ATCL: Miezi minne tumekusanya bilioni 9, tumetumia 80% ya makusanyo kulipa madeni

iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,437
14,924
FB_IMG_1490886998573.jpg
Hii ni biashara kichaa au?

Unakusanya bilioni 9,unalipa madeni unabakiza bilioni 1.4,hizo ulipe mshahara na gharama nyingine za uendeshaji ikiwemo mafuta,mshahara,ofisi na mengineyo.


Ni wazi hii kampuni inajiendesha kihasara na ulikuwa mradi hewa usio na uchambuzi wa kina.

Tangazo limeonyesha mapato kwa miezi 4,matumizi hayajaonyeshwa kwa muda huo.

Ni wastani wa bilioni mbili na point kwa mwezi,katika kila bilioni 1,ATCL imebakiza Tsh milioni mia mbili na point kwa mwezi ili kujiendesha,milioni 800 wametumia kulipa madeni


Tukumbuke ATCL inadaiwa bilioni 103

Chanzo: the citizen la leo
 
Kwa hiyo wasingenunua ndege madeni yangeisha?

Hujui kuwa kutolipa deni hakufuti deni?

Hujui kama dawa ya deni ni kulipa?

Hujui kuwa anayelipa madeni ni mteja mzuri ambaye anaweza kukopeshwa zaidi ili kupanua wigo wa kibiashara?

Kwa kukusaidia zaidi, hakuna biashara isiyokuwa na madeni lakini pia kwa kutumia ATCL nchi inapata multiply effect kwenye sekta nyingine kama utalii na hotel nchini

Kilicho cha muhimu kwa sasa ATCL inajiendesha mpaka inalipa madeni. Hii ni hatua kubwa sana kibiashara.
 
Bashite kama mimi sijaelewa....

"Unakusanya bilioni 9,unalipa madeni unabakiza bilioni 1.4,hizo ulipe mshahara na gharama nyingine za uendeshaj....."

Hizo Bil. 9 ni madeni ya nini?

Na hilo Deni la awali ni la nini? Kununulia Bombadier au deni la nyuma?
 
Mi nafikiri wako sahihi. Huwezi jiendesha au kijidanganya unapata faida kama una madeni. Na kulipa madeni haina.maana kampuni haipati faida. Ila watashindwa kuwekeza kwenye ukuaji wa kampuni mpaka hapo watakapokuwa wamemaliza madeni.
Ingekuwa vyema kama kwenye tangazo lao wangeweka mapato na matumizi,lazima ingeonyesha matumizi makubwa zaidi hata mara mbili
 
Bavicha mna mema. Sasa ulitaka wasilipe. Acha mambo ya kiswahili ndugu dawa ya deni ni kulipa si vinginevyo.
Ulichokiandika umeropoka. Mbona kilevi alikopa pesa nyingi na anazid kukupa? Yy km mr. Kilevi amelipa hilo deni?
Ningemuona wa maana sana alcohol angelipa madeni yote na kuiweka tz ktk hali ya kutokopa.
Tangu lini pombe ikaleta maendeleo?
 
Bavicha mna mema. Sasa ulitaka wasilipe. Acha mambo ya kiswahili ndugu dawa ya deni ni kulipa si vinginevyo.
Ulichokiandika umeropoka. Mbona kilevi alikopa pesa nyingi na anazid kukopa? Yy km mr. Kilevi amelipa hilo deni?
Ningemuona wa maana sana alcohol angelipa madeni yote na kuiweka tz ktk hali ya kutokopa.
Tangu lini pombe ikaleta maendeleo?
 
Ulichokiandika umeropoka. Mbona kilevi alikopa pesa nyingi na anazid kukupa? Yy km mr. Kilevi amelipa hilo deni?
Ningemuona wa maana sana alcohol angelipa madeni yote na kuiweka tz ktk hali ya kutokopa.
Tangu lini pombe ikaleta maendeleo?
Mku hata wafanya biashara wakawaida wanakopa mitaji kuendesha biashara, acheni roho za kwanini.
 
Back
Top Bottom