Infopaedia
JF-Expert Member
- Oct 28, 2011
- 1,231
- 1,495
Haya mambo ya online booking kama hamuyawezi ni bora muachane nayo tu. Na mnashindwa vipi kitu kidogo kama hicho!!!. Sasa mtaweza kuendesha shirika la ndege kweli kama kusimamia 'blog' yenu inakuwa kazi!!!. Kwanza web yenyewe ni kama mwanafunzi wa 'lasaba B' ndo mmempa ajifunzie kutengeneza website. Anyway, japo dalili ya mvua ni mawingu...hiyo dalili tunaivumilia. Basi hiyo website yenyewe iwe inafanya kazi kama inavyotakiwa. Ndiyo, matatizo yapo, lakini si kuna nafasi ya kutoa taarifa hapohapo kwenye hiyo website!!!!! Nafasi ya kujaza mapicha yasiyo na maana ipo, tena picha zenye poor scaling. Ila nafasi ya kuwasiliana na wateja hakuna. Mko serious kweli nyie!!!!!?. Kuna haja gani ya kuweka picha ya hizo ndege.......kwani mnadhani hatuamini kama mnazo hizo ndege. Media coverage yake ilikuwa kubwa kuliko, kabla hata hazijafika nchini. Basi hata muangalie toka website za mashirika mengine ziko vipi mpate changamoto mbili tatu. Inaonekana hata kuchungulia hamchungulii kabisa. Inakera kwa kweli. Mtu unaenda online booking, unajaza kilakitu. Then haijulikani uelekee wapi, link ya ku-execute hiyo booking 'book a flight now' imekufa. Ni shida. Kwa dunia ya leo na biashara hii ya usafiri wa ndege, huwezi kujiweka pembeni na online booking.