ATCL yakiri kutikiswa na COVID-19

ATCL yakiri kutikiswa na COVID-19

Swala ni je, zilikua na umuhimu kwa wakati huu?
Ndio zilikuwa na umuhimu rejea kauli ya Ndugu Zito Bungeni kuwa ni ajabu Tanzania tunazidiwa na kanchi kadogo Rwanda kana ndege zake
Pia ndugu zetu walikwama ktk baadhi ya nchi kwa Corona yuliwachukua uko kwa ndege zetu
 
17 Julai 2020
Dar es Salaam, Tanzania

Mkurugenzi wa ATCL amesema janga la covid-19 limeathiri safari za ndani kwa asilimia 75 upande wa mapato.

Pia kwa safari za nje ni mapato yameathirika kwa asilimia 100. Mfano anga la nchi ya India bado limefungwa na kwa upande wa China anga lipo wazi lakini kuna masharti magumu kwa abiria watokao Tanzania kiasi ya kushindwa kusafiri.

Yote hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Shirika la Ndege nchini ATCL Mhandisi Ladislaus Matindi wakati wa mahojiano maalum na Esterbella Malisa wa kituo cha televisheni cha Azam TV cha mjini Dar es Salaam wakati akitaka kufahamu zaidi juu ya mikakati ATCL kufuatia mkwamo huo......

Source : Azam TV

Hata China ambaye ilisemekana ni rafiki yetu ana masharti magumu ya kuingia kwake hadi kufikia kuistisha safari huko?

Anayebakia kuwa si beberu ni nani?
 
Inaeleweka kuwa biashara nyingi na katika mataifa mengi zimepata kiminyo cha covid.
 
17 Julai 2020
Dar es Salaam, Tanzania

Mkurugenzi wa ATCL amesema janga la covid-19 limeathiri safari za ndani kwa asilimia 75 upande wa mapato.

Pia kwa safari za nje ni mapato yameathirika kwa asilimia 100. Mfano anga la nchi ya India bado limefungwa na kwa upande wa China anga lipo wazi lakini kuna masharti magumu kwa abiria watokao Tanzania kiasi ya kushindwa kusafiri.

Yote hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Shirika la Ndege nchini ATCL Mhandisi Ladislaus Matindi wakati wa mahojiano maalum na Esterbella Malisa wa kituo cha televisheni cha Azam TV cha mjini Dar es Salaam wakati akitaka kufahamu zaidi juu ya mikakati ATCL kufuatia mkwamo huo......

Source : Azam TV

Covid-19 ni kisingizio kilichokuja wakati muafaka kuficha tatizo lenyewe lakini ukweli unabaki palepale hali ingekuwa hiyohiyo hata bila hilo gonjwa. Wachambuzi wamelizungumzia sana Shirika hilo namna lilivyoanzishwa upya bila kufuata taratibu za kibiashara za kupata faida. Kosa lililofanyika linafahamika lakini hakuna jitihada zinafanywa kurekabisha kosa hilo badala yake ni ndege zaidi zinanunuliwa huku zilizopo zimepark kiwanjani mwisho hata nafasi ya kupark ndege za Mashirika mengine yanayoleta watalii kukosekana. ATC haikufa kwa sababu ya ukosefu wa ndege bali kutokana na matumizi mabaya ya ndege na rasilimali nyingine zilizokuwapo, sababu hizohizo ndo zimerudiwa kwa ATCL. Mashirika ya kimataifa yameanza kuja Tanzania baada ya gonjwa hapa kwetu na kwingineko kupungua, Shirika letu kwanini nalo lisitumie fursa hiyo? Ndege ikiwa angani inatengeneza pesa, ikiwa ardhini inakula pesa, huo ni usemi wa kweli wa wataalamu wa usafiri wa anga.
 
Hivi huko nyumbani nasikia na reli ya moro Dom inakamilika sambamba na Dar Moro ni kweli? Huku ndo tunavyoambiwa

Bado ila sasa wamejikita ktk propaganda za kutembelea nyota za watu mashuhuri na wazito kutembelea saiti za ujenzi wa reli. Mambo ni magumu hakuna namna wabadilishe gia wafuate mawazo mbadala waachane na ndoto ya full SGR reli.

16 Julai 2020
Updates za mradi wa SGR RELI

Source : TRC RELI TV
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hayo ma-white elephant yataigharimu hii nchi pakubwa, ajira kwa vijana ni kama hazipo, maslahi ya watumishi yamepigwa kabari, sekta binafasi inapumulia mashine. Na hizi changamoto zilianza nyuma kabisa kabla ya Covid-19, kwa hiyo tusijaribu kutafuta kichaka cha kujificha..
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Bado ila sasa wamejikita ktk propaganda za kutembelea nyota za watu mashuhuri na wazito kutembelea saiti za ujenzi wa reli. Mambo ni magumu hakuna namna wabadilishe gia wafuate mawazo mbadala waachane na ndoto ya full SGR reli.

16 Julai 2020
Updates za mradi wa SGR RELI

Source : TRC RELI TV
Wanawatumia watu empty headed kama kina diamond ndo wanaamini wataeleweka?

Magufuli kaitumbukiza hii nchi kwenye hasara isiyo elezeka
 
Back
Top Bottom