Athari za Kutohimiza Kiingereza

Tatizo hujui kiingereza ndio maana unakichukia!!! Na sio wewe tu mpo wengi!!! Mtia mada ametaja athari za kutijua kiingereza vizuri wewe unaleta mambo ya kukinganisha !!! Hivi milsomea wapi!?
Wewe unajua kingereza? Niwekee andiko ulilowahi andika tangu umalize ngazi ya elimu ulioishia ili nithibishe kujua kwako.
Kama unashangaa mimi kulinganisha basi wewe ulisoma chini ya mwembe.
Hadi wana sheria hulingnisha kesi sembuse jf , huwezi kufanya jambo lolote hapa duniani bila kulinganisha, Ulitaka mimi nishabikie kama wewe ?
Sikufundishwa kushabika bali kuhoji na kujenga hoja.Kama huna hoja kaa pembeni au endelea kumshabikia mtoa mada.
 
Ujerumani na Japan ni nchi zenye teknolojia kubwa duniani na hawatumii kiingereza katika mitaala Yao yote na hata Kama lugha ya Taifa , Taifa imara ni lile linalosimamia misingi yake kuanzia kuwa na lugha yake wenyewe ukisema tuhamasishwe kutumia kiingereza ina maana unaturudisha katika utumwa wa kifikra na kuendelea kujiona dhaifu Kwa kudharau vitu vyetu
Mkuu upo sahihi kabisa. Ila ujue kuwa hizo nchi zimeshaendelea kwa technology lakini sisi tunahitaji misaada ndio maana tunahimizana kujiendeleza kwa lugha za wanaotusaidia.

Tofauti na hapo tukisema the tuendelee kwa kukaza shingo na hiki kiswahili chetu tutabaki hivi hivi mpaka mwisho wa dahari.
 
Ni kweli kabisa.

Kutokujua kiingereza kumeturudisha nyuma kwa kiasi kikubwa Watanzania.Bora elimu ianze kutolewa kwa kiingereza kuanzia chekechea.

Hakuna mtanzania anayependa kupeleka watoto wake shule wanazofundisha Kiswahili, ni umaskini tu ndio unasababisha.

Ajira nyingi kiingereza ndio kipaumbele. Sasa kwa nini tunawafundisha watoto lugha isiyo na future yoyote. Tena hao wanaosema tunaeneza Kiswahili, watoto wao wanasoma shule zinazotumia Kiingereza.

Jamani tuacheni tu unafiki tutoe elimu kwa kiingereza.
 
Wewe unajua kingereza? Niwekee andiko ulilowahi andika tangu umalize ngazi ya elimu ulioishia ili nithibishe kujua kwako.
Kama unashangaa mimi kulinganisha basi wewe ulisoma chini ya mwembe.
Hadi wana sheria hulingnisha kesi sembuse jf , huwezi kufanya jambo lolote hapa duniani bila kulinganisha, Ulitaka mimi nishabikie kama wewe ?
Sikufundishwa kushabika bali kuhoji na kujenga hoja.Kama huna hoja kaa pembeni au endelea kumshabikia mtoa mada.
Unaogopa kidhungu
 
Kuongea kiingereza sio utumwa!?? Mluokimbia umande acheni ujinga!? Nyerere aliijua vizuri hii lugha alijua mtumwa!?? Tatizo watanz wapumbavu ni wengi hasa huko chamani
Can you show me please where I said to speak english is slavery?
 
We jamaa serikali ya Tanzania haipeleki wvijsna kwenda kusoma huko ulaya na America?
Wachina na sisi nani syllbus yao imebebwa na kingereza zaidi?
Mnatafuta mchawi kila uchwao, tatizo la maendeleo ya Africa si lugha bali ni zaidi ya lugha.
Naona hukunielewa kuhusu mfano wa China. Nimejaribu kuonyesha kwa wale wanaotaka tuamini kuwa china imeendelea kwa kutumia mandarin tu. Kitu ambacho si kweli.
Hakuna niliposema kuwa tatizo letu ni lugha tu. Lakini lugha ni kitu muhimu kwa mawasiliano ya ndani na nje. Na kwa Tanzania vyote kingereza na kiswahili ni muhimu.
 
Kuna watu watasema kiingireza ni lugha tu kama lugha nyingine kama kichina. Ila kiukweli ngeli ni muhimu mno. Kwa dunia ya sasa. Ila kama maisha yako unataka kuishia tandika basi endelea na kuona kiswahili ni muhimu. Ni aibu kuona hata wachezaji wetu wa timu ligi kuu wanapoenda kwenye mashindano huko katika mahojiano wanajikanyaga hii ni aibu kwa taifa zima. Lazima tunde sawa na duni a ndugu zangu.
 
Back
Top Bottom