Atheism: Imani nusu na robo

Atheism is the absence of belief in the existance of deities....Atheism is a rejection of belief that any deities exist.
Complicated phenomenon [emoji15] [emoji15] [emoji15]so it is a belief! Right?
 
Unapotamani kuishi huru na bila kuamini chochote hiyo utaita ni nini?Imani ni nini? Sio kusadiki?Na hao Atheists matamanio yao ya kuwa watu huru na wasioamini lolote sio usadikifu juu ya kuwa huru na usadikifu wa kutofungamana na chochote(kadri ya ufafanuzi wako)? Na je usadikifu huo unawezekana?
1.Je kuishi huru kupi wanakokusadiki? Je mumojawapo katika kundi hilo anaweza kwenda kuishi Bara la Antaktika bila uhitaji wa mtu mwingine?Je unaweza kuwa huru bila kumhitaji kiumbe mwingine yeyote?Je unapomuhitaji kiumbe mwingine yeyote yule ili uishi je bado uko huru?
2. Unaweza kutoamini katika chochote kile?Kama ndivyo je kule kutamani kuishi huru hiyo siyo imani?
Je,unapohitaji hewa ya oxygen ili uishi bado hiyo siyo imani?Je unapofahamu na kukubali kuwa dunia ni duara je hiyo siyo imani?
 
Can't you just see that this is a total contradiction?
Contradiction must involve two things opposing each other....Now according to your question, what is a base of contradiction? what are the two sides opposing each other?
 
Contradiction must involve two things opposing each other....Now according to your question, what is a base of contradiction? what are the two sides opposing each other?
Belief in the absence of belief/ imani pasipo imani
 
Not a belief but absence of belief?
What is belief?
etymology ▼ show
pronunciation
(IPA): /bɪˈliːf/
noun
(plural beliefs)

Mental acceptance of a claim as likely true.

Faith or trust in the reality of something; often based upon one's own reasoning, trust in a claim, desire of actuality, and/or evidence considered.

Kwa hiyo atheism ni dini.
 
Atheism ni ukosefu wa imani juu ya uwepo wa Mungu/Shetani(Deities)...Uhuru niliomaanisha ni ule wa kutokufungamana na kinachoitwa amri/sheria za Mungu/shetani....Ingawa sheria hizo zaweza kuwa ni maisha yetu ya kila siku, na kama ni kuzitekeleza ni kwa hiyari na siyo kwa shurti.Hakuna uwepo wa kiumbe kimoja peke yake, ndio maana hata kuza unahitaji viumbe wawili....Mtu kusema najihamini ni Imani lakini haisimamii kwenye Mungu wala Shetani....kuna imani mbali mbali, lakini imani isiyokubalika kwenye Atheism ni ya kuwepo kwa Mungu/Shetani.
 
I feel sorry for people who don't believe in God, The Almighty
 
Belief in the absence of belief/ imani pasipo imani
Atheism ni kutokuwepo kwa Imani na siyo kuamini kwenye kutokuwepo kwa imani...Kumbuka Imani isiyotambulika kwenye Atheism ni ile inayoenezwa na dini ya kumwamini/kumkataa Mungu/Shetani.
 
Atheism ni kutokuwepo kwa Imani na siyo kuamini kwenye kutokuwepo kwa imani...Kumbuka Imani isiyotambulika kwenye Atheism ni ile inayoenezwa na dini ya kumwamini/kumkataa Mungu/Shetani.
Okay kwa hiyo tunaweza sema ni imani ya kupinga uwepo wa Mungu?
 
Hapana Atheism siyo dini.Dini husimamia kwenye Imani juu ya Mungu, Miungu ama Shetani (Deities).Ili ujenge imani juu ya hizo Deities, lazima uwe na imani kwamba vipo.Lakini maana ya Atheism ni ukosefu wa imani juu ya uwepo wa hizo Deities.
 
Mkuu
Atheism si dini ila ina viashiria vya udini
Kwa sababu inajikita kwenye masuala yanayo husu Mungu, ni sawa na kukuta mtu amenyoa kipara halafu ukasema ni staili ya nywele
 
Umesoma maana ya imani? kwa mujibu wa hiyo dictionary au unabisha tu? Imani inahusu chochote unachoaminini mfano: Mungu ama jiwe ama chochote. unapoamini hakuna ni "imani juu ya hakuna" maana hutathibtisha. Rudia hiyo definition au tafuta dictionary yako ulete hapa.
 
Mkuu ma atheist wana akili sana kwa sababu
Madai yasiyo na ushahidi yanaweza kupingwa bila ushahidi vile vile.
Ukisema Mungu, yupo halafu ukaeleza masuala ya roho na akili bado huja prove kwamba Mungu yupo.
 
Mkuu
Atheism si dini ila ina viashiria vya udini
Kwa sababu inajikita kwenye masuala yanayo husu Mungu, ni sawa na kukuta mtu amenyoa kipara halafu ukasema ni staili ya nywele

Ngalau wewe unaelewa haraka. Nini maana ya dini? kuamini juu ya Mungu anayehusika na creation. Nini maana ya atheism ni imani juu ya nguvu fulani iliyosababisha existence of the universe ambayo sio Mungu. Huu ndio mzizi wake, kukana uumbaji. Nje ya hapo hakuna atheism. Kwa hiyo ni imani mbadala tu.
 
Mkuu nadhani michango ya wadau wengi humu imebainisha kuwa hiyo ndo imani yao.Mimi nafurahi tu kuwa tunajadiliana.Tunahoji hata yale ambayo wenzetu wamepata ku-assume kuwa yako vile au hivi.Ni jambo jema.Ndio chakula cha akili.Na ile "Nguvu kuu" kuliko nguvu zote inatujalia yote haya.
 
Okay kwa hiyo tunaweza sema ni imani ya kupinga uwepo wa Mungu?
Ili kuzuia mafuriko lazima mafuriko yawepo au yawe yamewahi kutokea...kama hujawahi kuona mafuriko wala hayajawahi kuwako huwezi kuyazuia.Kwa hiyo Atheism haipingi uwepo wa Mungu bali haitambui uwepo wa Mungu kutokana na kukosekana kwa ushahidi wenye nguvu.Kupinga kitu ni kule kukataa kukikubali hata kama kitakuwepo, lakini kwenye Atheism ukipeleka ushahidi wa kueleweka kwamba Mungu yupo, basi Imani juu ya uwepo wa Mungu itakubalika.Kukataliwa kwa imani juu ya uwepo wa Mungu kwenye Atheism ni kutokana na ukosefu wa ushahidi wenye nguvu juu ya uwepo wake na siyo kwamba ni kasumba ya kukataa tu.Kama Mungu atajitokeza leo na kujidhihirisha kwa watu, Atheism itafikia ukomo wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…