelee kujichosha , kama Mungu ameandika wewe ni wamotoni ata ukiswali uendi peponi na kama ameandika wewe wa peponi ata usiposwali uendi motoni , wewe unachofanya ni kujichosha uwezi badilisha kitu
 
Nimekujibu mawazo ya Mungu ayajawai kubadilika na hakuna wa kuyabadilisha , ndio maana kila kitu kakiandika kwenye kitabu kuwa wewe chilubi kama ni wamotoni ata ukeshe ukifanya ibada wewe jikoni tu , na kama kwenye daftari umeandikwa wewe ni wa peponi ata ulewe na ulale bar utaenda tu peponi hakuna wa kubadili hicho kilichoandikwa
 
Mungu mnaemtangaza amejaa makando mengi wacha tumuhoji
 
kama Mungu yupo, kwa nini kuna watu wanateseka na maradhi mahospitalini? hao walimkosea nini Mungu?
nani alikuambia kumtumikia Mungu huwezi umwa... kuumwa kwako au matatizo yake hayamuondele UMungu wake
 
mimi najua ndio maana nikakuuliza wewe muislamu,biblia haijasema kwanini Mungu hataki tuonane naye.
Aya niliyokuletea hapo juu imeshasema kuwa hawezekani mtu akamuona akisha akaendelea kuishi. Jibu lipo wazi kwetu sisi waislam kwanini hatumuoni kwa usahih kabisa. Kama upande wenu bibilia haijakuwekeeni bayana tena hayo ni ya kwenu na ni wajibu wako kumuuliza mwalimu wako na kumhoji.

Musa a.s alitaka kumuona Allah baada ya shinikizo kutoka kwa mayahudi, alipoenda aliambiwa utizame mlima, ikiwa utabakia basi utaniona, matokeo yake mlima ulivurugika na yeye kuzimia. Kwaio sio kwamba Mungu kajificha, bali haonekani
 
Unajichosha kuswali ili iweje kumbe majibu Mungu wako anayo ?kumbe Mungu wako ndio anaamua wa motoni au wa peponi wala sio matendo yako
Tutaingia peponi kwa rehma zake ila muovu haingii peponi mzee.

Pepo inapambaniwa na inatafutwa.
 
Mungu amesema kuwa atakaefanya wema ataenda peponi na atakaefanya mabaya ataenda motoni. Kwaio Mungu ameshajua kuwa yoyote atakaefanya mema huyo ni mtu wa peponi, sasa wewe hujui mpaka siku yako ya kufa utakuwa una amal gani. Na Kama Mungu anajua mimi mtu wa Peponi, basi ni kwa sababu ameshajua kuwa nitakua nafanya ibada na ndio maana akajua ivo na haitobadilika.
 
kwahiyo unaamini qurani imeeleza vyema kwamba Mungu hajajificha si ndio???simply utukufu wake tu ndio unatutenga naye.

haya nipe connection kwanini unaamini ukisali atakusaidia katika utukufu huu?
 

Ni kweli. Hebu sikiliza hizi debates 2: ,
 
kwahiyo unaamini qurani imeeleza vyema kwamba Mungu hajajificha si ndio???simply utukufu wake tu ndio unatutenga naye.

haya nipe connection kwanini unaamini ukisali atakusaidia katika utukufu huu?
Allaha katika Quran ametwambia ivi:

4:124. "Na anaye fanya mema, akiwa mwanamume au mwanamke, naye ni Muumini - basi hao wataingia Peponi wala hawatadhulumiwa hata kadiri ya tundu ya kokwa ya tende."
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…