FATUMA SELEMANI 24
New Member
- Jul 13, 2021
- 2
- 0
Na Fatuma Seif
Sigara ni aina ya kilevi,kibirudisho ambacho hutumiwa na baadhi ya watu wa rika tofauti tofauti ikiwa na maana ya wanaume, wanawake, wazee na hata vijana ambao hupenda kutumia kiburudisho hicho.
Japo sigara hutumiwa na baadhi ya watu ambao hupenda kuitumia lakini ni ukweli usiopingika kuwa uvutaji wa sigara ni hatari kwa afya ya binadamu na ina madhara kwa wale wanaotumia na ikiwa mvutaji atavuta sigara yake Karibu na watu wasiotumia inaweza kuleta athari za kiafya kwa wale wasiotumia.
Si jambo la kushangaza kwa karne ya sasa kwa kuwakuta vijana wakiwa wanavuta sigara hadharani bila kujali kuwa wanahatarisha afya zao wenyewe.
Dr P. J. Lymo kutoka kliniki ya Papri iliyopo moshi alisema kuwa uvutaji wa sigara hauna faida yeyote kiafya katika mwili wa binadamu bali inazidisha matatizo ya afya kwa mtumiaji.
"Sigara haina vitamini yeyote katika mwili wa binadamu, haina protini wala wanga basi tu ni ile hali ya mtu kuwa na mazoea na kwa bahati mbaya mvutaji wa sigara akizoea kuitumia inakuwa ni vigumu kuiacha"Alisema Dr Lymo
Iwapo katika familia ikiwa baba au mama atakuwa ni mtumiaji wa sigara na akawa anavuta mbele ya watoto kuna uwezekano mkubwa wa watoto kurithi jambo hilo kwa kudhani kuwa ni sifa.
Ikiwa watoto watarithi suala hilo kutoka kwa wazazi wao basi kuna uwezekano mkubwa uvutaji wa sigara ukawa ni jambo la kurithi kizazi hadi kizazi katika familia hiyo.
Dr Lymo alisema kuwa Sigara ina hasara nyingi katika mwili wa binadamu Kama vile kuharibu mishipa damu ya ubongo ambayo husababisha mtumiaji kupata ugonjwa wa kiharusi (strock).
Aidha alisema kuwa mvutaji wa sigara anaweza kupata ugonjwa wa mapafu kutokana na kuvuta hewa safi na kushindwa kuitoa chafu na hivyo kupelekea kupata ugonjwa wa moyo.
"Sigara inaumiza mishipa ya damu ya ubongo, pia kutokana na kushindwa kutoa hewa chafu iliyopo mwilini hii hupelekea moyo kuelemewa na badae kupanuka na kuwa mkubwa "alisema Dr Lymo.
Hata hivyo uvutaji wa sigara huweza kusababisha mtumiaji kupata magonjwa mbalimbali Kama vile saratani ya mapafu,saratani ya mdomo, na ugonjwa wa moyo.
Dr Lymo alisema "pale anapoweka sigara yake mdomoni panaungua kila siku na mwisho wa siku inaleta saratani au kansa na vile vile kansa ya koo huletwa na sigara na watumiaji wengi wa sigara hupata vidonda vya tumbo na hata kupata saratani ya utumbo mpana"
Hata hivyo nilizungumza na baadhi ya watu waliowahi kuvuta sigara na wale wanaotumia kwa sasa na kila mmoja alikuwa na maoni yake juu ya uvutaji wa sigara.
Bi Mainda alisema kuwa katika kipindi cha nyuma alikuwa ni mvutaji mzuri wa sigara na hakuna faida yeyote aliyoipata katika uvutaji huo isipokuwa kwa sasa anaugua ugonjwa wa kifua uliosababishwa na matumizi ya sigara.
"Kiukweli nimeshatumia sigara zamani lakini sikuwahi kupata faida yoyote, nilikuwa natumia shilingi mia tatu (Tsh.300/=) hadi miatano (Tsh.500/=) kwa siku kwa ajili ya kununua sigara,wakati navuta nilikuwa nahisi kupata starehe fulani Ila kwa sasa nimeacha kutokana na kupata ugonjwa wa kufua ambao nipo nao kwa miaka mawili sasa"Alisema Bi Mainda.
Naye Daudi Minja alilimbia gazeti hili kuwa anatumia sigara kwa muda wa miaka mitano na amekuwa akitamani kuacha Ila anashindwa kutokana na kuizoea
"Natumia sigara kwa muda mrefu, ninapoivuta napata msisimko fulani katika akili na mwili Wangu japokuwa ni Hatari kwa afya lakini nashindwa kuiacha sababu nimeshazoea kiasi kwamba ninapoikosa napata tabu"Alisema Bw Daudi Minja.
Aidha Bw Daudi alisema kuwa japokuwa amekuwa akiambiwa kuwa Sigara ina madhara Ila kwa upande wake amekuwa akipatwa na ugonjwa wa kikohozi na wakati mwingine kuhisi maumivu ya Kichwa Ila anashindwa kuacha kutokana na kuwa ameshazoea kuitumia.
Hao ni baadhi ya watumiaji wa sigara waliozungumza na gazeti hili na kueleza namna walivyoathirika kutokana na Kutumia sigara.
Dhamira ya dhati katika kuacha matumizi ya sigara ni Mojawapo ya Ushauri wa Dr Lymo kwa wavutaji wa sigara ili kuepukana na Magonjwa mbalimbali.
"Kwakua sigara haina faida yoyote katika mwili wa binadamu inatakiwa wavutaji hao kuwa na dhamira ya dhati katika mioyo yao ili kuacha kabisa uvutaji huo "alisema Dr Lymo
Lakini pia Sigara inakondesha kwa kuwa mvutaji anashindwa kupata hewa ya oksijeni ya kutosha kutokana na ule moshi wa sigara anaouvuta.
"Kila anayetamani kuvuta sigara aachane kabisa na wazo hilo katika akili yake kwakua hakuna faida yoyote atakayoipata katika sigara isipokuwa atahatarisha afya yake kwasababu akijifunza kuacha itakuwa ni vigumu "alisema Dr Lymo
Hata hivyo Dr Lymo aliwashauriwa wazazi kuacha kuvuta sigara mbele ya watoto ili kuepusha watoto kuiga tabia hiyo kutoka kwa wazazi wao.
Aidha aliitaka Jamii kuacha tabia ya kuvuta sigara kwenye mkusanyoko wa watu ili kuepusha madhara kwa wale wasiotumia ambao kitaalamu huitwa (passive smoke).
Kimsingi jamii na katika familia ikiwa baba au mama anatumia sigara na kuacha hawezi ili kuepusha watoto kuiga tabia hiyo imeshauriwa avutie mbali na watoto wake kwani asipofanya hivyo inasababishwa watoto kuiga tabia hiyo kwa kuona ni jambo la kawaida.
Lakini pia kwa kuwa uvutaji wa sigara ni hatari kwa afya ni vyema watu wanaovuta wakaacha kabisa na Kama inakuwa ni vigumu ni vyema wakatembelea vituo vya afya kwa ajili ya kupata ushauri wa namna ya kuacha matumizi hayo.