ATCL kwaendelea kufuka moshi ;WAFANYAKAZI WAAPA KUGOMA KUONDOA UONGOZI; | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ATCL kwaendelea kufuka moshi ;WAFANYAKAZI WAAPA KUGOMA KUONDOA UONGOZI;

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Feb 24, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Feb 24, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,547
  Likes Received: 5,755
  Trophy Points: 280
  ATCL kwaendelea kufuka moshi Send to a friend Wednesday, 23 February 2011 19:46 0diggsdigg

  Gedius Rwiza
  WAFANYAKAZI wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), wametishia kugoma wakishinikiza uongozi wao kuondolewa na kwamba, hawamtaki Mkurugenzi wa shirika hilo, David Mattaka.
  Mwananchi ilishuhudia mabishano makali kati ya uongozi wa ATCL na wafanyakazi hao, ambayo nusura yasababishe mkutano baina yao kuvunjika, baada ya wafanyakazi kutaka wanahabari waingie mkutanoni huku uongozi ukipinga na kuwatoa nje. “Hatutaki mkutano wetu uwe na waandishi wa habari kama vipi tunavunja mkutano, waambie watoke nje haraka sana,” alisikika akiamrisha kiongozi wa shirika hilo.

  Baada ya mabishano makali na kuonekana mkutano unataka kuvunjika kwa ajili ya waandishi, waliamua kuondoka na mkutano uliendelea kama kawaida.

  Hata hivyo, chanzo chetu cha habari kilieleza kuwa, mada kubwa iliyojadiliwa ni kutaka kufahamu taarifa zilizotoka kwa Waziri wa Uchukuzi, Omari Nundu, kwani kuna baadhi ya wafanyakazi waliotumwa kwa waziri kuona kama menejimenti iliyopo itaondolewa na ikibidi shirika liundwe upya.

  Kilieleza kuwa hivi sasa wafanyakazi wako tayari shirika liundwe upya, lakini wanahofia ajira zao huenda zisiendelezwe kutokana na menejimenti iliyopo ndio maana wanamtaka Mattaka kuondoka mara moja.

  Kilisema aliwahi kuondolewa kutokana na shirika hilo kuonekana linadorora na baadaye alirudishwa. “Tunashangaa ni kwanini mkurugenzi alirudishwa maana tangu aliporudi hakuna maendeleo yoyote, bali shirika linaendelea kudidimia siku hadi siku,” kilieleza chanzo chetu.

  Kilieleza kuwa kama hali itaendelea ilivyo sasa wataandamana hadi kwa Waziri Nundu kueleza kilio chao na kwamba, wanakosa maslahi yao ya msingi kutokana na menejimenti mbovu. Hata hivyo, jitihada za kuzungumza na Mattaka hazikufanikiwa baada ya mwandishi wa habari hizi kuzuiliwa kuingia ofisini kwake.
   
 2. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #2
  Feb 24, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,547
  Likes Received: 5,755
  Trophy Points: 280
  Hii mislaba ya kugoma ishapitwa na wakati ushauri wangu kama wana nia ya kweli waingie street tutkutane squre mnazimmoja garden..basi hili la mogomo kuna usaliti mwingi sana na wengi huishia kuinafikikuonekana wazuri kwa wakubwa na hapo hapo kwa watu wa chini...kwa ushauri tu msigome..ingawa mmechelewa mgmo autasaidia kitu zaidi ya kuundiwa tume nyenyekevu...na aliewahi kusikia matokeo ya tume aje hapa...
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Feb 24, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,547
  Likes Received: 5,755
  Trophy Points: 280

  mi nafikiri chanzo si tu mattaka..ni wafanyakazi kukaa chini na kufanya analysis nini tatizo la atcl..na kufangalia limekuwa chini ya mwekezaji mwenye hela saa kampuni ya south africa..alikufanikiwa..likarudishwa kwa wadau alikuwafanikiwa..j e nini tatizo zaidi...maana nakumbuka wakati wa uongozi wa wazungu wafanyakazi walitishia kugoma mpaaka kwenye magazeti na waandishi wakaitwa wakaishia kuondoka na bahasha za wawekezaji....baada ya pale ukaja uongozi wa wazawa ....origin tz...nao ikawa tatizo so turudi nyuma na mbele na je wakati wa southafrican airways kuna mabadiliko gan i yalitokea......,ilipokuja nyu management..nakumbuka nikiwa pale jmoll kuna rafiki wangu mmoja akanipigia siku iliporindima dm kaula atcl..wakashangilia watawezeshwa kama ppf.....ni wakati wa kila mmoja management na wafanyakazi kumrudia mungu na kuomba afanye anavyoweza...wakati wa kutetana na kupigana majungu si sasa na umepitwa na wakati....waungane na kuamua wanatakka nini na si kunyoosheana vidole...kweli yawezekana shirika linamatatizo je wewe unaonyoosha kidole kwa managament umefanya nini kulifikisha hapo..na kama uliona matatizo haya kama niilivyosoma angu mwanzo uoni wewe ni mmuuwaji kuliko hiyo management..kila mtu achukue msalaba wake ajiulize nimeifanyia nini na wakati wote wa matatizo nimeifanyia nini....rais mmoja wa marekani alisema usisubiri marekani itakufanyia nini bali wewe umeifanyia nini??....

  Nawatakia amani njema
   
 4. M

  Mzee wa Usafi JF-Expert Member

  #4
  Feb 24, 2011
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 634
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Tatizo la ATCL linaeleweka ila kila mtu hataki kumfunga paka kengele....Bwana Mufuruki alipoona business proposal yake imepigwa chini, yeye pamoja na Managing director (Bwana Sangwene, kutoka kwa mzee Madiba) waliamua kuachia ngazi kuwapisha wachumia tumbo. Ni lazima tukubali ukweli huu kwa hali ilivyo sasa hakuna mtu wala menejimenti inayo weza kuendesha ATCL kwa faida. ATCL ina ndege 5, wafanyakazi 1300. Precision air ina ndege 8 na wafanyakazi wanaokaribia 600. Kati ya hao wafanyakazi 150 na wabeba mizigo ambayo mishahara yao sio mzigo mkubwa kwa kampuni. Nina shaka kama technical staff, pilots na mafundi kama wanazidi 50...pia wanaendesha kwa faida. ATCL wanatakiwa kupunguza wafanyakazi, ili wabaki wale wanaohitajika kwa ajili ya manufaa kwa shirika....wanunue ndege na wawe na menejimenti yente vision.. kwa Mataka hata ukimpa BAA ataiua tu..... viginevyo tuendelee kupiga blah blah tu
   
 5. Kiherehere

  Kiherehere JF-Expert Member

  #5
  Feb 24, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,804
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  wagome kwa ajili ya nini?? maana mi naona hapo hamna kitu kilichobaki bora waende wakapumzike tu nyumbani... kwanza hata mishahara sijui wanaipata wapi??
   
 6. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #6
  Feb 24, 2011
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,508
  Likes Received: 2,750
  Trophy Points: 280
  Hivi hii ATCL inasurvive vipi?? Mimi naona hiyo kampuni ni mzigo tu kwa walipa kodi sawa na IPTL, Downs etc.
   
Loading...