ATCL yakiri kutikiswa na COVID-19

ATCL yakiri kutikiswa na COVID-19

Bagamoyo

Platinum Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
30,065
Reaction score
34,218
17 Julai 2020
Dar es Salaam, Tanzania

Mkurugenzi wa ATCL amesema janga la covid-19 limeathiri safari za ndani kwa asilimia 75 upande wa mapato.

Pia kwa safari za nje ni mapato yameathirika kwa asilimia 100. Mfano anga la nchi ya India bado limefungwa na kwa upande wa China anga lipo wazi lakini kuna masharti magumu kwa abiria watokao Tanzania kiasi ya kushindwa kusafiri.

Yote hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Shirika la Ndege nchini ATCL Mhandisi Ladislaus Matindi wakati wa mahojiano maalum na Esterbella Malisa wa kituo cha televisheni cha Azam TV cha mjini Dar es Salaam wakati akitaka kufahamu zaidi juu ya mikakati ATCL kufuatia mkwamo huo......

Source : Azam TV
 
Dikteta ASINGEKURUPUKA, kama wengi tulivyoonya kwamba ndege si kipaumbele cha Watanzania, kwenda kununua ndege kwa trillion 2 cash ambazo sasa zinapigwa vumbi airports. Hizi hasara za mabilioni zisingekuwepo.

Sasa ni lini wanapunguza wafanyakazi wao na mishahara yao pia?
 
Kweli kabisa mfano hizo trilioni 2 zingekwenda ktk kilimo kuwagusa 75% ya waTanzania na kuiachia sekta binafsi kuendesha biashara ya usafiri wa anga hasara kwa serikali ingekuwa upande wa kodi tu ambayo kiwango chake kisingefika matrilioni ya shilingi hata kama covid-19 ingeendelea kufunga usafiri wa anga kwa miaka 5 ijayo.
 
Bado mrejesho wa SGR kipande cha Dsm - Morogoro sijui kitaleta pato gani wakati tayari trilioni kadhaa zimetumika ktk ujenzi wa kipande kifupi kinachotarajiwa kukamilika.

Mimi ningekabili ujenzi wa reli siyo kwa kutafuta sifa kushindana na Kenya au Ethiopia.

Ningewauliza ma engineer wa Tanzania Railways Corporation ni maeneo gani ya reli ya kati ya mkoloni ni korofi na yanahitaji kuyarekebisha.

Mfano mahandaki ya Kilosa ni sawa kabisa ningetoa pesa ili kukwepa mafuriko ya mto Mkondoa treni zifanye kazi bila kusitisha safari inyeshe mvua masika au mafuriko makubwa.

Ningeachana na mbwembwe za stesheni za kisasa kila kituo, sana sana ningejenga platforms tu za abiria kupanda na kuwezesha mizigo kupakiwa kwa uharaka.

Kwa approach hiyo reli ya kati ingeboreshwa na kukamilika yote ndani ya miaka 10 na fedha za bajeti ya SGR reli mpya chenji nyingi ingebaki na kutengeneza network ya reli zingine za Meter Gauge.

Hizi mbwembwe za SGR reli mpya zimeiingiza nchi katika gharama kubwa na reli hiyo kutokamilika yote ktk miaka 20 ijayo.
 
Dikteta ASINGEKURUPUKA, kama wengi tulivyoonya kwamba ndege si kipaumbele cha Watanzania, kwenda kununua ndege kwa trillion 2 cash ambazo sasa zinapigwa vumbi airports. Hizi hasara za mabilioni zisingekuwepo.

Sasa ni lini wanapunguza wafanyakazi wao na mishahara yao pia?
Mzee wa kukurupuka ameangukia pua tena!! Miaka 5 ni hasara tupu!!

SGR haijaisha na haijalipa!!

Stigla hasara

Ndege hasara!!

Huyu jamaa ana roho ya uharibifu!!
 
Bado mrejesho wa SGR kipande cha Dsm - Morogoro sijui kitaleta pato gani wakati tayari trilioni kadhaa zimetumika ktk ujenzi wa kipande kifupi kinachotarajiwa kukamilika.

Mimi ningekabili ujenzi wa reli siyo kwa kutafuta sifa kushindana na Kenya au Ethiopia.

Ningewauliza ma engineer wa Tanzania Railways Corporation ni maeneo gani ya reli ya kati ya mkoloni ni korofi na yanahitaji kuyarekebisha.

