Atheism: Imani nusu na robo


Na hata wasomi wa fani zingine nao hivyo hivyo.

Wapo ninaowafahamu mimi ambao wanakubali kabisa kuwa hayo mambo ya mungu ni hekaya tu kama za Abunuasi.

Lakini pia wanakubali dini zina baadhi ya vitu ambavyo ni vizuri na kama mtu akijitahidi kwa kadri ya uwezo wake kufuata hayo yaliyo mazuri, mtu huyo ataishi maisha ya uadilifu.

Huwa natolea mfano zile amri 10 za mungu [kwa hisani ya mshua].

Usiue, usiibe, usizini, usiseme uongo....yote hayo ni mambo mema ambayo watu tunapaswa kuyafuata.

Ubaya wa kuyafuata hayo ni upi kwa mfano? Mimi siuoni!

Naona ni mambo mema kabisa.
 
Maombi kwa kitu ambacho huna uhakika kama kipo?
Ulishawahi kujibiwa maombi yako?

Halafu hizo nguvu za kimungu zinakujibu kupitia kitu gani? Usiniambi kuwa utajibiwa kwa kupitia mtu fulani.

Mfano tuchukulie kuwa unaumwa malaria ukae ufanye maombi tu uone kama utapona Mkuu. Ukipona bila kwenda hospital hakika hapo ndipo Unaeza sema ombi lako limejibiwa.

Mfano wa pili, una uhitaji wa elfu kumi Fanya maombi ya kuipata hiyo elfu kumi uone kama atakupa akikupa hapo ombi lako litakuwa limefanikiwa.

Ila mbali na hapo maombi hata uombe vipi kwa imani hakika utaambulia patupu.
 
Hvi ww huoni aibu kuendelea kuandika huu upumbav mwenzio anakwambi vtu vya maana ww unaandika ujinga na upumbav
 
Well said,

Dini huwa zina vitu vizuri Sana katika jamii mfano kutoa huduma mbalimbali za kijamii.

Pia hata misaada mbalimbali pale ambapo kuna uhitaji.

Hivyo vitu ndivyo vinapelekea natambua umhimu wa dini.

Ingawa siyo kwamba watu wanakumbatia dini kwa sababu Mungu hapana ni kwa sababu zina faida ndani yake.
 

Lakini pia hufanya watu wawe wajinga, wapumbavu, na wazembe kupindukia.

Mambo ya kumwachia mungu kila kitu ni ujuha.

Kuna watu huwa wanakataa hadi matibabu ya hospitalini kisa tu mwanamuamini mungu.

Kuna watu wamemtumia huyo huyo mungu kukandamiza wenzao [kwanza mungu gani hata anaruhusu mambo kama hayo kutokea?].
 

Yeah. I get your point.

Unaweza kukukuta hata kiongozi wa imani anaogopa kukataa baadhi ya concepts kwa kuhofia kutenganisha waumini na kuharibu wenye imani juu ya dini hizo.

Kuna wengine wanadhani inahitaji dini kujua morals na lazima kuwa na dini kujua mema na mabaya which is a wrong assumption.

Kuna wengine hawana uhakika juu ya Mungu lakini hujiaminisha kwa kuhofia kusema kuwa hawana uhakika kama yupo au hayupo au yupo kama dini walizo nazo zinafundisha hivyo.

Lakini dini zinatofautiana na jinsi zinavyoelezea kuhusu mwanadamu na ulimwengu hazipo sawa. Kuna imani nyingi. Before mtu yoyote kusema dini zote sio kweli au kusema hakuna mungu au kuna mungu fulani ndio kweli au kuwa na mtazamo wowote lazima ajitolee kujifunza na kuchunguza imani mbalimbali na kuchagua uelewa wake unaona kipi sahihi.
 
Ila wao wanasema sio imani
 
Amini Mungu yupo uenda umkose kuliko kuamini hayupo uende umkute, itakuwa ni kilio na kusaga meno!

Kama unaamini Mungu anaiona nafsi yako basi jua hataridhika ukimuamini kwa unafki na kumuogopa. I believe kama kuna mungu, basi hayupo hivyo.
 
Hakika Mkuu.

Kama yupo kweli basi ana roho mbaya sana na hana upendo na watu wake.

Mfano tetemeko lililotokea bukoba angezuia lisitokee kwa sababu anajua kila kitu.

Lakini kuwaokoa watu wake lakini amewaacha wameumia sana.
 
Tuseme Mungu anaishi kwa kuwatega wanadamu ili apate faida gani sasa?

Exactly.

If He is supreme why akutege? Au why akuumbe ili umuabudu? Utamuongezea nini? What else does he gets from you if he is supreme?

Na ndio maana siamini kuwa lengo la Maisha ni kumjua Mungu, Kumuabudu na kumtumikia. Because He does not deed that kwa sababu hata usipofanya hivyo, if He is supreme then He is supreme tu. Hata ukimuabudu wala usimuabudu au usipomjua au kumjua He does not need pride, praises, fears wala sifa kumpa qualification za kuwa supreme.

Know thy self kwanza ndipo majibu mengine yatakuja. Hata Yesu mwenyewe alisema look within.
 
Tatizo linakuja Mungu huyo huyo yuko incoherent, pengine kwenye vitabu vyake mtu ukitaka kufanya mabaya unaweza kutumia maandiko yake ukafanyia mabaya.

Ndiyo maana ni muhimu kujuzana, jamani eeh, huyo Mungu kusema yupo poa tu, lakini msiende kuchukua mstari kasema ueni kwa jina langu mkaenda kuua kwa sababu kitabu kitakatifu kimesema.

Hayupo, ni hadithi tu inabidi mchukulie mambo kwenye context.
 
Hata mimi huwa nawaza along the same lines...

Yes na kama yupo wote hatumjui.Ikitokea mtu anamsemea mungu na kumuelezea vizur basi ana matatizo kwa maana hao hao ndo huwa wanasema god is beyond our thinking capacity.
Huwezi kuwa na ALL PERFECT GOD HALAFU AKAUMBA IMPERFECT MAN HAIWEKANI
 
Nini kiliwakuta Mkuu mpaka mkaacha na upadr. Mm niliishi ktk ukristo zaid ya miaka ishirini km mu anglican mwisho nikaachana nao baada ya kuuanza kutafuta elimu zaid niligundua vtu ambavyo nilishindwa kujibiwa

hakika elimu ni kitu muhimu sana
Umenikumbusha mbali nami ilibaki miez kadhaa niwe p.d.r
 
Ubaya wake ni kwamba mungu huyohuyo na watu haohao wa kwanza kupewa hizo amri ndio walikuwa vinara wa kuua watu na viumbe visivyo na hatia.

Na kwa nini hayo mafundisho/amri zinapendwa kuambatanishwa na dini? Ina maana mtu kama mtu hana empathy mpaka aambiwe?
 
Je,ni yapi ya kukufanya ufuate hizo amri? Ikiwa unajua hakuna mungu unaachaje kuzini kwa mfano?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…