Atembea tena baada ya miaka kumi kupita

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Apr 28, 2020
445
754
Zaidi ya miaka kumi imepita toka apate ajali ya baiskeli ilikatisha matumaini ya Kutembea toka kwa Jamaa anaitwa Gert Jan oskam baada ya kupata ajali na kupooza kutokana na majeraha toka kwenye Uti wa mgongo.

Ila sasa anaweza kutembea na kusimama tena baada ya Wana sayansi toka uswizi kubuni kifaa cha Bsi( brain spine interface). Ili kutembea lazima ubongo wako utume Amri kwenye spinal cord (Uti wa mgongo) kuweza kudhibiti mlolongo mzima.

Lakini ikitokea Kuna Tatizo kwenye Uti wa Mgongo kunaweza sababisha Usitembee Kabisa. Professor Grégoire Courtine walisema walikuja na wazo la kutengeneza kifaa ambacho kitasaidia kurejesha mawasiliano kwenye mwili wake ila kwa kutumia mfumo wa daraja la kidigitali.

Team yao ikaamua kutengeneza mfumo wa wireless interface kati ya Ubongo pamoja na Uti wake wa mgongo kwa kutumia ubongo wa kompyuta Brain computer interface (Bci) teknolojia ambayo itaweza kubadilisha mawazo kuwa kitendo.

Hatimaye Mr Oksam anaweza kusimama , kutembea pamoja na kupanda ngazi kikawaida kwa kufikiria tu. Kuna vipandikizi viwili vya kieletroniki kwenye ubongo vimewekwa ili kutambua shughuli zote za Neva za Oksam anapotaka kusogeza mguu, kutembea nk.

Vyote hii ufanyika kwa kuvaa kitu nyuma ya mgongo wake ukivaa kama mkoba ili kiweze kufanya kazi mara moja kuweza kudhibiti mwendo kwenye miguu yake uweza kuhamsha misuli kusonga na safari.

Oksam aliweza kufanya upasuaji mara mbili pamoja na vikao 40 toka jopo la Wana sayansi mbalimbali ili kurejesha Hali ya miguu yake kuwa sawa kuweza kufanya mawasiliano Kati ya Uti wa mgongo , Ubongo kuweza kutembea kukaa nk.

Cha kufurahisha Zaidi kuwa Oksam anaweza kutembea mwenyewe kwa msaada wa magongo ila umbali mfupi bila kifaa Ikiwa atatumia magongo. Watafiti wanasema kifaa icho akijaboresha tu hisia zake pia ilimsaidia kukuza muunganiko mpya wa Neva kwenye mwili wake.

Unaionaje hii teknolojia ikija na kwetu tuachie maoni yako? View attachment 2641684View attachment 2641685

images%20(91)%20-%202023-05-31T021313.513.jpg
View attachment 2641688View attachment 2641687View attachment 2641686
 
Back
Top Bottom