Mfano mahandaki ya Kilosa ni sawa kabisa ningetoa pesa ili kukwepa mafuriko ya mto Mkondoa treni zifanye kazi bila kusitisha safari inyeshe mvua masika au mafuriko makubwa.
Tumetumbukiza matrilioni ya shilingi kwenye white elephant projects ambazo return yake itatuchukua miaka kukamilika
 
Hii SGR reli yasitishe ujenzi na ibadilishwe kuwa Meter Gauge kuokoa usafiri na fedha kibao. Hatujachelewa ni kipande cha Dar Ruvu tukibadilishe kiwe Meter Gauge na waendelee kukarabati reli ya kati mkoloni mpaka Kigoma / Mwanza.

Ikiwa wameweza kukarabati Dar Tanga Moshi Arusha reli ya mkoloni ya kaskazini kwanini wasifanye hivyo na kumaliza kero ya usafiri wa reli ya kati kwa kufanya marekebisho sehemu korofi na kumaliza mradi wote Dar Moro Dodoma Itigi Tabora Kigoma Mwanza kuwa meter gauge yenye maboresho ndani ya miaka 4 ijayo na kuachana na ndoto za SGR Reli mpya.

Hakuna cha aibu nchini Australia na Canada kuna treni zinapiga kazi kubwa tu kwa kutumia miundo mbinu iliyoboreshwa katika Meter Gauge, serikali yetu ya Tanzania ijisahihishe tuende vizuri katika suala hili la reli ya kati mkoloni.
 
Hivi huko nyumbani nasikia na reli ya moro Dom inakamilika sambamba na Dar Moro ni kweli? Huku ndo tunavyoambiwa
 
17 Julai 2020
Dar es Salaam, Tanzania

Mkurugenzi wa ATCL amesema janga la covid-19 limeathiri safari za ndani kwa asilimia 75 upande wa mapato.

Pia kwa safari za nje ni mapato yameathirika kwa asilimia 100. Mfano anga la nchi ya India bado limefungwa na kwa upande wa China anga lipo wazi lakini kuna masharti magumu kwa abiria watokao Tanzania kiasi ya kushindwa kusafiri.

Yote hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Shirika la Ndege nchini ATCL Mhandisi Ladislaus Matindi wakati wa mahojiano maalum na Esterbella Malisa wa kituo cha televisheni cha Azam TV cha mjini Dar es Salaam wakati akitaka kufahamu zaidi juu ya mikakati ATCL kufuatia mkwamo huo......

Source : Azam TV

Ningeshangaa kama wangesema hawajaathirika!
 
Dikteta ASINGEKURUPUKA, kama wengi tulivyoonya kwamba ndege si kipaumbele cha Watanzania, kwenda kununua ndege kwa trillion 2 cash ambazo sasa zinapigwa vumbi airports. Hizi hasara za mabilioni zisingekuwepo.

Sasa ni lini wanapunguza wafanyakazi wao na mishahara yao pia?
Ni nchi gani kwa kipindi hiki cha corona ndege zake hazipigwi na vumbi!
 
Kwa akili hizi Watanzanja mtaendelea kuishi miaka 50 nyuma... maendeleo ya vitu siku zote yanapelekea maendeleo ya watu. hizo projects mnazozipinga hapa wenzetu wanazo toka miaka ya 60 na ni moja ya projects ambazo impact yake inaonekana sasahivi. mfano sgr ikikamilika hata bei za nyumba dar es salaam zitapungua sababu mtu anaweza ishi morogoro akafanya kazi zake Dar. Kuhusu ndege kama watu wanaona maono ya rais watajua kwanini anataka awekeze huko ndoto yake ni kwamba kwa east Africa Tanzania iwe hub. kwa kifupi tu strategical Tanzania ipo position nzuri sana kwa Africa kiasi kwamba tungekua hub nzuri sana kwa ndege zinazoenda maeneo mbali mbali africa na nje. Watanzania acheni ishi miaka 50 nyuma tembeeni nchi nyingine ili mshituke kiakili
 
Dikteta ASINGEKURUPUKA, kama wengi tulivyoonya kwamba ndege si kipaumbele cha Watanzania, kwenda kununua ndege kwa trillion 2 cash ambazo sasa zinapigwa vumbi airports. Hizi hasara za mabilioni zisingekuwepo.

Sasa ni lini wanapunguza wafanyakazi wao na mishahara yao pia?
Duuuuu ndugu kwani hujui kuwa kila kitu kimepata madhara kwa ajiri ya Corona hata baa na mashule zimehathirika pakubwa hivyo, kwa mtazamo wako watu walifanya makosa kuwekeza ktk shule na mabaa
 
Hata bila covid hakuna profit kwenye usafiri wa anga katika Nchi nyingi duniani. Tuliposema kwamba ndege si kipaumbele cha Watanzania COVID19 haikuwepo.

Mbona unahama ktk mada yako mwenyewe?
 
Back
Top Bottom