sungusungu
JF-Expert Member
- Dec 21, 2012
- 3,057
- 723
Kwa jina anaitwa Mangi, anamiliki jiko kwenye bar ya hapa kitaani kwetu. Usiku wa kuamkia jana alikumbwa na janga la kufungia mwaka 2014.
Ilikuwa hivi, jamaa alifunga ofisi (Jiko) lake mida ya saa tano usiku na kuelekea kwake maeneo ya Manzese Friends Corner. Saa kumi kasoro usiku jamaa alidamka kwa ajili ya kwenda kuchukua malighafi za jikoni maeneo ya Vingunguti Kiembe Mbuzi. Mfukoni alikuwa na sh. laki tano na elfu themanini za mauzo ya siku tatu. pamoja na simu yenye shilingi laki nane na elfu themanini tigopesa ambayo ni mauzo ya wiki moja na ushee.
So baada ya kudamka, jamaa akakaa kituoni pale Friends Corner akisubiri Bajaj impeleke Vingunguti. Baada ya kama dakika kumi hivi za kusubiri ikatokea bajaj. Ndani ya bajaj kulikuwa na abiria wawili pamoja na dereva jumla kulikuwa na watu watatu. ( Little to his knowledge, kumbe abiria pamoja na dereva wote walikuwa vibaka)
Mangi akaingia ndani ya bajaj na bajaj ikaanza kuondoka, baada ya kufika maeneo ya Magomeni mwembechai, mmoja kati ya wale abiria alimpia Mangi banzi kali sana la usoni, akiwa katika hali ya kutahamaki akapigwa banzi jingine la kichwani, then jamaa wakamtoa nje na kuanza kumsachi.
Wakiwa wanamsachi, yule dereva akapaza sauti yake akisema "Nyie vipo mnafanya use**** gani hapo? Mbona mnamchelewesha huyo Mse****?)
Basi unaambiwa, tangu dereva atoe tamko hilo, hazikupita dakika tatu, mangi akawa ameporwa kila kitu kuanzia hela, simu pamoja na nguo zote hadi nguo za ndani pamoja na kujeruhiwa kwa panga kwenye eneo la dole gumba.
Baada ya kufanya uporaji huo, jamaa walitokomea na bajaj yao kwa kasi ya ajabu sana wakimuacha Mangi asijue la kufanya.
Mangi hakuwa na jinsi zaidi ya kurejea nyumbani kwake, akiwa kaficha nyeti zake. Anasema njiani alikuwa anakutana na watu ila walikuwa hata hawadili nae kwa sababu walikuwa wanahisi labda ni kichaa.
So jamaa akawa ametembea uchi kutoka Mwembe Chai hadi Friends Corner.
Kimbembe kilikuwa aliporudi nyumbani kwa sababu, funguo za chumbani kwake zilikuwa kwenye nguo zilizoporwa na vibaka.
Anashukuru Mungu alipofika nyumbani alikuta majirani bado hawajaamka na bahati nzuri mlango wa chumbani kwake ni sio imara sana so aliweza kuuvunja ndani ya muda mfupi sana.
Tukio hili limetuathiri sana wanywaji wa vileo kitaani kwetu, kwani limemfanya Mangi ashindwe kuja kazini kwa sababu anashughulikia usajili wa line yake pamoja na kublock line yake ya Tigopesa yenye hela.
Yeye hajaenda uchagani kufanyiwa tambiko kama mke wangu aliyeenda?