Naomba nifafanue kidogo. Ndege iliyopata ajali Mwanza ni ndege ya kukodi (leased aircraft).Sio mali ya ATCL. La hasha. Ndege hiyo ina bima(insurance ) ya kiwango fulani. Ajali ilipotokea mwenye ndege na watu wa bima wamekwenda Mwanza na kuona jinsi ndege ilivyoharibika. Baada ya assesment inaonekana gharama ya kuitengeneza hiyo ndege inakuwa kubwa sana kuliko gharama ya bima (insured value) ya ndege. Gharama inakuwa kubwa kwa sababu imeharibikia Mwanza ambako hakuna vifaa na karakana (kama DAR) hivyo mobilazation ya vifaa inakuwa ya juu sana.
Baada ya kutafakari mwenye ndege na watu wa bima (sio ATCL) wamekubaliana mwenye ndege alipwe bima yake na hivyo ndege itabaki mikononi mwa kampuni ya Bima (Insurance company) ambayo itajua jinsi ya kufanya lakini sana sana ile ndege itauzwa kama scrap kwa ajili ya spea kwa kutangaza tender. This has nothing to do with ATCL. Ni jambo la kwaida sana kwenye mambo ya ndege. ATCL inaweza kukodi ndege nyingine au kununua. Hii ndio maana ya Bima.