damian marijani
JF-Expert Member
- Jan 31, 2010
- 695
- 466
Wakuu, naomba leo nitoe hii hoja ambayo inaniumiza kichwa. Wataalam waliobobea kwenye nyanja za watoto wanatuasa kuwa internet na luninga inapotumiwa sana na watoto inawafanya wasiweze kupevuka kiakili,kwani vitu hivi havileti changamoto yoyote ile kwa akili changa ya mtoto kuweza kumjenga aweze kutafakari na kuweza kutatua matatizo ambayo anaweza kukutana nayo katika maisha yake. Kwa maana nyingine ubongo wa huyu mtoto ambaye huwa anatumia muda mrefu kwenye tv au internet unabweteka kwani kila mara anapata jibu kwenye mtandao au tv.
Ninajua hili tatizo halipo katika majority ya Watanzania kwa sababu ya accessibility issues, lakini kwa wale wachache waliojaliwa kuaccess hizi huduma tuwe macho!!
Ninajua hili tatizo halipo katika majority ya Watanzania kwa sababu ya accessibility issues, lakini kwa wale wachache waliojaliwa kuaccess hizi huduma tuwe macho!!