Augustine Moshi
JF-Expert Member
- Apr 22, 2006
- 2,554
- 1,382
Madhara ya Kutokipa Kiingereza Umuhimu
Siku hizi nchi yetu ina tatizo la wananchi wengi kutoweza kuandika na kuzungumza kwa lugha ya Kiingereza. Kiuchumi, TAZIZO HILI SIYO HIMILIVU.
Adhari zake ni pamoja na zifuatazo:
1. Kukosa ajira za kimataifa. Nchi kama Uingereza inakuwa na upungufu wa manesi mara kwa mara. Wanaajiri toka Malawi, Kenya na nchi nyingine ambazo raia wake wanamudu lugha ya Kiingereza.
Mashirika kama Emirates huwa yanahitaji waajiriwa wachache wanaoweza kuongea Kiswahili na Kiingereza. Huwa wanaajiri Wakenya kwani wana hiyo sifa.
2. Kukosa ajira nchini. Nyumbani kwenyewe mashirika binafsi wanapenda zaidi wahitimu waliosoma nje kwani wao humudu lugha zote mbili.
3. Kukosa fursa za kusikika ulimwenguni. Mashirika ya habari kama Aljazeera na BBC World service wanapotaka kuongea na mtu wa Afrika Mashariki, kwa Kiingereza, huwa hawachagui Mtanzania. Wataongea na mwalimu wa chuo kikuu Mkenya au Mganda. Hii inafifisha umaarufu wa vyuo vyetu. Vinashuka kwenye viwango rasmi vya ubora duniani.
Ukiweka YouTube kitu kwa Kiswahili maana yake unakilenga kwa watu milioni 200. Ukiweka kwa Kiingereza basi umekielekeza kwa watu zaidi ya mara tano ya hao.
4. Kudumaza elimu. Reading materials mtandaoni sehemu kubwa ni za Kiingereza. Mtu asiyeelewa vizuri Kiingereza tayari anajinyima asilimia kubwa ya maarifa yaliyopo duniani.
5. Kudumaza utalii. Kutosikika kimataifa kunatunyima watalii wengi. Pia wachache wanaokuja wanajikuta hata watu wa uhamiaji na polisi hawawezi kuzungumza nao kwa Kiingereza.
Miaka ya sitini tulikuwa vizuri tu kwenye Kiingereza. Mhitimu wa shule ya sekondari alikuwa anabidika kufaulu Oral and written English.
Napendekeza kwamba:
1. Interview za ajira serikalini zizingatie uwezo wa kusema na kuandika Kiswahili na Kiingereza. Kumudu Kiingereza iwe a condition for employment of ALL civil servants.
2. Kuwe na sera ya wanafunzi shule za sekondari kuongea tu Kiingereza wawapo shuleni. Hii haitadhoofisha Kiswahili kwani watakiongea sana nyumbani na mitaani.
3. Kufaulu kidato cha nne iwe ni pamoja na kufaulu Oral English. Mitihani yake itasimamiwa na shule kama ilivyokuwa miaka ya sitini.