Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Allie Dowdle anasema wazazi wake walikataa kumpatia fedha kwa sababu hawakupenda uhusiano wake na kijana huyo mweusi.
Akiandika katika ukurasa wake wa GoFundMe ,Allie alisema: Nikiwa na umri wa miaka 18 wazazi wangu wamekataa kunifadhili katika maisha yangu ya baadaye ,na kunipokonya raslimali zangu zote.
Babake msichana huyo hatahivyo amekana kwamba sababu ya kukata uhusiano huo ni ile ya ubaguzi wa rangi.
Allie anasema kuwa yeye na Michael Swift wamekuwa katika husiano wa kimapenzi kwa takriban mwaka mmoja baada ya kuwaelezea wazazi wake lakini swala hilo likazuka tena baada ya Michael kukutana na wazazi wake msichana huyo.
Anadai kwamba baada ya mkutano huo wazazi wake walimtenga na sasa hawezi kupata fedha alizohifadhiwa ,gari, simu na hawezi kulipia masomo yake.
''Babangu hakunipa sababu nyengine, aliniambia kwamba siruhusiwi kumuona Michael tena'' ,alisema. Kwa nini? kwa sababu ya rangi ya ngozi yake.
''Sitasahau vile wazazi wangu walivyonikaripia walipoelezea vile walivyokasirishwa nami kwamba ningeweza kutafuta mtu mwengine mzuri zaidi''.
Chanzo: BBC