Atheism: Imani nusu na robo

Mkuu. Nimeona ni heri nikuulize huku kwenye mada husika.

Kwa mtazamo wako na Agnostic ni imani?
Sorry nilikuwa offline twende kule...nimefika kule sijaona kitu...naweza bila shaka kusema ndio ni imani
 
Sasa endelea kuedit mpaka hadithi zote zitoke na ibakie reality
I never expected this from you Jimena! Kwakuwa tu nimekataa kukubaliana na mitazamo yenu? [emoji22] [emoji22] [emoji22]
 
I never expected this from you Jimena! Kwakuwa tu nimekataa kukubaliana na mitazamo yenu? [emoji22] [emoji22] [emoji22]
Tatizo ni pale unapodhani kuwa atheist wote wana mitazamo ile unayoifikiria wewe. Ila nimefurahishwa kidogo na edit uliyofanya na nadhani utaendelea kuedit kidogo kidogo kadri unavyozidi kuelewa huhusu hii kitu uliyoiita imani nusu na robo
Eid Mubarak
 
Jimena kwanini unataka kuwa rigid? Hivi unajua kuwa hii ni mitazamo tuu?kwanini unataka kupractice extremism?
 
Sasa kwani kitu kikiwa ni mtazamo tu ndo hakihitajiki kuwa sahihi??
Jimena Tanzania daily tunakula nyama ya ng'ombe ni vigumu kabisa au ni kitu kisichowezekana kuwa ipite siku bila kuchinja ng'ombe na hakuna tatizo huku kwetu lakini imagine umchukue mhindu nyumbani kwako halafu umpe chakula chenye nyama ya ng'ombe uone reaction yake
My point is kwa mhindu ng'ombe ni Mungu kwa mswahili ni kitoweo huu ndio mtazamo ninaozungumzia
 
Okay. Endelea kunipatia somo mkuu.

so, how come Agnosticism ni imani?
Apollo pls don't tease me naomba twende kwa hoja na kupingana kwa weledi rejea tafsiri ya kamusi kuhusu agnosticism
 

Study ishafanyika ya near-death situations kwenye death bed,hayo unayosema si sahihi...

Atheist amefunga mlango wa Mungu na Amefunga mlango wa shetani...kwake kuna shetani au mungu ni kitu hakipo,hatambui...yaani kwake kuna void,vacuum,ni empty...sasa utasemaje anaamini negative maana kaikataa positive wakati kwake zote mbili haziexist

Na mnaoamini deit au god figure head sio kwamba ndio ukweli,inaweza kua uwongo pia...hamna assertion 100% mpo sahihi...na kitu chochote ambacho hakina 100% proof hakiwezi kua Godly...huo ndio ukweli.
 

Correction Mr Mshana na kwa wengine ambao hawafahamu.

Hinduism haiabudu ng'ombe wala hana nafasi katika deity wa hinduism. Ng'ombe anakuwa mnyama anayeheshimiwa kama sacred kwa sababu ya symbolism iliyobebeka tangu zamani katika India. Pia ilikuwa ni kama kipimo cha mali (mfano hata sisi tuna makabila ambayo yanaona ng'ombe ni dhamani na wana count utajiri kupitia idadi ya ng'ombe). Hivyo India zamani ng'ombe walikuwa hawauawi na wanaachwa katika matumizi ya maziwa, butter na mafuta. Pia ilikuwa sign of power.

Ng'ombe ana symbolism ya fertility. Anatoa maziwa kutunza mwanae, anatoa maziwa kwa mfugaji wake, ng'ombe ana upendo kwa mwanae na hata mwanae akifa atagoma kutoa maziwa. Ni sign of love kwa kutoa maziwa yake kutunza mtoto na kumpa mfugaji kwa pamoja bila hasira. Krisha ambaye ni mojawapo wa Deity wa kihindi alipokuwa mdogo alitunzwa kwa maziwa ya ng'ombe na hata alipokuwa mwalimu wa imani alipenda kutumia mfano wa upendo wa ng'ombe kukumbuka maisha yake alivyotunzwa kwa upendo wa ng'ombe aliyemuona kama mwanaye huku akitoa 'ombe maziwa kwake na kwa ndama wake. Krishna akaitwa protectors of cows. Akapinga kuua ng'mbe na ndipo heshima juu ya ng'ombe ilipoanza na mpaka leo.

Hivyo ng'ombe haabudiwi bali anaheshimiwa. Katika kuheshimu symbolism hiyo hawaui ng'ombe kwa symbolism iliyohadithiwa kupitia mfano wa ng'ombe.
 
Apollo pls don't tease me naomba twende kwa hoja na kupingana kwa weledi rejea tafsiri ya kamusi kuhusu agnosticism

Come on Sir, sina ubishi. Najifunza. Pia ninajua unajua maana yake.

Kwa tafsiri ya ujumla Agnostic unlike Atheists na Theists yeye hayupo upande wowote. Agnostic ni sawa na kusema "sijui kama mungu yupo wala sijui kama hayupo".

Ninapenda nijue kwa sababu mada yako imewalenga atheists, ndio maana nikaja na swali je ambaye haamini wala hapingi uwepo wa mungu wala miungu na kusema "I Don't Know", is it a belief?
 
It's a belief
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…