Jamani, kuna impact yoyote akina dada mtu na mdogo wake kuolewa na kwenda kuishi sehemu moja? Hapa ninapoishi kuna mdada ameolewa tumepanga nyumba moja, mimi nakaa vyumba vyangu viwili na yeye viwili (vya uani). Nyumba inayofuata ameolewa mdogo wake, ila kama ujuavyo nyumba za uswahilini, kwa huyu dada na huyo mdogo wake ni kama vile wako nyumba moja jinsi zilivyo karibu (akitoka getini hatua nne tuu yuko kwa mdogo wake. Mbaya zaidi kwa wazazi wao ni mwendo wa dakika kumi kutembea kwa mguu.
Kilichonifanya niulize swali hili ni kuwa hawa wanawake kila mmojawao hakuna anayeelewana na mumewe, yaani ugomvi kila mara, utakuta leo mkubwa ana bifu na mumewe, kesho yake mdogo wake ana ugomvi na mumewe. Kuna siku dada mkubwa alikuwa anapigana na mumewe, basi mdogo mtu kaja kumsaidia dada yake. Sasa mi nashindwa kuwaelewa yaani mwaka mzima sijaona wakiwa na amani.
Ninachojiuliza hizi bifu ni kwa sababu wako karibu? au wanashauriana vibaya? Au ni malezi mabaya waliyopewa toka kwao (family background?). Tumechoka kusuluhisha jamani na sasa nimeamua nikirudi zangu toka kazini hata nikiambiwa wamegombana wala sishituki maana ni kama kutwanga maji kwenye kinu.